Jeshi
ni
kundi
kubwa la
watu
wanaopewa
mamlaka
ya kutumia nguvu ya
silaha
kutetea nchi kwa niaba ya
dola
au kutekeleza maagizo ya
serikali
dhidi ya maadui wa nje.
Neno
linatumika hasa kwa kutaja
jeshi la ardhi
,
jeshi la wanamaji
na
jeshi la anga
.
Kazi ya jeshi ni
- kulinda nchi dhidi ya maadui wa nje
- kutetea nchi dhidi ya mashambulizi kutoka nje au
- pia kushambulia nchi nyingine kama hatua hii imeamriwa na serikali halali.
Kusudi hilo dhidi ya hatari ya nje ndiyo tofauti kuu na
kazi
ya
polisi
ambayo ni
mkono
mwingine wa serikali ya
taifa
wenye silaha. Hata hivyo kuna nchi ambako tofauti kati ya jeshi na polisi si wazi vile, hasa kuna nchi nyingi ambako jeshi limepewa
wajibu
wa ndani ya taifa au ambako wanajeshi walichukua mamlaka
mikononi
mwao kwa nguvu ya silaha.
Katika nchi mbalimbali kuna vikosi vinavyotekeleza shughuli ndani ya taifa lakini vina silaha sawa na sehemu za jeshi na wakati mwingine vinahesabiwa kama sehemu ya jeshi. Kwa mfano vikosi vinavyolingana na
FFU
ya
Tanzania
vinaitwa
gendarmerie
huko
Ufaransa
na nchi nyingi za
Afrika Magharibi
au
carabinieri
huko
Italia
na kule vinahesabiwa kama mkono wa jeshi ingawa kazi yao ni ya ndani ya nchi.
Hali ya jeshi vitani husimamiwa na
sheria ya kimataifa ya vita
jinsi ilivyoundwa katika
mikataba
mbalimbali ya kimataifa.
Sheria
hiyo inalenga kulinda
raia
wakati wa
vita
na pia
haki
za
wanajeshi
wakikamatwa na adui. Sheria inadai ya kwamba wanajeshi wote wanahitaji
- kuwa na
sare
rasmi inayoonekana na kuwatofautisha na raia
- kuwa chini ya mamlaka rasmi inayoeleweka na kuwajibika kwa serikali yao
- kubeba silaha zao wazi
- kutimiza masharti ya sheria ya kimataifa
Wanajeshi wanafuata utaratibu huo wanalindwa na sheria inayokataza pia raia kubeba na kutumia silaha na kushiriki katika mapigano. Katika vita nyingi sheria ilipuuzwa lakini kuna mifano kadhaa katika
karne ya 20
ambapo
jinai za vitani
zilifuatiliwa kwa mfano kwenye
Kesi za Nuremberg
kuhusu jinai za vitani upande wa
Ujerumani
na
kesi
zilizofikishwa mbele ya
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai
tangu
mwaka
2000
.
Jeshi la ardhi lina
kituo
ama
kambi
ambayo kambi hii yaweza kulinda makundi ya Jeshi, divisheni ama umma wa jeshi. Kukitokea vita, Jeshi huwa wakipeleka divisheni na makundi ya kijeshi kwa vipimo kulingana na vita na mbinu za kusukuma ama kushinda adui kwa
vita
. Na pia ratili ya vita ikiwapendukia, Jeshi hupeleka wanajeshi pulikiza ili kusukuma adui kabisa ama kumshinda.
Jeshi la Taifa ni chombo kilichoanzishwa kisheria chenye silaha na askari wenye mafunzo ya kivita amabao kazi yao ni kupambana kivita kulinda ardhi ya nchi husika dhidi ya
uvamizi
kutoka nje. Nchi huwa na jeshi moja la kulinda mipaka yake dhidi ya uchokozi kutoka nje, lakini pia huwa na majeshi 'Usu' kadhaaa kwaajili ya kulinda usalaama wa ndani. kwa mfano; majeshi ya nchi ni kama Jeshi la
Uganda
(UPDF),
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
(TPDF). Majeshi Usu ni kama Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na TANAPA.
Shughuli nyingi za majeshi hutofautiana kulingana na kitengo husika cha jeshi, kwa mfano jeshi la nchi kavu,Jeshi la Anga na Jeshi la Majini, haya ndiyo matawi makuu matatu ya jeshi . