Jamhuri ya Kenya
ni
nchi
iliyoko
Afrika Mashariki
katika
ikweta
, kando ya
Bahari ya Hindi
.
Kenya imepakana na
Ethiopia
(kaskazini),
Somalia
(kaskazini mashariki),
Tanzania
(kusini),
Uganda
na
Ziwa Victoria
(magharibi), kisha
Sudan Kusini
(kaskazini magharibi).
Kenya ni nchi mwanachama wa
Jumuiya ya Afrika ya Mashariki
na wa miundo mingine mbalimbali ya kimataifa.
Mji mkuu
ni
Nairobi
.
Idadi
ya watu imeongezeka sana katika miaka ya karibuni na kufikia
milioni
49.
Kenya ina
mbuga
mbalimbali wanamoishi aina
elfu
kadhaa za
wanyama pori
.
Jina
la nchi limetokana na
mlima Kenya
[2]
, ulio wa pili kwa
urefu
barani
Afrika
.
[3]
[4]
Jiografia
Kenya ni nchi ya 47 kwa ukubwa
duniani
ikifuata mara
Madagaska
km
2
580 367 (sq mi 224 081)
[5]
ikiwa na eneo la
kilomita mraba
580,367 (
maili mraba
224,081).
Kutoka
pwani
ya Bahari ya Hindi, nyanda za chini zimeinuka hadi milima ya kati. Milima hii imetenganishwa na eneo la
Bonde la Ufa
; sehemu
tambarare
yenye
rutuba
upande wa
mashariki
. Milima ya Kenya ni kati ya iliyofaulu kwa
kilimo
barani Afrika.
Eneo hili la milima ndilo la juu zaidi nchini Kenya (na la pili kwa urefu barani Afrika):
Mlima Kenya
, unaofikia
urefu
wa
mita
5,199 (
futi
17,0570) m 5 199 (ft 17 057)na ni eneo lenye
mito
ya
barafu
.
Kusini mashariki
milima ya Taita
ndiyo mwanzo wa
tao la Mashariki
,
safu za milima
zenye miaka zaidi ya
milioni
100 ambazo zinaenea hasa nchini Tanzania.
Upande huohuo wa
kusini
Mlima Kilimanjaro
(m 5 895 (ft 19 341)
*
) huweza kuonekana ukiwa ng'ambo ya mpaka wa Kenya na Tanzania.
[6]
Halihewa
Kenya ni nchi yenye
jua
kali na
nguo
za
majira ya joto
huvaliwa mwaka mzima. Hata hivyo, huwa na
baridi
usiku
na pia
asubuhi
na mapema.
Hali ya hewa
ina
joto
na
unyevu
sehemu za pwani, joto kiasi sehemu za
bara
na ni
kame
katika sehemu za kaskazini na kaskazini-mashariki mwa nchi. Hata hivyo kuna
mvua
nyingi kati ya
Machi
na
Aprili
, na mvua ya kadiri kati ya
Oktoba
na
Novemba
.
Halijoto
huwa juu zaidi miezi hii yote.
Mvua ya
masika
hunyesha kuanzia Aprili hadi
Juni
. Mvua ya
vuli
nayo hunyesha kuanzia Oktoba hadi
Desemba
. Wakati mwingine mvua hii huwa nyingi na aghalabu hunyesha wakati wa
alasiri
na
jioni
. Majira ya joto jingi ni kuanzia
Februari
hadi Machi nayo ya baridi ni
Julai
hadi
Agosti
.
Wastani wa halijoto
|
Mji
|
Mwinuko (mita)
|
Upeo wa juu (°C)
|
Upeo wa chini(°C)
|
Mombasa (Mji wa Pwani)
|
|
17
|
30.3
|
22.4
|
Nairobi(Mji Mkuu)
|
|
1,661
|
25.2
|
13.6
|
Eldoret
|
align = "center"
|
3,085
|
23.6
|
9.5
|
Lodwar (Sehemu kame nyanda za juu)
|
|
506
|
34.8
|
23.7
|
Mandera (Sehemu kame nyanda za juu)
|
|
506
|
34.8
|
25.7
|
Mazingira
Kenya ina maeneo makubwa wanapoishi
wanyamapori
likiwemo
Masai Mara
, ambapo
nyumbu
na
wanyama
wengi
walanyasi
hushiriki katika
uhamaji
kila
mwaka
. Uhamaji huo, hasa uhamaji wa nyumbu, hutokea Juni hadi Septemba na hushirikisha mamilioni ya wanyama. Tukio hili huwavutia sana wapigaji
picha
za
sinema
. Takribani nyumbu 250,000 huangamia kila mwaka katika uhamaji huu wa kutafuta
lishe
wakati wa
kiangazi
.
Wale wanyama wakubwa watano wa Afrika wanapatikana Kenya:
simba
,
chui
,
nyati
,
kifaru
na
ndovu
. Wanyama wengine wengi wa
pori
na
ndege
hupatikana katika
mbuga za taifa
na
hifadhi za wanyama
hawa nchini.
Mazingira ya Kenya yanahatarishwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu na athari zake.
Historia
Historia ya awali
Mabaki ya
mamba
mkubwa ajabu wa zamani za Mesozoic Era, ambayo ni miaka
milioni
200 iliyopita, yaligunduliwa nchini Kenya katika
chimbo
zilizochimbwa na
wataalamu
kutoka
Chuo Kikuu cha Utah
na
Makavazi ya Kitaifa
nchini Kenya miezi ya Julai hadi Agosti
2004
katika
bonde
la
Lokitaung
, karibu na
Ziwa Turkana
.
[7]
Mabaki yaliyopatikana Afrika Mashariki yaonyesha kuwa miaka
milioni
20 iliyopita
viumbehai
mfano wa
sokwe
waliishi eneo hili.
Uchunguzi
wa juzijuzi karibu na Ziwa Turkana waonyesha kuwa viumbe aina ya
Homo habilis
(walioishi miaka milioni 1.8 na 2.5 iliyopita) na
Homo erectus
(walioishi miaka milioni 1.8 na miaka 350,000 iliyopita) huenda ndio wazazi wa watu wa kisasa
homo sapiens
walioishi Kenya
enzi za barafu kuu
kuisha barani.
Katika mwaka wa
1984
,
uvumbuzi
uliofanywa na
mtafiti
maarufu
Richard Leakey
na
Kamoya Kimeu
huko Ziwa Turkana ulikuwa wa
mifupa
ya
mvulana
iliyohusishwa na
Homo erectus
wa miaka milioni 1.6 iliyopita. Utafiti wa awali wa viumbe hawa unahusishwa na
Mary Leakey
na
Louis Leakey
, ambao ndio waliofanya uchunguzi wa mwanzo wa ki
akiolojia
huko
Olorgesailie
na
Hyrax Hill
. Baadaye utafiti wa Olorgesailie uliendelezwa na
Glynn Isaac
.
Historia kabla ya ukoloni
Wakazi wa kwanza wa eneo linaloitwa Kenya walikuwa wa jamii ya
Wakhoisan
: hadi leo kuna makabila matatu madogo yenye asili hiyo, ingawa yanatumia
lugha za Kikushi
:
Waata
,
Waawer
na
Wadahalo
.
Wakushi
kutoka
kaskazini
waliingia Kenya kati ya
miaka ya 3200 KK
na
1300 KK
[8]
. Mwaka
500 KK
hivi wazungumzaji wa
lugha za Kinilo-Sahara
na katika
milenia ya kwanza KK
wale wa
lugha za Kibantu
waliingia katika eneo hili, na sasa
Waniloti
ni 30% ya Wakenya wote.
Wafanyabiashara
Waarabu
walianza kufika
pwani
ya Kenya
karne ya 1
BK
. Ukaribu wa Kenya na Uarabuni ulirahisisha
ukoloni
, hivyo Waarabu na
Waajemi
walianza kuishi eneo la pwani
karne ya 8
. Hata hivyo, baadhi ya walioitwa "Waarabu" katika eneo la Afrika Mashariki walikuwa ma
chotara
, Waafrika-Waarabu.
Pwani ya Kenya imekuwa makao ya jamii ya
wahunzi
na jamii ya
wakulima
wadogowadogo,
wawindaji
na
wavuvi
ambao walikuwa
mhimili
wa
uchumi
kwa kushiriki katika kilimo, uvuvi, utengenezaji chuma, na
biashara
na nchi za kigeni.
[8]
Kuanzia
karne ya 6
au
karne ya 9
, Kenya ilijihusisha na
shughuli
za u
baharia
kukuza
uchumi
ikaanza kutengeneza
meli
za kuabiria kusini hadi miji mingine yenye
bandari
kama
Kilwa
na
Shanga
iliyo katika pwani ya Afrika Mashariki.
Mombasa
ulikuwa
mji
wenye bandari wa nchi ya Kenya katika
karne za kati
. Bandari hiyo ilitumika kuendeleza
biashara
na miji mingine yenye bandari Afrika,
Uajemi
, na wafanyabiashara Waarabu,
Yemeni
na hata
Bara Hindi
.
