Ethiopia
au
Uhabeshi
(
Kiamhara
: ?????
Ityopp'ya
) ni nchi ya
Afrika ya Mashariki
iliyoko kwenye
Pembe ya Afrika
.
Nchi zinazopakana na Ethiopia ni
Sudan
na
Sudan Kusini
upande wa
magharibi
,
Eritrea
na
Jibuti
kaskazini
,
Somalia
mashariki
na
Kenya
upande wa
kusini
.
Ni nchi ambayo ina
historia
ya pekee
Afrika
na hata
duniani
kwa ujumla.
Ethiopia ni moja ya nchi mbili za
Afrika
ambazo hazikutawaliwa na
wakoloni
wakati walipong’ang’ania Afrika. Nchi nyingine ni
Liberia
. Kabla ya
Vita Kuu ya Pili ya Dunia
Ethiopia ilivamiwa na
Waitalia
(
1936
) lakini ilipata
uhuru
wake tena baada ya miaka michache.
Jina
Asili
ya
jina
"
Ethiopia
" haijulikani. Kuna maelezo mbalimbali lakini yote yanakosa uhakika. Hilo ni sawa pia kwa jina la pili la kihistoria ambalo ni "Habasha" ilikuwa "Uhabeshi".
Ethiopia mara nyingi linaelezwa kuwa neno la
Kigiriki cha Kale
Α?θιοπ?α
Aithiopia
lililotokana na Α?θ?οψ "Aithiops" ; maana yake "uso" (?ψ) "kuwaka" (αιθw) hivyo labda "uso uliochomwa" ama
sura
nyeusi
. Lakini jina hili halikumaanisha hasa nchi ya Ethiopia ya leo lakini nchi zote zenye watu wenye rangi nyeusinyeusi. Kwa muda mrefu watu wa
Ulaya
waliita Afrika yote kwa jina "Ethiopia". Pia si wazi kama neno la Kiafrika lenye maana tofauti limechukuliwa na
Wagiriki
kwa maana ya neno lao la "aithiops".
Nchi yenyewe ilijulikana kwa muda mrefu wa historia yake kwa jina la
Habasha
. Habasha ilikuwa jina la
Kiarabu
kwa ajili ya nchi ikaingia kama "Uhabeshi" katika Kiswahili au "Abisinia" katika
lugha
za
Ulaya
. Asili ya jina hilo haliko wazi; wengine husema ni katika lugha ya kale ya nchi yenyewe kumaanisha "nchi kwenye
nyanda za juu
"; tena wengine wanadai kwamba jina limetoka
Uarabuni
wa kusini lilipokuwa jina la
kabila
moja lililohamia na watu walioleta
lugha za kisemiti
Ethiopia.
Jiografia
Tazama pia
:
Orodha ya mito ya Ethiopia
Ethiopia ina eneo la
kilometa mraba
1,127,127 (
maili mraba
435,071). Nchi yenyewe ni mojawapo ya nchi za
Pembe ya Afrika
upande wa mashariki.
Nchini Ethiopia kuna milima mirefu; sehemu kubwa ya nchi inaundwa na
Nyanda za juu za Ethiopia
zilizotenganishwa na
Bonde la Ufa la Afrika Mashariki
, ambalo limepasua kutoka kusini - magharibi kwenda kaskazini ? mashariki na kuzungukwa na
mbuga
maeneo yaliyo chini.
Mabonde
na milima hasa nchini Ethiopia yanaathiri
hali ya hewa
,
udongo
,
mimea
, na makazi ya watu.
Ukweo wa milima na eneo la kijiografia vinasababisha aina mbili za hali ya hewa: eneo lililopoa liko zaidi ya ukweo wa
mita
2,400 (
futi
7,900) ambapo
vipimo vya joto
ni kati ya kuganda na 16°
C
(32°?61°
F
); vipimo vya joto kwa ukweo wa mita 1,500 na 2,400 (futi 4,900?7,900) joto ni 16°C hadi 30°C (61°?86°F); joto zaidi liko chini ya mita 1,500 (futi 4,900) ni
hali ya hewa
ya
tropiki
na hali ya hewa ya
ukame
na joto saa za mchana ni 27°C mpaka 50°C (81°?122°F).
