Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Shule ya msingi
ni hatua ya kwanza katika mfululizo wa masomo katika nchi nyingi.
Masomo ya msingi huchukua kati ya miaka 5 hadi 8 ya kwanza ya
elimu rasmi
.
Kwa jumla
elimu ya juu
hujumulisha miaka 6-8 ya masomo kuanzia mwaka wa tano au sita, lakini hutofautiana kati ya nchi na nchi.
Asilimia
70 ya
watoto
waliotimu
umri
wa kujiunga na
shule
hujiandikisha katika masomo ya msingi kote
ulimwenguni
na viwango hivi vinaongezeka.
Chini ya mipango ya Elimu kwa wote inayoendeshwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la
Umoja wa Mataifa
(
UNESCO
), nchi nyingi zina nia ya kufanikisha uandikishaji katika elimu ya msingi ifikapo mwaka
2015
, na katika nchi nyingi, ni lazima kwa watoto kupata elimu ya msingi.
Kwa nchi ya
Tanzania
ni tofauti na nchi nyingine
duniani
kwani huanzia awali hadi darasa la saba, baada ya hapo unajiunga na
elimu ya sekondari
kwa miaka 6 yaani kidato cha kwanza hadi cha sita, baada ya hapo unajiunga na
chuo kikuu
. Serikali inazidi kujenga shule vijijini kwa sababu watu wengi huko hawana elimu; lakini bado kuna suala la ubora.