[9]
Baharia
Mreno
Duarte Barbosa
wa
karne ya 15
alidai kuwa "[Mombasa] ni bandari nzuri na yenye shughuli nyingi,
mashua
nyingi na hata meli kubwa ajabu, ambazo zote hutoka
Sofala
na nyingine kutoka
Cambay
,
Melinde
na nyingine zinazoabiri hadi kisiwani
Unguja
."
[10]
Karne kadhaa kabla ya ukoloni,
upwa
wa Kenya wanakoishi
Waswahili
ulikuwa sehemu ya eneo la mashariki mwa Afrika lililofanya biashara, hasa ya
watumwa
na
pembe za ndovu
na Waarabu na
Wahindi
. Inasemekana kwamba
kabila
la
Wameru
lilitokana na watumwa waliotoroka utumwa
Uarabuni
miaka ya 1700
. Mwanzoni wafanyabiashara wengi walitokea
milki
za Uarabuni lakini baadaye wengine wakatokea Unguja (kama
Tippu Tip
).
[11]
Kiswahili
, ambacho ni
lugha
ya
Kibantu
iliyokopa
misamiati
ya
Kiarabu
,
Kiajemi
na mingine kutoka
Mashariki ya Kati
na
Asia Kusini
, baadaye ilikua ikawa
lingua franca
ya biashara kwa jamii mbalimbali.
[8]
Kwa
karne
nyingi, upwa wa Kenya umekuwa mwenyeji wa wafanyabiashara na wasafiri. Kati ya miji iliyopo kwenye upwa wa Kenya , mji wa
Malindi
umebakia kuwa makazi muhimu ya Waswahili tangu
karne ya 14
na wakati mmoja ulishindana na Mombasa kwa ukuu pande hizi za Afrika Mashariki. Kwa kawaida, Malindi umekuwa mji na bandari ya kirafiki kwa
serikali
nyingine. Mwaka wa
1414
,
Sultani
Mwarabu wa Malindi alianzisha uhusiano wa ki
diplomasia
na utawala wa
Uchina
wa
Ming
, wakati wa safari za
mchunguzi
Zheng He
.
[12]
Katika mwaka wa
1498
, utawala wa Malindi ulimkaribisha msafiri na
mvumbuzi
maarufu kutoka Ureno,
Vasco da Gama
.
Chini ya ukoloni
Wareno
walikuwa
Wazungu
wa kwanza kuzuru eneo la Kenya ya sasa:
Vasco da Gama
alikuwa amezuru Mombasa mwaka wa
1498
. Safari ya Vasco da Gama ilifaulu alipofikia huko
India
, na jambo hilo liliwawezesha Wareno kufanya
biashara
moja kwa moja na
Mashariki ya Mbali
kupitia
bahari
na hivyo kutatiza mitandao ya kibiashara ya awali ya
nchi kavu
na baharini kama njia za biashara ya
viungo
zilizotumia
Ghuba la Uajemi
,
Bahari Nyekundu
na misafara iliyofika hadi eneo la mashariki ya
Mediterranea
.
Jamhuri ya Venisi
ndiyo iliyotawala maeneo ya biashara kati ta
Uropa
na
Asia
. Baada ya njia za kawaida za nchi kavu hadi India kufungwa na
Waturuki
wa
Ottoman
, Ureno ulitarajiwa kutumia njia ya baharini iliyotumiwa kwanza na Vasco da Ghama ili kuvunja
ukiritimba
wa
Venice
.
Utawala wa Wareno huko Afrika Mashariki ulijihusisha hasa na pwani iliyokaribia Mombasa. Kuwepo kwa Wareno Afrika Mashariki kulianza rasmi baada ya mwaka wa
1505
, wakati
manowari
za Wareno, zikiongozwa na Don
Francisco de Almeida
, zilipokishinda
Kilwa
,
kisiwa
kilicho katika eneo ambalo sasa ni
Tanzania
kusini.
Kuwepo kwa Wareno Afrika Mashariki kuliwawezesha kudhibiti biashara katika
Bahari ya Hindi
, na kulinda njia za baharini zinazounganisha Uropa na Asia. Manowari zao za kivita zilikwamisha biashara za maadui wao magharibi mwa Bahari ya Hindi na walitoza
kodi
juu ya
bidhaa
zilizosafirishwa kupitia eneo hilo kwani walitawala
bandari
zote na njia kuu za
meli
.
Kujengwa kwa
ngome
iliyoitwa
Fort Jesus Mombasa
mwaka wa
1593
kulikusudiwa kuimarisha utawala wao katika eneo hilo, lakini
ushawishi
wao ulikatizwa na kuja kwa
Waingereza
,
Waholanzi
na
Waarabu
wa
Omani
katika eneo hilo
karne ya 17
.
Waarabu kutoka Omani ndio waliokuwa
tishio
kuu la utawala wa Wareno Afrika Mashariki na waliizingira ngome ya Wareno, wakazishambulia meli zao za kivita, kisha kuwafukuza Wareno waliobaki kutoka pwani ya Kenya na Tanzania mwaka wa
1730
. Kufikia wakati huo, ufalme wa Ureno haukuwa na
haja
na njia ya bahari ya biashara ya viungo kwani
faida
yake ilikuwa imepungua sana. Utawala wa Wareno ulibakia tu katika bandari na maeneo ya kusini mwa
Msumbiji
hadi mwaka wa
1975
.
Kutawaliwa kwa pwani ya Kenya na Tanzania na Waarabu kutoka Omani kuliifanya miji hii iliyojitawala hapo awali iwe chini ya uangalifu mkali wa wageni kuliko ilivyokuwa katika enzi za utawala wa Wareno. Waarabu wa Omani, kama Wareno waliowatangulia, waliweza kutawala eneo la pwani tu, si eneo la bara. Hata hivyo, kuanzishwa kwa ma
shamba
makubwa ya mi
karafuu
, kuongezeka kwa
biashara ya utumwa
na kuhamishwa kwa
makao makuu
ya Waomani hadi
Zanzibar
mwaka wa
1839
na
Seyyid Said
kulisababisha Waomani kuimarisha utawala wao katika eneo hilo.
Utawala wa Waarabu katika bandari kuu zote za pwani ya Afrika Mashariki uliendelea hadi
Uingereza
ilipoamua kumaliza biashara ya utumwa na uanzishaji wa
utaratibu
wa kufanya
kazi
kwa
malipo
ukaanza kushinikiza utawala wa Waomani.
Kufikia mwisho wa
karne ya 19
, biashara ya watumwa katika bahari zote kuu ilikuwa imeharamishwa na Waingereza: Waarabu wa Omani hawakuwa na uwezo wa kupingana na
jeshi la wanamaji
la Uingereza lililokuwa likitekeleza amri hiyo. Waomani waliendelea kuwepo visiwani
Unguja
na
Pemba
hadi
mapinduzi
ya mwaka wa
1964
, lakini kuwepo kwa Waarabu wa Omani nchini Kenya rasmi kulisitishwa wakati Wajerumani na Waingereza walipozidhibiti bandari zote kuu na kuanzisha mahusiano ya kibiashara na viongozi mashuhuri waliokuwa wenyeji
miaka ya 1880
. Hata hivyo,
urithi
waliouacha Afrika Mashariki ungali unaonekana kupitia kwa vizazi vyao vipatikanavyo pwani ya Kenya na ambavyo vinaona kuwa asili yao ni Oman. Vizazi hivi hata leo humiliki
utajiri
mwingi na ndio wenye ushawishi mkubwa wa kisiasa katika jamii za pwani ya Kenya.
Hata hivyo,
wanahistoria
wengi hushikilia kuwa
historia
ya
ukoloni
nchini Kenya ilianza wakati Wajerumani walipoanza kutawala
mali
ya
Sultani wa Unguja
iliyo pwani mwaka wa
1885
, ikifuatwa na kuja kwa
kampuni
ya Imperial British East Africa Company mwaka wa
1888
.
Uhasama
wa kwanza baina ya ma
bepari
ulikatizwa wakati Ujerumani ulipouachia Uingereza sehemu ya pwani iliyomiliki. Hii ilifuatia kujengwa kwa
reli
iliyounganisha Kenya na
Uganda
. Baadhi ya ma
kabila
ya Kenya yalipinga
ujenzi
huo, hasa
Wanandi
wakiongozwa na
Orkoiyot
Koitalel Arap Samoei kwa miaka kumi, kuanzia
1895
hadi
1905
? lakini hatimaye Waingereza waliijenga reli hii.
Inaaminika kuwa Wanandi walikuwa kabila la kwanza kuwekwa kwenye maeneo yaliyotengewa
Waafrika
ili kuwazuia kutatiza ujenzi wa reli. Wakati huo
Wahindi
wengi wenye
ujuzi
waliingia nchini ili kuchangia ujenzi. Wakati wa ujenzi wa reli kupitia
Hifadhi ya Taifa ya Tsavo Magharibi
, Wahindi wengi na wenyeji Waafrika walivamiwa na
simba
wawili waliojulikana kama “
wala watu wa Tsavo
”. Wahindi hao na vizazi vyao baadaye walibakia nchini Kenya na kuunda
kitovu
cha
jamii
za Wahindi zijulikanayo kama
Ismaili Muslim
na
Sikh
.