Mvua
ya kawaida ni kuanzia kati ya Juni mpaka kati ya Septemba lakini eneo la milima ya kusini mvua hunyesha zaidi ikianzia na mvua kidogo ya Februari ama Machi.
Ethiopia ni nchi ambayo ina
ikolojia
tambakazi.
Ziwa Tana
, ambalo liko kaskazini mwa nchi, ndilo
chanzo
cha
Mto
Naili ya Buluu
(kwa
Kiarabu
: Bahr al Zraq). Eneo la mto huo lina aina za
wanyama
za pekee kama
Gelada - nyani
,
Walia ibeka
na pia
Mbwa mwitu
.
Historia
Historia ya awali
Historia ya
binadamu
katika Ethiopia ilianza mapema kabisa.
Mifupa
ya kale kabisa ya
viumbe jamii ya watu
imepatikana katika nchi hii kwa sababu zilihifadhiwa katika
mazingira
yabisi
ya nchi.
Wataalamu
wengi huamini ya kwamba Ethiopia (pamoja na
Kenya
na
Tanzania
) inaweza kuwa mahali ambako watu wa aina ya
Homo Sapiens
walianza kupatikana duniani.
Kuna ma
baki
mbalimbali ya ki
utamaduni
yanayochunguzwa na
akiolojia
, lakini sehemu kubwa ya nchi haijaangaliwa bado kitaalamu. Inaonekana kwamba katika
karne
za
K.K.
kulikuwa na
uhusiano
wa karibu na
Uarabuni
kwa sababu lugha za Kiethiopia ni karibu na lugha za upande mwingine wa
Bahari ya Shamu
. Inaaminiwa kwamba watu kutoka Uarabuni Kusini walihamia Ethiopia na kuleta lugha yao huko.
Biblia
ina taarifa juu ya
ziara
ya
malkia wa Sheba
aliyemtembelea
mfalme
Suleimani
wa
Yerusalemu
.
Milki ya Sheba
imedaiwa kuwepo ama Ethiopia au
Yemen
na wengine huamini ya kwamba ilikuwa
dola
la pande zote mbili za
mlangobahari
wa
Bab el Mandeb
unaotenganisha
Eritrea
ya leo na Uarabuni Kusini.
Historia ya kale
Milki
ya kwanza ya Ethiopia inayoweza kutajwa kutokana na mabaki ya ma
jengo
na
maandishi
ilikuwa milki ya
D'mt
(pia: Da'amot) katika Ethiopia ya kaskazini pamoja na
Eritrea
ya leo. Kuna mabaki ya
hekalu
la
Yeha
pamoja na ma
kaburi
ambako majina ya wafalme kadhaa yamehifadhiwa kwa maandishi kwenye
mawe
.
Lugha
ilikuwa karibu sana na lugha za kale za
Uarabuni
. Ilikuwa na
athira
juu ya sehemu za kaskazini ya Ethiopia kwa kipindi kikubwa cha
milenia ya 1 KK
.
Ilifuata milki kubwa ya
Aksum
, iliyoanzishwa wakati wa kuzaliwa
Yesu
.
Ufalme wa Aksum
ulikuwa milki ya kwanza kutawala maeneo makubwa ya Ethiopia.
Nabii
Mwajemi
Mani
aliuweka
Ufalme wa Aksum
kwa
utukufu
sawa na
Roma
,
Uajemi
na
Uchina
kama nchi zilizokuwa na nguvu duniani
karne ya 3
BK
, wakati yeye alipoishi.
Ilikuwa
karne ya 4
BK
ambapo
Frumentius
, mtu
Msiro
-
Mgiriki
aliyekuwa amepotelea
baharini
kutokana na kuzama kwa
jahazi
, alishikwa na Wahabeshi na kupelekwa
kortini
na baadaye kumuongoa mfalme
Ezana
kuingia
Ukristo
. Kwa hiyo Wahabeshi wakampa jina
Abba Selama
. Kwa muda mfupi dini hiyo mpya ilienea kote
[4]
.
Mara nyingi
karne ya 6
Aksum ilitawala eneo la
Yemeni
ng'ambo ya
Bahari ya Shamu
.
Aksum ilistawi hasa kutokana na
biashara
kati ya
Mediteranea
na
Bara Hindi
iliyopita kwenye
mlangobahari
wa
Bab el Mandeb
ikatumia
bandari
ya
Adulis
(karibu na
Massawa
ya leo nchini Eritrea).
