Askofu
ni
mtu
mwenye
cheo
cha juu katika
Kanisa
. Kwa kawaida huliongoza katika eneo la
dayosisi
(jimbo) akisimamia
shirika
au
parokia
nyingi.
Neno
la
Kiswahili
"askofu" limetokana na
????
"uskufu" ambalo ni
umbo
la
Kiarabu
la neno la
Kigiriki
επισκοπο? "episkopos". Neno hilo katika
mazingira
ya
Wakristo
wa kwanza lilitumika kumtaja mwangalizi au msimamizi wa shughuli mbalimbali
serikalini
, katika shirika za wananchi au penye
ujenzi
.
Maandiko
ya kwanza ya
Agano Jipya
yanayotumia neno hili ni
nyaraka
za
Mtume Paulo
, ambaye anataja
kazi
hiyo katika
Fil
1,1. Lakini hakuna "episkopos" katika
1Kor
12,28 inayoorodhesha vyeo na kazi mbalimbali. Hii imechukuliwa na
wataalamu
wengi kama
dalili
ya kwamba wakati huo kile cha "episkopos" hakikuwa bado cheo cha kawaida katika shirika zote.
1Tim
3,1-7 na
Tit
1,7 zinataja "episkopos" lakini wengine hudhani ya kwamba nyaraka hizo zimeandikwa baada ya Paulo.
Katika
Mdo
20,28
wazee
au
viongozi
wa ushirika wa
Efeso
waitwa "episkopoi" kwa jumla.
Haya yote yanachukuliwa wa wataalamu wengi ya kuwa wakati wa
uandishi
wa Agano Jipya cheo cha "askofu" hakikuwa bado cheo maalumu. Lakini katika shirika kadhaa alipatikana tayari kiongozi aliyekuwa na cheo cha juu kuliko wazee.
Neno episkopos linaonekana kama cheo katika maandishi ya mwisho wa
karne I
na mwanzo wa
karne II
kama vile
waraka wa kwanza wa Klementi
ambapo askofu aonekana kuwa kiongozi mkuu wa kanisa la
mji
fulani.
Katika uenezi wa
Ukristo
madaraka
ya askofu yalipanuka. Kadiri makanisa yalivyoenea hata nje ya miji hadi
mashambani
askofu akawa kiongozi wa eneo, si wa mji tu.
Wakati ule ngazi za
daraja
zilionekana: Kanisa la mji au eneo likiongozwa na episkopos (askofu) akishauriana na "presbiteri" (kiasili: wazee; baadaye: ma
kasisi
) na kusaidiwa na ma
shemasi
au madikoni.
Kanisa Katoliki na Waorthodoksi
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Wakatoliki
na
Waorthodoksi
wana
daraja takatifu
ya Askofu, ambaye kwa kawaida ni mkuu wa kanisa katika ngazi ya
dayosisi
. Askofu ni kama baba wa makasisi (mapadri) na waumini wengine katika eneo lake.
Maaskofu hukutana kwenye
sinodi
na kufanya maazimio kuhusu mambo ya Kanisa lote.
Maaskofu wa nchi au eneo kubwa wako pamoja chini ya usimamizi wa
Patriarki
au wa
Askofu mkuu
.
Katika
Kanisa Katoliki
askofu wa Roma
ni mkuu wa Maaskofu wote na wa Kanisa lote
duniani
akitajwa kwa jina la
Papa
.
Mafundisho ya mlolongo wa mitume
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Katika
mapokeo
hayo askofu hutazamwa kama
mwandamizi
wa
Mitume wa Yesu
. Katika mafundisho hayo
Yesu Kristo
mwenyewe aliwaweka
mitume
wake 12 kuwa viongozi wa Kanisa lote na kuwapa madaraka. Madaraka hayo yalitolewa na mitume kwa kuwawekea
mikono
kichwani
waandamizi
wao waliopata hivyo kuwa maaskofu wa kwanza baada yao, nao wakafanya hivyo kwa waandamizi wao.
Kwa namna hiyo kuna mlolongo wa kuwekeana mikono kati ya wanaopokea nafasi ya uaskofu kuanzia mitume na kila
kizazi
cha maaskofu hadi leo. Hivyo maaskofu ni kiungo kati ya
Yesu
na waumini wa leo.
Baadhi ya
madhehebu
ya
Uprotestanti
, hasa ya
Anglikana
,
Wamoravian
na sehemu za
Walutheri
yanadai kuwa yameendeleza
mlolongo wa mitume
. Hiyo iliweza kutokea hasa katika nchi kama
Uingereza
na
Uswidi
ambako wakati wa
matengenezo ya Kiprotestanti
maaskofu Wakatoliki wa awali walihamia upande wa matengenezo na utaratibu wa kiaskofu uliweza kuendelea.
Pamoja na hayo, Kanisa Katoliki halikubali kwamba ilitokea hivyo
kihistoria
, au kwamba mtazamo wa Waprotestanti wa wakati huo kuhusu
daraja takatifu
na
ekaristi
ulitosha kushirikisha kweli
mamlaka
ya
Mitume wa Yesu
. Hivyo Kanisa hilo kwa jumla halitambui maaskofu wa Kiprotestanti kuwa na
sakramenti
ya daraja.
Upande wao, Waprotestanti wengi hawaoni umuhimu wa mlolongo wa kuwekewa mikono tangu wakati wa Mitume hadi leo: kwao muhimu zaidi ni uaminifu kwa
imani
ya Mitume.
Madhehebu mengine kadhaa ya Kiprotestanti yanatumika cheo cha askofu kuwa kiongozi katika Kanisa.
Kwa kawaida mamlaka yake ni ndogo kuliko ile ya maaskofu wa Kikatoliki na wa Kiorthodoksi, kutokana na mtazamo tofauti kuhusu Kanisa na
sakramenti
, ambao katika miaka ya mwisho imezidi kuwa tofauti kutokana na Waprotestanti wengi kukubali
wanawake
wapewe uaskofu na ukasisi, kinyume cha mapokeo na
imani
ya Wakatoliki na Waorthodoksi.
|
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Askofu
kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|