[13]
[14]
Mnamo Agosti
1914
,
Vita vya Kwanza vya Dunia
vilipoanza, ma
gavana
wa
British East Africa
(kama eneo hilo lilivyojulikana) na
German East Africa
walifikia makubaliano ili kuepusha ma
koloni
yao machanga na uhasama. Hata hivyo,
Luteni Kanali
Paul von Lettow-Vorbeck
alichukua
mamlaka
ya majeshi ya Ujerumani, akiwa na kusudi la kutwaa
raslimali
nyingi iwezekanavyo za Uingereza. Jeshi la Uingereza likiwa limemtenga na Ujerumani, von Lettow aliendesha
kampeni
iliyofaulu ya
vita vya kuvizia
, wakila walichopata, wakiteka bidhaa za matumizi za Uingereza, na kuepuka kushindwa. Mwishowe alisalimu amri na akajisalimisha nchini
Zambia
siku kumi na moja baada ya mapatano ya kusimamisha vita kutiwa
sahihi
mwaka wa
1918
. Waingereza walitumia jeshi la Wahindi kumfukuza Lettow na walihitaji
wachukuzi
wengi ili kubeba vifaa vya matumizi hadi
bara
kwa
miguu
na hivyo kutatua
shida
kuu ya uchukuzi. Kundi la wanajeshi wachukuzi liliundwa na kuwajumuisha Waafrika 400,000, na kuchangia katika
uhamasishaji
wao wa muda mrefu kisiasa.
Hadi mwaka wa 1920, eneo linaloitwa Kenya lilijulikana kama Himaya ya Uingereza ya Afrika Mashariki.
[15]
Mwaka huo,
koloni
la Kenya liliundwa na kupatiwa jina linalotokana na Mlima Kenya
[16]
Waingereza walilitamka jina hilo kama pronounced
/?kiːnj?/
[17]
ingawa matamshi ya wenyeji na yaliyokusudiwa katika maendelezo asili,
Kenia
yalikuwa ?k?nja.
[18]
Enzi ya
Jomo Kenyatta
kuwa
rais
wa Kenya miaka ya
1960
-
1969
, matamshi ya
Kiingereza
, yaani
/?k?nj?/
yalikubalika na kutumiwa sana kwa sababu jina lake lilidumisha matamshi asilia ya wenyeji.
[19]
Kumbe saa ya uhuru, mwaka
1963
,
Jomo Kenyatta
alichaguliwa kama rais wa kwanza.
[20]
Awali alikuwa alishika jina hili kutafakari ahadi yake ya kuikomboa nchi yake na matamshi yake ya jina lake ulisababisha katika matamshi ya Kenya katika Kiingereza kubadilisha nyuma ya makadirio ya awali uliotokea matamshi, pronounced
/?k?nj?/
Mwanzoni mwa
karne ya 20
,
wakulima
Waingereza na Wazungu wengine walituama katika
nyanda za juu
katika eneo la kati walikoondokea kuwa ma
tajiri
kwa kulima
kahawa
na
chai
.
[21]
Kufikia mwaka
1930
, takribani
walowezi
30,000 waliishi katika maeneo hayo na walikuwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa kwa sababu ya uwezo wao wa ki
uchumi
.
Maeneo hayo yalikuwa makao ya watu
milioni
moja wa kabila la
Wakikuyu
, na wengi wao hawakuwa na
ithibati
ya kumiliki mashamba kwa mujibu wa Waingereza (ingawa mashamba hayo yalimilikiwa na kabila hilo kabla ya Wazungu kufika), na waliishi kama wakulima wanaohamahama. Ili kuendeleza matakwa yao, walowezi waliwakataza kilimo cha kahawa na kuwalazimisha kulipa kodi ya
nyumba
, na maskwota walipewa mashamba madogo baada ya kuwafanyia kazi. Wakikuyu wengi walihamia mijini kwani mashamba yao hayangeweza kutosheleza mahitaji yao.
Mwaka wa
1951
,
Horace Hector Hearne
akawa
mkuu wa sheria
nchini Kenya (alitoka
Ceylon
alikoshikilia
wadhifa
huohuo) na alifanya kazi katika
Mahakama Kuu
mjini
Nairobi
. Alihudumu katika wadhifa huo hadi mwaka
1954
alipoteuliwa kama
Hakimu wa Rufaa
katika
Mahakama ya Rufaa
ya
Afrika Magharibi
.
Usiku
wa tarehe
5 Februari
1952
, wakati
Mfalme
George VI
alipoaga dunia, Hearne alimsindikiza
Malkia
Elizabeth II
na
mumewe
Filipo
mwanamfalme
wa
Edinburgh
, kwa dhifa ya kitaifa hotelini Treetops, ambayo sasa ni kivutio maarufu cha watalii. Hapa ndipo alipouanzia umalkia.
[22]
Alirudi Uingereza mara moja akiandamana na Hearne.
Kuanzia Oktoba 1952 mpaka Desemba
1959
, Kenya ilikuwa katika
hali ya hatari
kufuatia
uasi
wa
Mau Mau
dhidi ya utawala wa Uingereza. Gavana aliomba na kupata msaada wa wanajeshi Waingereza na Waafrika, pamoja na
King's African Rifles
. Mnamo Januari
1953
,
Meja Jenerali
Hinde aliteuliwa kuwa mkuu wa oparesheni ya kuzima uasi. Hali hii haikuimarika kwa kukosa uchunguzi, kwa hivyo
Jenerali
George Erskine
aliteuliwa kuwa
kamanda
msimamizi wa majeshi ya kikoloni mnamo Mei 1953, akiungwa mkono hasa na
Winston Churchill
.
Kutiwa mbaroni kwa
War?hi? Itote
(aka
General China
) tarehe
15 Januari
1954, na kuhojiwa kwake kulipelekea Waingereza kuuelewa vyema usimamizi wa Mau Mau.
Oparesheni Anvil
iliyoanzishwa tarehe
24 Aprili
1954 ilipangwa na
jeshi
kwa
wiki
kadhaa baada ya kukubaliwa na kamati kuu ya vita. Wakati wa oparesheni hiyo, mji wa Nairobi ulidhibitiwa na wanajeshi na wakazi wake walihojiwa huku wafuasi wa Mau Mau wakikamatwa na kupelekwa vizuizini.
Mnamo Mei 1953, walinzi wa nyumbani walitambulika rasmi kama
askari wa usalama
. Askari hao wa nyumbani ndio waliounda kikosi cha kupambana na mikakati ya Mau Mau kwani walikuwa Waafrika waaminifu, na si majeshi ya kigeni kama Jeshi la Uingereza na King's African Rifles. Kufikia mwisho wa hali ya hatari, askari hao walikuwa wamewaua Mau Mau 4886, ambao ni asilimia 42% ya waasi wote. Kukamatwa kwa
Dedan Kimathi
huko
Nyeri
tarehe
21 Oktoba
1956
kuliashiria kushindwa kwa Mau Mau kukamaliza vita.
Baada ya uhuru
Utawala wa Kenyatta
Waafrika walichaguliwa moja kwa moja katika
bunge la uwakilishi
kwa mara ya kwanza mwaka wa
1957
. Licha ya Waingereza kutamani kuwakabidhi
mamlaka
wapinzani wasio na
siasa kali
ya Kiafrika, ni
chama
cha
Kenya African National Union
(KANU) kilichoongozwa na
Jomo Kenyatta
kilichounda
serikali
punde tu kabla ya Kenya kupata
uhuru
tarehe
12 Desemba
1963
. Tarehe 12 Desemba
1964
, Kenya ilipotangazwa kuwa
jamhuri
, Kenyatta akawa
rais
wa kwanza.
Mwaka huohuo,
jeshi la Kenya
lilipigana na
Vita vya Shifta
dhidi ya kabila la
Wasomali
waliokusudia kuiona NFD imejiunga na
Jamhuri ya Somalia
.
Mashifta
walililemea jeshi la Kenya lakini baadaye walishindwa mwaka wa
1967
.
Kenya ilitia
saini
mkataba
na nchi ya
Ethiopia
mwaka wa
1969
unaodumu mpaka leo kwa kuhofia ma
shambulizi
kutoka kwa
jeshi la Somalia
lililokuwa na nguvu zaidi.
[23]
Eneo la NFD nchini Kenya halijaendelea kutokana na
kiangazi
na
mafuriko
. Hata hivyo,
wakimbizi
wafanyabiashara wa Kisomali waliotajirika wamebadilisha
mtaa
wa Eastleigh uliokuwa wa ma
banda
na kuufanya kuwa ngome ya kibiashara katika sehemu kubwa ya mashariki mwa mji wa Nairobi.