Uenezi wa
Uislamu
ulivuruga biashara hiyo na Aksum ilipoteza
utawala
juu ya
pwani
. Kuporomoka kwa uwezo wa kibiashara kunaonekana katika kusimamishwa kwa
uchapaji
pesa
ya wafalme wa Aksum katika
karne ya 7
. Nchi ilishambuliwa pia kutoka milki za barani.
Mabaki ya ufalme wa Aksum yaliharibiwa mnamo mwaka
900
wakati na
malkia Gudit
(au Judith) aliyekuwa ama
Myahudi
ama kiongozi wa makabila ya Kipagani kutoka
nyanda za juu
.
Milki ya Ethiopia
Kiongozi wa kabila la Agaw alimwoa
binti
wa mfalme wa mwisho wa Aksum akaanzisha
nasaba
ya Zagwe na kuunda upya ufalme wa Kikristo katika nyanda za juu.
Kitovu
cha ufalme huu kilipelekwa zaidi mbali na pwani.
Nasaba hii ilipinduliwa mnamo
1270
na
Yekuno Amlak
aliyetumia jina la kifalme
Tasfa Iyasus
. Alianzisha nasaba iliyojiita "Wa Suleimani" kwa kudai ilikuwa
ukoo
wa
mwana
wa mfalme Suleimani na malkia wa Sheba. Tasfa Iyasus alitumia
cheo
cha
Negus Negesti
("Mfalme wa Wafalme").
Enzi ya Mfalme
Lebna Dengel
, Ethiopia iliweza kuwasiliana na nchi za Ulaya na kudumisha
ubalozi
na nchi kama
Ureno
. Lakini, Mfalme
Susenyos
alipojiunga na
Kanisa Katoliki
mwaka
1622
, chakari na misukosuko ilifuata.
Wamisionari
Wajesuiti
walichukiwa na waamini wa
Kanisa la Ethiopia
, na katika hiyo
karne ya 17
Susenyos mwana wa Mfalme
Basil
aliwafukuza wanamisheni hao.
Baadaye
Waoromo
wakaanza kuasi
amri
ya
Kanisa la Ethiopia
na kutafuta njia za
dini
yao, eneo hili la Uhebeshi.
Mambo hayo yote yalifanya Ethiopia itengwe
miaka ya 1700
. Wafalme wakawa kama
wakurugenzi
, ambao waliamriwa na ma
sharifu
kama Ras
Mikael Sehul
wa
Tigrinya
. Ethiopia ilitoka kutoka utengo kwa kufuatia
misheni
ya
Uingereza
kufika Ethiopia na kukamilisha
muungano
kati ya nchi hizi mbili; lakini, hadi milki ya
Tewodros II
ndipo Ethiopia ilipoanza tena shauri za Duni.
Miaka ya 1880
ilikuwa miaka ya Ulaya kung’ang’ania
ukoloni
Afrika ambapo Waitalia na Waingereza walitafuta kutawala eneo la
Assab
, bandari iliyoko karibu na
mdomo
wa bahari ya Shamu. Bedari ya Kusini, karibu na kiingilio cha bahari ya Shamu, ilinunuliwa na Waitalia kutoka
sultani
mwenyeji Machi
1870
ambayo mwaka
1882
ilizaa
koloni
la
Eritrea
.
Haya yalizua magombano kati ya Waethiopia na Waitalia na
Vita vya Adowa
mwaka
1896
, ambapo Waethiopia walishtua dunia kwa kupiga nguvu za wakoloni na kulinda
madaraka
yao kwa
uongozi
wa
Menelik II
.
Italia
na Ethiopia zilisaini
mkataba wa amani
tarehe
26 Oktoba
1896.
Karne ya 20 hadi leo
Karne ya 20
miaka ya kwanzakwanza ilimilikiwa na Mfalme
Haile Selassie
, aliyechukua nafasi ya kuendeleza Ethiopia mpaka uongozi wake ulipokatizwa kwa
Vita ya pili ya Uhabeshi na Italia
(
1936
).
Waingereza
na wazalendo wa Jeshi la Ethiopia wakakomboa nchi mwaka
1941
, na Waingereza kukiri madaraka ya Ethiopia kwa
mkataba wa Uingereza na Ethiopia
mnamo
Desemba
1944
.
