Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Umoja wa Afrika (UA)
(kwa
Kiingereza
:
African Union (AU)
;
Kifaransa
:
Union Africaine (UA)
;
Kihispania
:
Union Africana (UA)
;
Kireno
:
Uniao Africana (UA)
)
[1]
ni muungano wa nchi 55 za
Afrika
ulioanzishwa mnamo Julai
2002
.
Umoja huu unaendeleza kazi za
Umoja wa Muungano wa Afrika
(kwa Kiingereza: Organisation of African Union - OAU) uliokuwepo
1963
hadi 2002.
Nia ya umoja huu ni kujenga muundo na mfumo wa kisiasa, wa kiuchumi, na wa kijamii ili kufikia wakati ambapo
bara
la Afrika litakuwa na
bunge
moja,
benki
moja,
jeshi
moja,
rais
mmoja,
sarafu
moja, n.k.
Dhumuni kubwa la umoja huu ni kuunganisha nguvu za mataifa ya Afrika ili kuweza kutatua matatizo yanayokabili bara hili kama vile
vita
,
njaa
,
Ukimwi
, n.k.
Nchi wanachama
Umoja wa Afrika ina nchi wanachama 55, yaani nchi zote za bara la Afrika (baada ya kurudi kwa
Moroko
, iliyokuwa imejiondoa mwaka
1985
kwa sababu UA ilitambua
Sahara ya Magharibi
kuwa nchi huru wakati Moroko inadai ni eneo la majimbo yake ya kusini).
[2]
[3]
Mkutano wa kwanza wa
Bunge la Umoja wa Afrika
ulifanyika mwaka
2004
huko
Afrika Kusini
.
Mikutano mikuu ya UA
- Durban (Afrika Kusini): 9-11 Julai 2002.
- Maputo (Msumbiji): 10-11 Julai 2003.
- Sirte (Libya), mkutano wa dharura: Februari 2004.
- Addis Ababa (Ethiopia): 6-8 Julai 2004.
- Abuja (Nigeria): 24-31 Januari 2005.
- Sirte (Libya): 28 Jun. - 5 Julai 2005.
- Khartoum (Sudan): 16-24 Januari 2006.
Viongozi
Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya UA ni
N. Dlamini-Zuma
.
Spika
wa
Bunge la Umoja wa Afrika
ni
Roger Nkodo Dang
.
Tanbihi
Viungo vya nje
|
---|
Nadharia
| |
---|
Watetezi
| |
---|
Mashirika
| |
---|