[24]
Utawala wa Moi
Mwaka wa
1978
, Kenyatta alifariki na
Daniel Arap Moi
akawa rais. Moi alidumisha
urais
kwa kuchaguliwa bila kupingwa katika chaguzi za mwaka wa
1979
,
1983
(uchaguzi wa
dharura
) na
1988
, zote zikiwa zilifanyika chini ya
katiba
ya
chama kimoja
. Uchaguzi wa 1983 ulifanyika mwaka mmoja kabla ya wakati kutokana na
njama
ya
kupindua serikali
iliyokosa kufaulu tarehe
1 Agosti
1982
.
Mapinduzi
hayo yaliyotibuka yalipangwa na
askari
mwanahewa
wa
cheo
cha chini, Bwana
Hezekiah Ochuka
na kuendelezwa hasa na wanahewa.
Jaribio
hilo lilizimwa kwa haraka na wanajeshi waaminifu wakiongozwa na
Jeshi la Nchi Kavu
, General Service Unit (GSU) - kikosi cha
polisi
wenye
hadhi
ya kijeshi - na baadaye polisi wa kawaida. Hata hivyo
raia
kadhaa walijeruhiwa na wengine kuuawa.
Tukio
hilo lilisababisha kuvunjwa kwa kikosi chote cha wanahewa, huku wengine wakiachishwa kazi na wengine wakishtakiwa kwenye
mahakama ya kijeshi
.
Katika uchaguzi wa 1988
kura za mlolongo
zilianzishwa, ambapo wapigakura walitakiwa kupiga
foleni
nyuma ya
wagombea
wanaowapenda, badala ya kutumia
kura ya siri
[25]
Jambo hilo lilionekana kama
kilele
cha enzi ya
ukiukaji
mkubwa wa
demokrasia
likasababisha
msukumo
mkuu wa
mageuzi
ya kikatiba. Vipengele vilivyokuwa na utata, kikiwemo kile kilichoruhusu chama kimoja pekee cha kisiasa, vilibadilishwa miaka iliyofuata.
[26]
Katika uchaguzi wa kidemokrasia wa vyama vingi wa miaka ya
1992
na
1997
, Daniel Arap Moi alichaguliwa tena.
Utawala wa Kibaki
Kulingana na katiba, mwaka
2002
Moi hakuruhusiwa kuwania urais tena, na
Mwai Kibaki
wa
chama cha upinzani
cha "
National Rainbow Coalition
" ? NARC akachaguliwa kuwa rais. Uchaguzi huo ulitambulikana kuwa wa kidemokrasia na
wachunguzi
wa humu nchini na wa kimataifa na hivyo kuwa chanzo cha mageuzi makubwa ya kidemokrasia nchini Kenya.
Mnamo Desemba
2002
, Wakenya walifanya uchaguzi uliokuwa wa kidemokrasia na uwazi ambao kwa kiasi kikubwa uliamuliwa kuwa huru na wa haki na wachunguzi wa kimataifa. Uchaguzi wa mwaka huo ulikuwa mwanzo mpya na uliiletea Kenya mabadiliko makuu ya kisiasa yaliyowezesha chama cha Kenya African National Union (KANU), kilichokuwa kimeitawala nchi tangu uhuru, kukabidhi kwa amani mamlaka kwa chama cha National Rainbow Coalition (NARK), uliokuwa muungano wa vyama vingi.
Chini ya uongozi wa Rais Mwai Kibaki, muungano wa vyama tawala ulihahidi kushughulikia ukuaji wa kiuchumi, kumaliza ufisadi, kuimarisha elimu na kuandika katiba mpya. Baadhi ya ahadi hizi zimeshatimizwa. Kuna elimu ya msingi ya bure. Mwaka wa 2007 serikali ilitangaza kuwa, kuanzia mwaka 2008 gharama ya masomo ya shule za upili itapunguzwa huku serikali ikilipia gharama zote za mafundisho.
Uchaguzi wa 2007
Katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 27 Desemba 2007, Rais Kibaki wa chama cha Party of National Unity (PNU) aliwania uchaguzi dhidi ya chama kikuu cha upinzani Orange Democratic Movement (ODM). Kulingana na wachunguzi wa kimataifa, uchaguzi huo ulikumbwa na udanganyifu na hivyo kutofikia kiwango kinachokubalika kimataifa. Chama cha ODM kilisambaratika na kupoteza 8 % ya kura zake kwa chama kipya cha Orange Democratic Movement-Kenya (ODM) - kikiongozwa na
Kalonzo Musyoka
. Kinyang’anyiro kilikuwa kikali kati ya mgombea wa ODM,
Raila Odinga
na Kibaki wa PNU. Kuhesabiwa kwa kura na
Tume ya Uchaguzi ya Kenya
kulionyesha Raila akiongoza kwa
kura
chache na baadaye kwa kura nyingi. Hata hivyo, kura zilipoendelea kuhesabiwa na Tume ya Uchaguzi, Kibaki alimkaribia
mpinzani
wake kwa kura, kisha akamshinda. Matokeo hayo yalisababisha
maandamano
na kulaumiwa kwa Tume ya Uchaguzi ya Kenya kwa kumpendelea Kibaki, hivyo Oginga akajitangaza “rais wa watu” na kutaka kura zihesabiwe tena.
[27]
Maandamano hayo yalibadilika kuwa
ghasia
zilizosababisha kuharibiwa kwa
mali
.
[28]
. Viongozi mashuhuri wa Afrika, wakiongozwa na aliyekuwa
katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa
Kofi Annan
walisuluhisha
mzozo
huo wa kisiasa. Kundi la Annan liliungwa mkono na
Umoja wa Mataifa
,
Jumuia ya Ulaya
,
Muungano wa Nchi za Afrika
, Serikali ya Marekani na nchi nyingine maarufu ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi rejelea
Ghasia nchini Kenya (2007-2008)
.
Annan aliomba usaidizi kwa
kamati
yake ya
upatanishi
kutoka kwa shirika la kushughulikia mizozo la
Uswisi
lijulikanalo kama Kituo cha Mazungumzo ya Kihisani yaani Centre for Humanitarian Dialogue.
Serikali ya muungano
Tarehe
12 Februari
2008 Kibaki na Odinga walitia sahihi mkataba wa kuunda
serikali ya muungano
ambapo Odinga angekuwa
waziri mkuu
wa pili nchini Kenya. Kulingana na mkataba huo, rais angeteua
baraza la mawaziri
kutoka pande zote mbili za PNU na ODM kulingana na wingi wa wabunge wa kila chama bungeni. Mkataba huo ulieleza kuwa baraza la mawaziri litajumuisha
Makamu wa Rais
na manaibu wawili wa Waziri Mkuu. Baada ya majadiliano bungeni ilipitishwa kuwa muungano huo utadumu hadi mwisho wa kipindi cha bunge, ama chama kimoja kikijitoa kwenye muungano kabla ya kipindi cha bunge kuisha.
Wadhifa
huo mpya wa waziri mkuu utakuwa na nguvu na mamlaka kuratibu na kusimamia shughuli za serikali. Vilevile itaongozwa na mbunge aliyechaguliwa ambaye pia atakuwa kiongozi wa chama au muungano wa vyama wenye idadi kubwa ya wabunge bungeni. Ulimwengu ulimshuhudia Annan na kamati yake iliyoungwa mkono na Umoja wa Mataifa na mwenye kiti wa muungano wa nchi za Afrika Jakaya Kikwete, walipowaleta pamoja wapinzani hawa sugu kwenye sherehe za kutia sahihi mkataba huu. Sherehe hizi zilionyeshwa moja kwa moja kwenya televisheni ya kitaifa kutoka kiingilio cha Jumba la Harambee mjini Nairobi. Wawakilishi wa PNU na ODM walianza majadiliano ya kina kuhusu ugavi wa mamlaka tarehe 29 Februari 2008.
[29]
Wabunge wa Kenya, kwa pamoja, waliidhinisha mkataba wa ugawaji mamlaka tarehe 18 mwezi wa Machi 2008 ili kuiokoa Kenya iliyoaminika kama mojawapo ya nchi thabiti na iliyoendelea barani Afrika. Mkataba huu uliunganisha PNU iliyoongozwa na Kibaki na ODM ya Odinga kisha kupelekea kuundwa kwa serikali ya muungano, vyama vyote viwili vikiwa na mamlaka sawa.
[30]
Tarehe
13 Aprili
2008, Rais Kibaki aliitangaza baraza la mawaziri 41 wa serikali hii ya muungano ikijumuisha waziri mkuu na makamu wake wawili. Baraza hili lilijumuisha pia manaibu wa mawaziri 50 na lilitawazwa katika
Ikulu
ya Nairobi tarehe
17 Aprili
2008 huku Kofi Annan na viongozi wengine mashuhuri wakishuhudia.
Tarehe
4 Novemba
2008
ilitangazwa kuwa
sikukuu ya kitaifa
kusherehekea
ushindi
wa
Barack Obama
, ambaye
baba
yake alikuwa Mkenya, kama rais wa
Marekani
.