Milki ya Haile Selassie ilikoma mwaka
1974
, ambapo
Wakomunisti
wa "
Derg
" walimpindua na kuanzisha
serikali ya kikomunisti
chini ya
Mengistu Haile Mariam
.
Mapinduzi hayo yalifuatwa na
msukosuko
wa
vita
na migogoro pamoja na
ukame
na shida za
wakimbizi
.
Mwaka
1977
Somalia
ilivamia eneo la
Ogaden
(
Vita vya Ogaden
), lakini Ethiopia iliweza kuwafukuza Wasomali kwa msaada wa vifaa vya kijeshi vya
Urusi
, na majeshi ya
Kuba
,
Ujerumani Mashariki
na
Yemeni
. Usaidizi mwingi kutoka
Nchi za Kikomunisti
uliwezesha Ethiopia kudumisha mojawapo ya majeshi kubwa Afrika.
Lakini hii haikuzuia
ukereketwa
wa jimbo la Eritrea na
Tigray
, ambapo ukame wa mwaka
1985
na
mapinduzi
ya
siasa
hasa kwa Kambi za
Ujamaa
, zilileta uongozi wa Derg
1991
kukoma. Chama cha kukomboa Eritrea (EPLF) na
Chama cha Mapinduzi cha Kidemokrasi Ethiopia
(EPRDF), ziliungana kukomboa Ethiopia, wengi wa
wanamgambo
wakiwa wanaharakati wa Eritrea.
Mwaka
1993
jimbo la
Eritrea
likawa huru kutoka Ethiopia, kufuatia
kura ya maoni
iliyofanywa ili kumaliza vita hivyo vilivyodumu miaka 20, mmojawapo kati ya migogoro ya muda mrefu zaidi Afrika.
Mwaka
1994
Ethiopia kaiweka
Katiba
mpya ambayo ilileta
uchaguzi
wa ki
demokrasia
.
Mwaka
1998
magombano ya mipaka na Eritrea yalileta
Vita vya Eritrea na Ethiopia
ambayo vilidumu hadi
Juni
2000
. Vita hivyo vilileta
uvivu
wa uchumi na nguvu ya muungano unaongoza nchi.
Siasa
Uchaguzi wa Ethiopia ulipitisha wanabaraza 547 Bungeni. Baraza hilo la bunge lilijumuika Juni 1994 na kupitisha katiba mpya ya Jimbo la Demokrasia ya Jamhuri ya Ethiopia mnamo Desemba 1994. Uchaguzi huu ulikuwa wa kwanza kuchagua wanabaraza wa kitaifa kwa sifa bungeni na wanabaraza wa majimbo mnamo Mei na Juni
1995
. Vyama vingi vya upinzani viligoma kushiriki uchaguzi. Ushindi ulichukuliwa na
Chama cha Mapinduzi cha Kidemokrasi cha Watu wa Ethiopia
(EPRDF). Umoja wa Mataifa ukasema vyama vya upinzani vingeweza kushiriki uchaguzi kama zingetaka.
Serikali ya Majimbo ya Demokrasia ya Jamhuri ya Ethiopia ilichukua mamlaka mnamo Agosti 1995. Rais wa kwanza
Negasso Gidada
. EPRDF ikaongoza serikali na Waziri Mkuu
Meles Zenawi
ambaye aliunga mkono majimbo ya kikabila, na kuwapa madaraka viongozi wa kikabila. Ethiopia sasa ina majimbo 9 ambayo yana serikali ya
madaraka ya shirika
, na hata majimbo haya yanakubaliwa kutoza ushuru na kutumia
akiba ya ushuru
. Hata hivyo, uhuru wa habari na kisiasa bado umefinywa.
Serikali ya Zenawi ilichaguliwa tena mwaka 2000 kwa uchaguzi wa kwanza wa Kidemokrasia, Rais akiwa
Girma Wolde-Giorgis
.
Kutoka
1991
, Ethiopia imetafuta urafiki zaidi na
Marekani
na
Umoja wa Ulaya
, ili kuweza kukopa fedha za kusaidia uchumi wake na pia kutoka
Benki ya Dunia
.
Mwaka
2004
, serikali ilianza kuhamisha watu kutoka maeneo ya ukame wakisema hii itazuia njaa.
[1]
.
Uchaguzi
mwingine wa Ethiopia ulikuwa tarehe
15 Mei
2005
, ambao ulivutia wapigakura kiasi cha juu zaidi, asilimia 90% ya wananchi waliojiandikisha. Watazamaji wa
Umoja wa Ulaya
walidai uchaguzi haujafikia kiwango cha kimataifa, lakini
Umoja wa Afrika
ulitoa ripoti tarehe
14 Septemba
kwamba Waethiopia walionyesha kujitokeza na kuheshimu demokrasia, halafu tarehe 15 Septemba, Carter Center, ikasema matokeo ya uchaguzi yaaminika na kuonyesha ushindani wa kisiasa. Uangalizi na ushuhuda wote ulimalizia kuranki Uchaguzi wa Ethiopia na kesi nyingine waipa, asilimia 64% ya matokeo mazuri, na vizuri zaidi kulingana na kesi nyingine 24%.
Katika
Uchaguzi wa Ethiopia, 2005
EPRDF ilitokea iking’ang’ania uongozi.
Tarehe za kwanza za Juni na tena Novemba,
polisi
kwa amri ya EPRDF wakafyatua
risasi
na kuua watu kwa
maandamano
yaliyokuwa yakipinga
matokeo ya kura
.
Ni kwamba vyama vya upinzani vililalamika kwamba EPRDF iliiba kura na kuwazisha wananchi na kusema baraza 299, wapata hitilafu ya wizi wa kura. Hayo yote yalichunguzwa na Watazamaji wa Uchaguzi wa kimataifa na pia Kamisheni ya Uchaguzi Ethiopia.
Matokeo ya uchunguzi huo kama haijatokea mnamo
Juni 2005
, wanafunzi wa
chuo kikuu
walianza maandamano wakisaidiwa na wanamgambo wa Muungano wa Vyama vya Upinzani. Lakini serikali kwa kutoa amri ya kukomesha maaandamano, mnamo
8 Juni
, watu 26 waliuliwa mjini
Addis Ababa
kwa msukosuko wa maandamano na wengine wengi kushikwa.
Mnamo
5 Septemba
2005
, Kamisheni ya Uchaguzi Ethiopia, ilitoa matokeo na kusema kwamba (EPRDF) kashinda uchaguzi na kwa hiyo iongoze serikali. Lakini vyama vya upinzani viliongezea viti bungeni kutoka 12 mpaka 176. Muungano wa umoja na demokrasia ulishinda viti vyote vya Addis Ababa, kwa Bunge la Taifa na
Baraza la mtaala
.
Maandamano yalizuka tena mitaani
1 Novemba
, ambapo vyama vya upinzani viliitisha mgomo kwa jumla na pia kwa Bunge mpya, wakatae matokeo ya uchaguzi. Polisi tena walijaribu kuzuia maandamano hayo na watu 42 wakafa kwa misukosuko mjini Addis Ababa. Polisi saba pia wakafa na mwingine pia kafa kutokana na majeruhi ya mlipuko wa
bomu
. Tope la watu walishikwa na kufungwa jela. Februari 2006 watu elfu sita bado walikuwa jela wakingoja hukumu Machi.
Mnamo 14 Novemba, Bunge la Ethiopia lilipitisha mkataba kuimarisha Kamisheni huru na kuchunguza visa vya 8 Juni na tarehe 1 na tarehe 2 Novemba. Februari 2006 Waziri mkuu wa Uingereza
Tony Blair
, alitamka kwamba, EPRDF kashinda kura, lakini angetaka kuona Ethipia ikitatua shida zake yenyewe na iendelee katika njia ya demokrasia.
[2]
.
Majimbo ya Kujitawala
Ethiopia imegawiwa katika
majimbo
9 ya
mamlaka
ya kikabila (
kililoch
; umoja:
kilil
), na maeneo 68.
Zaidi ya hayo kuna maeneo ya miji miwili (
astedader akababiwoch
; umoja:
astedader akababi
):
Addis Ababa
na
Dire Dawa
.
Watu
Idadi
ya wakazi ilikadiriwa kuwa 113,656,596 (
2022
) ambao wanaongezeka kwa
asilimia
2.88 kwa mwaka.
Ethiopia ina makabila zaidi ya 80 yenye utamaduni tofautitofauti. Watu wengi huongea
lugha za Kisemiti
na
lugha za Kikushi
.