Katika sehemu za mashambani, kama wilayani
Kisii
, visa vya kuchoma watu wakidaiwa kuwa
wachawi
vinaongezeka.
[31]
Waathiriwa hasa ni wanawake wakongwe. Mnamo Mei 2008, watu 11 waliuwa na nyumba 30 kuchomwa.
[32]
Siasa
Tazama pia:
Orodha ya vyama vya kisiasa nchini Kenya
Kwa sasa Kenya ni
jamhuri
ya
kidemokrasia
ya kiuwakilishi inayoongozwa na rais, ambaye ndiye mkuu wa taifa na kiongozi wa serikali, na yenye
mfumo wa vyama vingi
.
Serikali
ndiyo yenye
mamlaka
ya juu.
Utungaji wa
sheria
ni jukumu la serikali na la
bunge
la taifa. Idara ya Mahakama ni huru, na imejitenga na serikali kuu na bunge. Hata hivyo, kulikuwa na kutoridhika kwingi, hasa katika enzi ya rais mstaafu
Daniel Arap Moi
, kuwa serikali iliingilia sana shughuli za mahakama.
Kenya imedumisha uthabiti wa kutosha licha ya mabadiliko katika mifumo yake ya kisiasa na michafuko katika nchi kadhaa jirani. Bunge la mseto wa vyama vingi la
1997
lilianzisha
mageuzi
yaliyobadilisha sheria za kikoloni zenye
dhuluma
zilizotumika kuuzuia uhuru wa kuongea na kutangamana. Jambo hilo liliimarisha uhuru wa
umma
na kuchangia kiasi kuaminika kwa
uchaguzi
wa Desemba 1997.
Kaunti na tarafa
Kenya ina
kaunti
47, kila moja ikiongozwa na Mkuu wa Kaunti anayechaguliwa na watu ambao wanaishi kwenye hiyo kaunti.
Serikali za mitaa
huendelezwa kupitia mabaraza ya miji. Maeneo mengi ya mijini huwa ni
mji
,
manisipaa
au baraza la mji. Serikali za mitaa katika maeneo ya
mashambani
huitwa
serikali
za
wilaya
. Ma
diwani
wa mitaa hii huchaguliwa katika
uchaguzi
wa madiwani unaofanywa wakati mmoja na
uchaguzi mkuu
.
Maeneo ya uwakilishi bungeni yamegawanywa kwa sababu ya upigaji
kura
. Kuna maeneobunge 210 nchini Kenya.
[33]
Idadi ya watu katika miji muhimu
Watu
Kenya ni nchi yenye ma
kabila
mengi tofautitofauti, hasa ya
Kibantu
(67%) na ya
Kiniloti
. Wakenya wengi huzungumza
lugha
mbili,
Kiingereza
na
Kiswahili
, na
asilimia
kubwa pia huzungumza
lugha mama
ya kabila lao.
Makundi ya makabila ni kama ifuatavyo:
Wakikuyu
22%,
Waluyia
14%,
Wajaluo
13%,
Wakalenjin
12%,
Wakamba
11%,
Wakisii
6%,
Wameru
6%, makabila mengine ya Kiafrika 15%, wasio Waafrika (
Wahindi
,
Waingereza
na
Waarabu
) 1%
[5]
Kila kundi au kabila lina lugha yake na Kiswahili hutumika kama chombo cha kuwasiliana miongoni mwa makabila tofauti.
Dini
Upande wa
dini
, idadi kubwa ya Wakenya ni
Wakristo
: kulingana na
sensa
ya mwaka
2019
,
asilimia
85.5 ya
wakazi
wa
Kenya
walikuwa
Wakristo
(asilimia 53.9 ni
Waprotestanti
, asilimia 20.6 ni
Wakatoliki
, asilimia 11.8 ni Wakristo wa
madhehebu
mengine mbalimbali, wakiwemo Waorthodoksi 621,200), asilimia 10.9 ni
Waislamu
, asilimia 0.7 ni wafuasi wa
dini asilia za Kiafrika
, asilimia 1.7 ni wa makundi mengine ya dini (kuna
Wahindu
takribani 60,000, ambao wameingiliana vyema na Wakenya wengine na huchangia pakubwa uchumi wa nchi), na asilimia 1.6 wanadai hawana uhusiano na
dini
yoyote ile.
[34]
Asilimia 60 ya idadi ya Waislamu huishi katika Mkoa wa Pwani, wakiwa asilimia 50 ya jumla ya wakazi wa pale. Wengi wa wanaoishi sehemu ya magharibi mkoani Pwani ni Wakristo. Eneo la kaskazini la Mkoa wa Mashariki ni makazi ya asilimia 10 ya jumla ya Waislamu nchini; hii ndiyo
dini
ya wakazi wengi wa hapa, na mbali na idadi ndogo ya
Wasomali
wanaoishi Nairobi, idadi kubwa ya Wakenya wengine ni Wakristo.
[35]
Utamaduni
Kenya ni nchi yenye tamaduni anuwai. Tamaduni zinazotambulika ni pamoja na Waswahili walio katika eneo la pwani, jamii za wafugaji katika eneo la kaskazini na jamii nyingine mbalimbali katika maeneo ya kati na magharibi.
Wajaluo
wa Kenya ni wazawa wa
jamii
za
wakulima
na
wafugaji
walioishi magharibi mwa Kenya kabla ya ukoloni. Inafahamika kwamba asili ya Wajaluo na makabila mengine ya
Waniloti
ni kaskazini mwa Kenya, pengine maeneo ya Sudan Kusini ya sasa. Waniloti, kama wanavyoitwa, ni kikundi cha ki
anthropolojia
kilichotoka maeneo ya kaskazini mashariki mwa Afrika. Pengine walihamia kusini kutokana na
vita
vilivyosababishwa na ukuaji wa
Kush
na
Misri
. Waniloti nchini Kenya ni
Wajaluo
,
Waturkana
,
Wakalenjin
na
Wamasai
. Hili linadhihirika kutokana na kuwepo kwa
lahaja
zinazofanana kati ya makabila fulani nchini Sudan Kusini leo. Makabila haya ni pamoja na
Akoli
na
Lwo
(si sawa na Luo) wanaoishi katika eneo la
Darfur
.
Kuna makabila mengine ya Waniloti yanayoishi nchini
Uganda
na
Tanzania
. Hii hasa ni kwa sababu ya Wajaluo kuvutiwa na
Ziwa Victoria
, ambako wanapatikana katika nchi hizi tatu (Uganda, Tanzania na Kenya). Nchini Uganda, wanajulikana kwa kuanzisha
himaya
ya
Waganda
na ya himaya ya
Watoro
. Wajaluo nchini Kenya walipigana vita na majirani wao, hasa Wakalenjin, ili kulidhibiti ziwa hilo.
Leo hii, utamaduni wa Wamaasai unajulikana sana kwa kuangaziwa vilivyo na utalii, hata hivyo Wamaasai ni asilimia ndogo ya idadi ya Wakenya kwa jumla. Wamaasai wanatambulika kwa kujipamba sehemu ya juu ya mwili na kwa vito.
Kenya ina utajiri mwingi wa
muziki
, vituo vya
runinga
na
maonyesho ya sanaa
.
Elimu
Mfumo wa elimu nchini Kenya unajumuisha elimu ya
chekechea
,
ya msingi
, ya
sekondari
na ya
vyuo
. Elimu ya watoto wadogo aghalabu huchukua miaka mitatu, ya msingi miaka minane, sekondari minne na chuo kikuu miaka minne au sita kwa kutegemea kozi.
Shule za chekechea, ambazo ni za watoto wa umri wa miaka mitatu hadi mitano, ni sehemu muhimu ya mfumo huu wa elimu na ni kigezo muhimu kabla ya kusajiliwa katika darasa la kwanza (Gredi ya Kwanza).
Mwishoni mwa elimu ya msingi wanafunzi hufanya mtihani wa Cheti cha Kuhitimu Masomo ya Msingi Kenya (KCPE), ambao huamua watakaojiunga na shule ya sekondari au vyuo vya ufundi. Umri wa shule ya msingi ni miaka 6/7 hadi 13/14.
Wale wanaojiunga na shule ya upili hufanya mtihani wa taifa mwishoni mwa kidato cha nne - Mtihani wa Cheti cha Kuhitimu Masomo ya Shule ya Upili Kenya (KCSE), ambao huamua watakaojiunga na vyuo vikuu, vyuo vya taatuma nyinginezo au kuajiriwa. Baraza Kuu la Usajili (JAB) ndilo lenye jukumu la kuwachagua wanafunzi watakaojiunga na vyuo vikuu vya umma. Mbali na shule za umma, kuna shule nyingi za binafsi nchini, hasa katika sehemu za miji. Vilevile, kuna shule kadhaa za kimataifa zinazofundisha mifumo mbalimbali ya elimu ya ng'ambo.