Waoromo
(34.49%),
Waamhara
(26.89%),
Wasomali
(6.20%) na
Watigrinya
(6.07%) ni zaidi ya 73% ya wananchi wote. Kumbe kuna makabila mengine yenye watu wachache kiasi kama 10,000.
Lugha
Ethiopia ina lugha 84 za kienyeji (angalia
Orodha ya Lugha za Ethiopia
). Mifano fulani ni kama ifuatavyo:
Kiingereza
ndiyo lugha ya kigeni inayoongelewa zaidi na kufunzwa katika
shule ya upili
.
Kiamhara
ilikuwa lugha ya ufundishaji katika
shule ya msingi
lakini sasa sehemu nyingi nafasi yake imeshikwa na
Kioromo
na
Kitigrinya
.
Dini
Wakristo
, ambao ndio wengi (67.3%, kati yao
Waorthodoksi wa mashariki
43.8%), wanaishi hasa kwenye milima, na
Waislamu
(31.3%) na
Wapagani
(0.6%) wengi wanaishi kwenye mabonde.
Ukristo
Ufalme wa Aksum
ulikuwa milki na nchi ya kwanza kukubali
Ukristo
, ambapo
askofu
Frumentius
wa
Taya
, aliyetumwa na
Atanasi
wa
Aleksandria
kuiinjilisha
nchi, alimuongoa
Ezana wa Aksum
katika
karne ya 4
. Kwa hiyo Wahabeshi wakampa jina
Abba Selama
. Kwa muda mfupi dini hiyo mpya ilienea kote
[5]
.
Labda Frumentius alifika tayari na
wamonaki
kama
wamisionari
. Lakini
umonaki
hasa ulianza mnamo mwaka
500
walipofika wamonaki tisa wenye asili ya
Siria
waliotokea
Misri
katika
monasteri
za
Pakomi
.
Hivyo mpaka leo mtindo huo ndio unaotawala kati ya umati wa wamonaki wa Ethiopia, wakati
wakaapweke
ni wachache, ingawa hawajawahi kukosekana. Athari za Siria na Misri zinajitokeza katika mambo mengi.
Wamonaki wanaishi katika vibanda vya binafsi wakikutana kwa
sala
tu. Wamonaki
wanawake
(kawaida ni
wajane
) wanaishi jirani na monasteri ya kiume wakiitegemea kiroho na kiuchumi.
Uislamu
Uislamu
nchini Ethiopia unapatikana kutoka mwanzo wa dini hiyo; ambapo
nabii
Muhammad
aliwaambia Waislamu waepuke kuuliwa
Maka
kwa kukimbilia Uhabeshi, ambayo ilitawaliwa na Mfalme Mkristu.
Hata
utamaduni
wa Kiislamu wasema
Bilal
, mfuasi wa Nabii Muhammad, alikuwa ametokea Ethiopia.
Uyahudi
Wayahudi
, ambao wanaitwa Beta Israeli a Wafalasha, walioishi Ethiopia tangu karne nyingi, wengi wao wamehamia
Israeli
hasa katika
karne ya 20
.
Dini za jadi
Mbali na dini hizo za kimataifa, kuna wafuasi wa
dini za jadi
za
Kiafrika
.
Utamaduni
Mnamo Aprili
2005
,
Mnara wa Aksum
, mojawapo ya dafina za kidini Ethiopia, ulirudishwa na Waitalia
[6]
ambao waliunyakua mwaka
1937
na kuupeleka
Roma
. Italia ikakubali kuurudisha mnamo
1947
kulingana na mkataba wa
Umoja wa Mataifa
.
Ethiopia ndiyo Nyumba ya kiroho ya
Mwendo wa Rastafari
, ambao wanaamini Ethiopia ni
Zion
. Warastafari wamuona mfalme Haile Selassie I kama
Yesu
.
Sikukuu
Ona pia:
Kalenda ya Waethiopia
Uchumi
Ethiopia imebaki
nchi fukara
mojawapo: Waethiopia wengi wanapewa
chakula cha msaada
kutoka ng’ambo.
Baada ya mapinduzi ya mwaka
1974
, uchumi wa Ethiopia ulikuwa
uchumi wa kijamaa
: amri ya uchumi iliwekwa na jimbo, na upande mkubwa wa uchumi uliwekwa kwa jamii, kutoka viwanda vyote vya kisasa,
kilimo cha biashara
,
taasisi za kukopesha
na mashamba yote na mali yote ya kukomboa.
Kutoka kati ya
1991
, uchumi ulianza kutolewa katika
ujamaa
na kuendekeza
uchumi wa soko huria
, serikali inasisitiza uchumi wa rasilimali ili kuzuia uvivu wa uchumi uliojitokeza wakati wa amri ya ujamaa. Mwaka
1993
,
Ubinafsishaji
wa kampuni kaanza, viwanda, mabenki, ukulima,
biashara za ndani
na
biashara za kimataifa
.
Kilimo ni karibu asilimia 41% ya
mapato ya uchumi
(GDP), ambayo ni asilimia 80 ya biashara ya kimataifa, na asilimia 80 ya wananchi wanategemea kilimo.
Mambo mengi ya biashara hutegemea ukulima, wauzaji, viwanda vya kufunganya na kuuza nje mavuno ya ukulima. Mavuno yanayouzwa nje mengi yanatolewa na
wakulima wa kiasi
binafsi. Wanazalisha
kahawa
,
nafaka
(hasa maharagwe),
mbegu za mafuta
,
viazi
,
miwa
, na
mboga
.
Biashara ya nje hasa ni ya kuuza mazao, kahawa ikiwa ndiyo inayoleta pesa nyingi za kigeni.
Mifugo
ya Ethiopia inaaminika kuwa ndiyo wengi zaidi Afrika. Mnamo
1987
ilihesabika kuwa asilimia 15 ya mapato ya uchumi yanatokana na mifugo.
Michezo
Ethiopia ni nchi mojawapo inayotoa
wanariadha
wazuri zaidi duniani, hasa kama wa
mbio
wa
masafa ya kati
na
masafa marefu
.
Kenya
na
Morocco
ni wapinzani wa Ethiopia kwa
Michezo ya mabingwa wa Dunia
na
Olimpiki
kwa masafa ya kati na marefu.
Machi
2006
, Waethiopia wawili walitamalaki mbio za masafa marefu, kwa jina wakiwa:
Haile Gebreselassie
(Bingwa wa Dunia na Olimpiki) aliyevunja
rekodi
ya
kilometa
10 na sasa pia kilomita 20, Nusu
Marathoni
, na rekodi ya kilomita 25, na kijana
Kenenisa Bekele
(bingwa wa dunia, mbio za majira (bara), na pia bingwa wa olimpiki), anayeshikilia
Rekodi za Dunia
za
mita
5,000 na 10,000.
Huko nyuma Ethiopia ilitoa mwanariadha maarufu katika historia ya mchezo huu duniani,
Abebe Bikila
.
Tazama pia
Marejeo
- ↑
1.0
1.1
"Ethiopia"
.
The World Factbook
(kwa Kiingereza) (toleo la 2024).
Shirika la Ujasusi la Marekani
. Iliwekwa mnamo
23 Machi
2024
.
{{
cite web
}}
: CS1 maint: date auto-translated (
link
)
- ↑
2.0
2.1
2.2
2.3
"World Economic Outlook Database, October 2023 Edition. (Ethiopia)"
.
IMF.org
.
International Monetary Fund
. 10 Oktoba 2023
. Iliwekwa mnamo
12 Oktoba
2023
.
{{
cite web
}}
: CS1 maint: date auto-translated (
link
)
- ↑
"Human Development Report 2021/2022"
(PDF)
(kwa Kiingereza).
Mradi wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa
. Septemba 8, 2022
. Iliwekwa mnamo
Septemba 8,
2022
.
{{
cite web
}}
: CS1 maint: date auto-translated (
link
)
- ↑
https://www.avvenire.it/agora/pagine/ritrovate-le-chiese-piu-antiche-dell-africa-subsahariana
- ↑
https://www.avvenire.it/agora/pagine/ritrovate-le-chiese-piu-antiche-dell-africa-subsahariana
- ↑
http://news.bbc.co.uk/1/hi/world/africa/4458105.stm
- Zewde, Bahru (2001).
A History of Modern Ethiopia, 1855?1991
(toleo la 2nd). Athens, OH: Ohio University Press.
ISBN
0-8214-1440-2
.