Historia ya elimu
Mfumo wa kwanza wa elimu nchini Kenya baada ya uhuru uliletwa na wakoloni Waingereza. Baada ya nchi kupata uhuru tarehe 12 Desemba 1963, Tume ya Ominde iliundwa ili kuleta mabadiliko ambayo yaakisi matarajio ya taifa huru la Kenya. Tume hii ilimulika masuala ya usawa na umoja, ambayo yalikuwa muhimu hasa wakati huo. Mabadiliko ya kilichofundishwa katika historia na jiografia yalifanywa ili kuakisi umoja wa kitaifa. Kati ya miaka 1964 na 1985, mfumo wa 7-4-2-3 ulifuatwa (miaka saba masomo ya msingi, miaka minne sekondari ya daraja la chini, miaka miwili sekondari ya daraja la juu, na miaka mitatu masomo ya chuo kikuu). Shule zote zilifuata
mtaala
mmoja.
Mwaka wa 1981, kamati iliyoteuliwa na rais kuratibu namna ya kuanzisha chuo kikuu cha pili nchini Kenya, na pia kuubadilisha mfumo wa elimu kwa jumla, ilianza kazi yake. Kamati hii ilipendekeza kuwa mfumo ule wa 7-4-2-3 ubadilishwe kuwa mfumo wa 8-4-4 (miaka minane shule ya msingi, miaka minne shule ya upili, miaka minne elimu ya chuo kikuu). Jedwali lililo katika Elimu ya Sasa Nchini Kenya linaonyesha muundo wa mfumo wa 8-4-4. Ingawa mfumo wa 7-4-2-3 kinadharia ulifikia kikomo mfumo wa 8-4-4 ulipoanzishwa mwaka wa 1985, kundi la mwisho la mfumo huo wa awali lilihitimu kutoka vyuo vikuu vya Kenya mwaka wa 1992.
Elimu nchini Kenya sasa
Mfumo wa sasa wa 8-4-4 ilizinduliwa Januari 1985. Ulitilia mkazo masomo ya kiufundi kwa matarajio kuwa, muundo huu mpya utawawezesha wanaoacha shule katika viwango mbalimbali aidha kujiajiri wenyewe au kupata ajira katika sekta ya juakali.
Mnamo Januari 2003, Serikali ya Kenya ilitangaza kuanzishwa kwa masomo ya shule za msingi bila malipo. Hili lilipelekea kuongezeka kwa wanafunzi waliojiunga na shule za msingi kwa asilimia 70. Hata hivyo, idadi ya waliojiunga na shule za upili na vyuo haikuongezeka sana kwa sababu malipo bado yalihitajika ili kuhudhuria masomo.
Mtihani wa kuhitimu cheti cha masomo ya msingi nchini Kenya (KCPE) hufanywa katika darasa la nane. Matokeo ya mtihani huu huhitajika ili kusajiliwa katika shule ya upili. Mtihani wa kuhitimu cheti cha masomo ya shule ya upili nchini Kenya (K.C.S.E.) hufanywa katika kidato cha nne. Wanafunzi hufanya mtihani katika masomo nane.
Ukosoaji
Mfumo wa elimu wa Kenya 8-4-4 umepitia mengi magumu katika kipindi kirefu ulichodumu. Punde tu baada ya kufuzu kwa kundi la kwanza la wanafunzi wa mfumo huu mwaka wa 1989, wananchi wengi walijitokeza kuilaumu na kuihukumu serikali kwa kuuanzisha mfumo huu. Wakosoaji hao walidai kuwa waliohitimu hawajaandaliwa vyema na hawangeweza kushindana na wenzao kutoka sehemu nyingine za
ulimwengu
. Wengine walihoji kuwa waliofuzu kupitia mfumo huu walikuwa aidha wachanga sana au hawajaandaliwa vyema kwa nafasi za kazi zilizokuweko. Serikali haikusikiliza hayo yote pengine kwa sababu uwezekano wa kuubadilisha na kuuunda upya kungeigharimu pesa nyingi.
Hata hivyo, kwa miaka mingi waliofuzu kupitia mfumo huu wamewaaibisha walioupinga kwa kufualu katika vyuo vya nchini na ng’ambo. Pia wasomi na wafanyakazi wa afya kuhamia
nchi zilizoendelea
ni dhihirisho tosha la hali hii.
Mkazo uliotiliwa masomo ya ufundi umefifia na mabadiliko ya hivi juzi katika mtaala yanasisitiza
teknolojia
ya
upashanaji habari
,
sayansi
,
hesabu
na lugha. Kwa vyovyote vile, kazi ya kiakademia na kusisitizwa kwa kupita mitihani iliyoandikwa hakujaacha nafasi kwa
useremala
,
uashi
,
upishi
na mafunzo mengine ya
ufundi
.
Michezo
Kenya hushiriki katika
michezo
mbalimbali ikiwemo
kriketi
,
mbio za magari
,
soka
,
raga
na
ngumi
.
Lakini nchi hii inajulikana hasa kwa kutawala katika
mbio za masafa ya kadiri
na
mbio za masafa marefu
. Kenya, kwa muda mrefu, imetoa
mabingwa
wa
Olimpiki
na
michezo ya Jumuia ya Madola
katika nyanja mbalimbali, hasa katika mbio za mita 800, mita 1,500, mita 3,000 kuruka viunzi na maji, mita 5,000, mita 10,000 na mbio za masafa marefu.
Wanariadha
wa Kenya (hasa wa kabila la Wakalenjin) wanaendelea kutawala mbio za masafa ulimwenguni, ingawa ushindani kutoka nchi ya
Moroko
na Ethiopia umepunguza umaarufu huu.
Wanariadha
wa Kenya wanaosifika sana ni pamoja na mshindi mara nne wa mbio za masafa marefu za
Boston
kwa
wanawake
na mshindi mara mbili wa mbio za dunia
Catherine Ndereba
, aliyeshikilia rekodi ya awali ya mbio za dunia
Paul Tergat
, na
John Ngugi
.
Wakati wa michezo ya Olimpiki ya
Beijing
Kenya ilishinda
medali
6 za
dhahabu
, 4 za
fedha
, 4 za
shaba
na kulifanya taifa lililofaulu sana barani Afrika katika michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008. Wanariadha wapya walitambulikana, kama
Pamela Jelimo
, mshindi wa medali ya dhahabu katika mbio za mita 800 kwa wanawake aliyejitahidi na kushinda tuzo la Golden League, na
Samuel Wajiru
aliyeshinda mbio za masafa marefu kwa wanaume.
Bingwa mstaafu wa mbio za Olimpiki na za Jumuia ya Madola,
Kipchoge Keino
, alisaidia kuanza ubingwa wa mbio za masafa marefu
miaka ya 1970
akafuatwa na bingwa wa michezo ya Jumuia ya Madola,
Henry Rono
, aliyeshikilia rekodi kadhaa za dunia.
Hivi majuzi, kumekuwa na mzozo wa wanariadha wa Kenya waliosaliti nchi yao na kuwakilisha nchi nyingine, hasa
Bahrain
na
Qatar
.
Wizara ya michezo
ya Kenya imejaribu kuzuia usaliti huu, lakini umeendelea tu,
Bernard Lagat
akiwa wa mwisho, akichagua kuiwakilisha
Marekani
.
[36]
Usaliti huu, kwingi unatokana na sababu za kiuchumi au kifedha ingawa pia wanariadha wazuri wasioweza kufaulu katika timu nzuri ya taifa huona ni rahisi kufaulu kwa kukimbilia nchi nyingine.
Kenya pia imetawala
voliboli
ya wanawake barani Afrika, huku vilabu na
timu ya taifa
vikishinda mashindano kadhaa barani Afrika katika
mwongo
uliopita. Timu ya wanawake pia imeshiriki katika michezo ya Olimpiki na Mashindano ya Ulimwengu ingawa haijafaulu vilivyo.
Mchezo wa kriketi ni maarufu na pia ni mchezo wa timu ambao umefaulu sana. Kenya imeshiriki katika
Kombe la Dunia la Kriketi
tangu mwaka
1996
. Timu hii ilishinda baadhi ya timu maarufu ulimwenguni na kufikia
semifainali
katika mchuano wa mwaka
2003
. Walishinda ligi ya kriketi ya dunia daraja la 1 iliyofanyika Nairobi kwa mara ya kwanza, kisha wakashiriki katika mchuano wa ulimwengu wa T20.
Nahodha
wa sasa wa timu ni
Collins Obuya
.
Kenya imejiundia jina katika muungano wa raga. Mchezo huo ni maarufu nchini hasa kwa sababu ya mchuano wa kila mwaka wa Safari Sevens. Timu ya Kenya ya raga ya wachezaji
saba
kila upande ilikuwa nambari ya 9 katika michezo ya dunia ya wachezaji saba IRB katika msimu wa mwaka 2006.
Kenya ilikuwa bingwa wa soka katika eneo hili lakini ubingwa huu umefifia kutokana na kutoelewana kwa maafisa wa Kamati ya Soka Nchini.
[37]
Mizozo hii ilipelekea Kenya kupigwa marufuku na FIFA, lakini marufuku hii iliondolewa mnamo Machi 2007.
Kwa upande wa mbio za magari, Kenya ndio waandalizi wa mbio za magari maarufu za
Safari Rally
zinazotambulika kuwa ngumu zaidi ulimwenguni,
[38]
na ambazo ni sehemu ya Bingwa wa Mbio za Magari kwa miaka mingi hadi kuondolewa kwake baada ya mbio za 2002 kwa sababu ya matatizo ya kifedha. Baadhi ya
madereva
maarufu wa mbio za magari ulimwenguni walioshiriki na kushinda mbio hizi ni
Bjorn Waldegard
,
Hannu Mokkola
,
Tommi Makinen
,
Shekhar Mehta
,
Carlos Sainz
na
Colin McRae
. Ingawa mbio hizi bado huendelea kila mwaka kama sehemu ya kutafuta Bingwa wa Mbio za Magari Afrika, waandalizi wanatarajia kuruhusiwa kujiunga tena na Ubingwa wa Magari Ulimwenguni katika miaka michache ijayo.
Fasihi
Ngugi wa Thiong'o
ni mmoja wa
waandishi
maarufu wa Kenya.
Kitabu
chake
en:Weep Not, Child
ni ufafanuzi wa
maisha
yalivyokuwa Waingereza walipoitwaa Kenya. Hii ni
hadithi
kuhusu athari za Mau Mau katika maisha ya Wakenya asili. Kinavyochanganya maudhui - ukoloni, elimu, na mapenzi - kunakifanya kuwa kimojawapo kati ya vitabu bora vya hadithi barani Afrika.
Kitabu cha hadithi cha
M. G. Vassanji
The In-Between World of Vikram Lall
kilishinda tuzo la Giller Prize mwaka 2003. Hii ni hadithi ya kubuni ya Mkenya mwenye asili ya Kihindi na
familia
yake wavyojizatiti na mabadiliko ya kisiasa wakati wa ukoloni na baada ya ukoloni nchini Kenya.
Kuanzia mwaka wa 2003, jarida la fasihi
Kwani?
limekuwa likichapisha fasihi ya kisasa ya Kenya.
Uchumi
Baada ya uhuru, Kenya iliendeleza ukuaji wa kiuchumi haraka kupitia kwa uwekezaji wa umma, kuhimiza uzalishaji wa kilimo, na kushawishi uwekezaji wa watu binafsi na wageni katika viwanda. Pato la taifa lilikua kwa asilimia 6.6 kuanzia 1963 hadi 1973. Uzalishaji wa kilimo ulikua kwa asilimia 4.7 kila mwaka kwa kipindi hicho ukiwa umechochewa na ugawaji upya wa mashamba, kuanzishwa kwa kilimo cha mimea iliyoimarishwa, na kuanzisha mashamba mapya.
Hata hivyo, kati ya 1974 na 1993 ukuaji wa uchumi wa Kenya ulipungua. Kupungua kwa kilimo kulisababishwa na sera za kilimo zisizofaa, mikopo isiyotosha na vikwazo visiyofaa vya biashara ya kimataifa.
Mnamo mwaka wa 1993, Serikali ya Kenya ilianzisha mpango mkuu wa kuimarisha uchumi na kuufanya huru. Waziri mpya wa fedha na gavana mpya wa Benki Kuu ya Kenya walianza mikakati iliyofuatana kuimarisha uchumi kwa usaidizi wa
Benki ya Dunia
na
Shirika la Fedha la Kimataifa
). Kama sehemu ya mpango huu, serikali iliondoa usimamizi wa bei za bidhaa, leseni za uagizaji na uthibiti wa ubadilishaji fedha, kubinafsisha kampuni nyingi zilizomilikiwa na umma, kupunguza idadi ya wafanyi kazi wa serikali na kuanzisha sera madhubuti za kulinda fedha. Kuanzia mwaka wa 1994 hadi 1996 ukuaji halisi wa uchumi wa Kenya ulikadiriwa juu kidogo ya asilimia 4 kwa mwaka.
Hata hivyo, kati ya 1997 na 2000, uchumi uliingia kipindi cha kupungua au kutoimarika, kwa sababu ya hali mbaya ya anga na kupungua kwa shughuli za kiuchumi. Mwaka wa 2001 pato la taifa liliimarika kiasi kwani mvua ilirejea kunyesha karibu na viwango vya awali. Ukuaji wa kiuchumi uliendelea kuimarika kiasi mwaka wa 2002 na kufikia asilimia 1.4 mwaka wa 2003, asilimia 4.3 mwaka wa 2004, kisha asilimia 5.8 mwaka wa 2005.
Mnamo Julai 1997, Serikali ya Kenya ilikataa kutimiza makubaliano ya awali na IMF kuhusu mabadiliko ya utawala wake. Jambo hili lilisababisha kukatizwa kwa misaada kwa miaka 3, nayo Benki ya Dunia ikaubana mkopo wa dola milioni 90 za mpango wa kuufufua uchumi. Ingawa mabadiliko mengi ya kiuchumi yaliyofanywa kati ya 1993-94 yalibakia, wataalamu wa maswala ya kiuchumi wasiopendelea mabadiliko waliamini kuwa Kenya iliitaji mabadiliko zaidi, hasa ya kiutawala ili kuongeza ukuaji wa pato la taifa (GDP).
Serikali ya Kenya ilichukua hatua yakini za mabadiliko, pamoja na kuunda Tume ya Kupambana na Ufisadi (KACA), kuanzisha hatua za kuimarisha uwazi wa katika mikakati ya serikali kupata bidhaa na kupunguza fedha inayotumiwa na serikali kulipia mishahara. Mnamo Julai 2000, shirika la IMF lilitia saini dola milioni 150 za Poverty Reduction and Growth Facility (PRGF), nayo Benki ya Dunia ilifuatia na mkopo wa dola milioni 157 kuimarisha uchumi na kuibadilisha sekta ya umma. Mwezi wa Desemba 2000, iliamuliwa kuwa tume ya kupambana na ufisadi haikuwa ya kikatiba na sehemu za juhudi za mabadiliko kukatizwa mwaka 2001. Shirika la IMF na Benki ya Dunia zilikatiza mipango yao. Juhudi zilizofanywa kuanzisha upya mipango hii katikati ya mwaka wa 2002 hazikufaulu.
Chini ya uongozi wa Rais Kibaki, aliyechukua hatamu za uongozi tarehe 30 mwezi wa Desemba 2002, serikali ya Kenya ilianzisha mipango mipya na kabambe ya uimarishaji uchumi na imerejelea ushirikiano wake na Benki ya Dunia na IMF. Serikali mpya ya National Rainbow Coalition (NARC) iliidhinisha Sheria dhidi ya Ufisadi na Uhalifu wa Kiuchumi pamoja na Sheria ya Maadili ya Watumishi wa Umma mnamo Mei 2003 iliyolenga kupiga vita ufisadi katika ofisi za umma. Mabadiliko mengine, hasa katika idara ya sheria, kuagiza bidhaa za umma na kadhalika yamepelekea kurejelewa kwa misaada na matumaini ya kuimarisha uchumi. Kufuatia kupitishwa kwa sheria muhimu za kupambana na ufisadi na serikali mpya, wafadhili walirejelea ufadhili mwezi wa Novemba 2003 na IMF ikaidhinisha msaada wa miaka mitatu wa dola milion 250 ili kupunguza umaskini na kuimarisha uchumi. Wafadhili wakatoa dola bilioni 4.2 kama msaada wa miaka minnne. Kurejelewa kwa ufadhili na kujihusizisha upya kwao kumevutia imani ya wawekezaji.
Mswada wa
ubinafsishaji
umeidhinishwa ingawa kuanzishwa kwa tume ya ubinafsishaji hakujakamilika, mabadiliko katika utendakazi wa umma yametekelezwa na mwaka wa 2007 Kenya ilishinda tuzo la Umoja wa Kimataifa la Utendakazi wa Umma.
[39]
[40]
Hata hivyo, kazi nyingi zinahitajika kufanywa ili kuiwezesha nchi hii kuyafikia mataifa yaliyoendelea sana kiuchumi, hasa yale ya Mashariki ya Mbali. Changamoto kuu ni pamoja na kuchukua hatua thabiti dhidi ya ufisadi, kupitisha sheria zinazoshughulikia ugaidi na biashara haramu, kutatua upungufu wa ufadhili wa bajeti kisha kurekebisha na kuunda miundo msingi. Inaaminika haya yatasaidia kudumisha sera za kimsingi za kiuchumi, na kuhakikisha ukuaji wa kasi wa kiuchumi uliofikia asilimia 7.2 mwaka wa 2007.
Mwaka wa 2007, serikali ya Kenya ilizindua
Ruwaza 2030
, ambao ni mpango wa kiuchumi wenye matumaini makuu na ambao ikiwa utatekelezwa kikamilifu, una uwezo wa kuifanya nchi hii kuwa katika kiwango sawa na mataifa yaliyoendelea kiuchumi ya Asia.