- Selassie I., Haile
(1999).
My Life and Ethiopia's Progress: The Autobiography of Emperor Haile Selassie I
. Translated by Edward Ullendorff. Chicago: Frontline.
ISBN
0-948390-40-9
.
- Deguefe, Taffara (2006).
Minutes of an Ethiopian Century
, Shama Books, Addis Ababa,
ISBN 99944-0-003-7
.
- Hugues Fontaine,
Un Train en Afrique. African Train
, Centre Francais des Etudes Ethiopiennes / Shama Books. Edition bilingue francais / anglais. Traduction : Yves-Marie Stranger. Postface : Jean-Christophe Belliard. Avec des photographies de Matthieu Germain Lambert et Pierre Javelot. Addis Abeba, 2012,
ISBN 978-99944-867-1-7
. English and French.
[3]
- Henze, Paul B. (2004).
Layers of Time: A History of Ethiopia
. Shama Books.
ISBN
1-931253-28-5
.
- Marcus, Harold G. (1975).
The Life and Times of Menelik II: Ethiopia, 1844?1913
. Oxford, U.K.: Clarendon.
Reprint, Trenton, NJ: Red Sea, 1995.
ISBN 1-56902-009-4
.
- Marcus, Harold G. (2002).
A History of Ethiopia
(toleo la updated). Berkeley: University of California Press.
ISBN
0-520-22479-5
.
- Mauri, Arnaldo (2010).
Monetary developments and decolonization in Ethiopia
, Acta Universitatis Danubius Œconomica, VI, n. 1/2010, pp. 5?16.
[4]
and WP
[5]
- Mockler, Anthony (1984).
Haile Selassie's War
. New York: Random House.
Reprint, New York: Olive Branch, 2003.
ISBN 1-902669-53-3
.
- Murphy, Dervla (1968).
In Ethiopia with a Mule
. London: Century, 1984, cop. 1968.
N.B
.: An account of the author's travels in Ethiopia. 280 p., ill. with a b&w map.
ISBN 0-7126-3044-9
- Rubenson, Sven (2003).
The Survival of Ethiopian Independence
(toleo la 4th). Hollywood, CA: Tsehai.
ISBN
0-9723172-7-9
.
- Siegbert Uhlig, et al. (eds.) (2003).
Encyclopaedia aethiopica
, Vol. 1: A-C. Wiesbaden: Harrassowitz Verlag.
- Siegbert Uhlig, et al. (eds.) (2005).
Encyclopaedia aethiopica
, Vol. 2: D-Ha. Wiesbaden: Harrassowitz Verlag.
- Siegbert Uhlig, et al. (eds.) (2007).
Encyclopaedia aethiopica
, Vol. 3: He-N. Wiesbaden: Harrassowitz Verlag.
- Siegbert Uhlig & Alessandro Bausi, et al. (eds.) (2010).
Encyclopaedia aethiopica
, Vol. 4: O-X. Wiesbaden: Harrassowitz Verlag.
- Alessandro Bausi & S. Uhlig, et al. (eds.) (2014).
Encyclopaedia aethiopica
, Vol. 5: Y-Z and addenda, corrigenda, overview tables, maps and general index. Wiesbaden: Harrassowitz Verlag.
- Abir, Mordechai (1968).
Ethiopia: The Era of the Princes; The Challenge of Islam and the Re-unification of the Christian Empire (1769?1855)
. London: Longmans.
- Beshah, Girma and Aregay, Merid Wolde (1964).
The Question of the Union of the Churches in Luso-Ethiopian Relations (1500?1632)
. Lisbon: Junta de Investigacoes do Ultramar and Centro de Estudos Historicos Ultramarinos.
{{
cite book
}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (
link
)
- Munro-Hay, Stuart (1991).
Aksum: An African Civilization of Late Antiquity
(PDF)
. Edinburgh: University Press.
ISBN
0-7486-0106-6
. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
(PDF)
mnamo 2013-01-23
. Iliwekwa mnamo
2016-03-30
.
- Valdes Vivo, Raul (1977).
Ethiopia's Revolution
. New York: International Publishers.
ISBN
0717805565
.
Viungo vya nje
Serikali
Habari
Masomo
Maelekezo
Utalii
Lugha
Mashirika ya msaada
Mengineyo
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Afrika
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Ethiopia
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|