Nairobi inaendelea kuwa kituo muhimu na cha kimsingi kwa mawasiliano na biashara cha Afrika Mashariki. Kinajivuna kuwa na miundo msingi ya uchukuzi na mawasiliano bora zaidi katika eneo hili, na wafanyi kazi wenye ujuzi. Makampuni mengi ya kigeni hudumisha matawi yao katika eneo hili ama ofisi za kuyawakilisha mjini Nairobi. Mnamo Machi 1996, Marais wa Kenya, Tanzania na Uganda waliifufua Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC). Shabaha za EAC ni pamoja na kusawazisha kodi na ada zinazotozwa bidhaa, utembeaji huru wa watu na kuimarisha miundo msingi katika eneo hili. Nchi hizi tatu za Afrika Mashariki zilitia saini mkataba wa Customs Union Agreement mwezi wa Machi 2004.
Muhtasari wa uchumi wa nchi
|
Pato la taifa
|
Dola bilioni 41.84 (2012) kwa bei ya sasa. Dola bilioni 76.07 (Uwezo wa kununua bidhaa usio sawa, 2012) Kuna pia uchumi mkubwa usio rasmi ambao haujawahi kujumuishwa kama sehemu ya pato la taifa.
|
Ukuaji wa kiuchumi kwa mwaka
|
5.1% (2012)
|
Pato la kila mtu kwa mwaka
|
Pato la kila mtu kwa mwaka (PPP)= $1,800
|
Malighafi ya kiasili
|
Wanyama wa pori, Ardhi (5% inayolimika)
|
Bidhaa za kilimo
|
Chai, kahawa, mahindi, ngano, miwa, mboga na matunda, pareto, bidhaa za maziwa, nyama na bidhaa za wanyama
|
Viwanda
|
Bidhaa za petroli, usagaji wa nafaka na miwa, saruji, pombe, vinywaji, nguo, uunganishaji magari, makaratasi, utengenezaji wa bidhaa za kimsingi, utalii
|
Biashara ya mwaka 2012
Biasharanje
|
Dola bilioni 5.942
|
chai, kahawa, bidhaa za mboga na matunda, bidhaa za petroli, saruji, samaki
|
Masoko muhimu (2012)
[5]
|
Uganda, Tanzania, Uholanzi, Uingereza, Marekani, Misri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
|
Maduhuli
|
Dola bilioni 14.39
|
mashine, magari, bidhaa za petroli, vyuma, resini na bidhaa za plastiki
|
Mataifa muhimu yaletayo bidhaa Kenya
|
China, Uhindi, Muungano wa Falme za Kiarabu, Saudi Arabia, Afrika Kusini, Ujapani
|
Utafutaji wa mafuta
Mwanzoni mwa mwaka wa
2006
Rais wa
Uchina
,
Hu Jintao
, alitia saini kandarasi ya utafutaji wa mafuta na Kenya. Haya ndiyo makubaliano ya hivi punde kati ya mfululizo wa mapatano yaliyopagwa kuelekeza maliasili ya Afrika huko Uchina ambako uchumi wake waendelea kukua kwa haraka.
Kandarasi hii iliwezesha kampuni inayoongozwa na taifa la Uchina “offshore oil and gas company” CNOOC Ltd kutafuta mafuta Kenya, ambayo ilianza kuchimba visima vya kwanza mpakani mwa Sudan na Somalia na katika maji ya upwa wake.
[41]
Tazama pia
Marejeo
- ↑
1.0
1.1
"World Economic Outlook database: April 2022"
.
imf.org
.
- ↑
Kabla ya mwaka wa
1920
, eneo linaloitwa Kenya liliitwa
Himaya ya Uingereza Afrika Mashariki
, kwa hiyo hapakuwa na haja ya kutaja neno
mlima
uliporejelea mlima huo.
- ↑
The Times|articlename=British East Africa Annexed--"Kenya Colony"
|author=Reuter|section=News|day_of_week=Thursday|date=8 Julai 1920|page_number=13|issue=42457|column=C
- ↑
"East Africa: Kenya: History: Kenya Colony".
Encyclopedia Britannica
.
17
(15 ed.). 2002. pp. 801, 1b.
ISBN 0-85229-787-4
.
- ↑
5.0
5.1
5.2
Hitilafu ya kutaja: Invalid
<ref>
tag; no text was provided for refs named
CIA World factbook Kenya
- ↑
Rough Guide (2006).
Rough Guide Map Kenya
[map], 9 edition, 1:900,000, Rough Guide Map. Cartography by World Mapping Project.
ISBN 1-84353-359-6
.
- ↑
[1]
,
ABC News Online,
2005/03/10
- ↑
8.0
8.1
8.2
Wonders wa Afrika World -
PBS
- ↑
Hybrid Urbanism By Nezar Al-Sayyad
- ↑
Dispersal Afrika katika Deccan By Shanti Sadiq Ali
- ↑
Kiswahili Coast.
Archived
30 Desemba 2007 at the
Wayback Machine
. Nationalgeographic.com.
- ↑
Sultani wa Malinda, PBS
- ↑
"Ismaili muslim"
. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2009-01-03
. Iliwekwa mnamo
2021-01-16
.
- ↑
Sikh
- ↑
The Times|articlename=British East Africa Annexed--"Kenya Colony"|author=Reuter|section=News|day_of_week=Thursday
|date=8 Julai 1920|page_number=13|issue=42457|column=C
- ↑
- ↑
"
Kenya
".
Oxford English Dictionary
. Oxford University Press. 2nd ed. 1989.
- ↑
The Spelling ya Kenya.
BJ Ratcliffe. Journal ya Royal African Society, Vol. 42, Namba 166 (Januari 1943), uk. 42-44
- ↑
- ↑
Castro, Alfonso Peter (1995).
Facing Kirinyaga
. London: Intermediat Technology Publications Ltd.
ISBN
1-85339-253-7
.
- ↑
"Tunataka nchi yetu"
Archived
23 Julai 2013 at the
Wayback Machine
.. Wakati. 5 Novemba 1965.
- ↑
Kenya, AfricaGenWeb
- ↑
Post-Uhuru Low intensiteten Conflict Nchini Kenya
- ↑
E. H., Campbell (2006). "Urban Refugees in Nairobi: Problems of Protection, Mechanisms of Survival, and Possibilities for Integration".
Journal of Refugee Studies
.
19
(3): 396.
doi
:
10.1093/jrs
.
;
- ↑
Wapiga kura wengi kukaa nyumbani kama Kenya Drops Secret Ballot katika Uchaguzi Parliamentary
http://www.highbeam.com/doc/1P2-1241691.html
Archived
15 Februari 2011 at the
Wayback Machine
.: The Washington Post Kifungu tarehe: 25 Februari 1988 Author: Blaine Harden
- ↑
religiousfreedom.lib.virginia.edu / rihand / Kenya.html
- ↑
ghasia za uchaguzi Kenya unatishia mafanikio yake ya kiuchumi
http://www.chinadaily.com.cn/language_tips/auvideo/2008-01/07/content_6375707.htm
- ↑
"Nakala iliyohifadhiwa"
. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2009-07-15
. Iliwekwa mnamo
2009-12-07
.
- ↑
'Hope is back' kwa Kenya - CNN.com
Archived
5 Machi 2008 at the
Wayback Machine
. saa edition.cnn.com
- ↑
wabunge Kenya kupitisha sheria ya kugawana madaraka-english.aljazeera.net/NR/exeres/111A3F40-0FD9-4DCB-ACB0-822D1E3A09EA.htm Al Jazeera Kiingereza 18 Machi
- ↑
Horror ya Kenya's 'Witch' lynchings
- ↑
Mob nzito kifo 11 Kenya 'witches'
- ↑
Kenya Roads Board
Constituency ufadhili chini ya RMLF
Archived
13 Januari 2008 at the
Wayback Machine
.
- ↑
34.0
34.1
"The World Fact Book: Kenya"
. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2020-08-31
. Iliwekwa mnamo
21 Juni
2014
.
- ↑
US Department of State
- ↑
Hitilafu ya kutaja: Invalid
<ref>
tag; no text was provided for refs named
IAAF
- ↑
New Vision, 3 Juni 2004:
Wrangles ardhi Kenya utan faststalld FIFA marufuku
Archived
10 Januari 2008 at the
Wayback Machine
.
- ↑
The Auto Channel, 21 Julai 2001:
FIA Rally: Delecour inachukua pointi kumaliza tarehe Safari Rally kwanza
- ↑
"Nakala iliyohifadhiwa"
. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2008-02-15
. Iliwekwa mnamo
2009-12-07
.
- ↑
"Nakala iliyohifadhiwa"
(PDF)
. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
(PDF)
mnamo 2009-03-24
. Iliwekwa mnamo
2009-12-07
.
- ↑
Barber, Lionel; Andrew England. "
China's scramble for Africa finds a welcome in Kenya
", Financial Times, 10 Agosti 2006. Retrieved on 2008-06-27.
Viungo vya nje
- Serikali
- Jumla
- Vyombo vya habari
- Utalii
- Historia
- Nyingine
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Afrika
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Kenya
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|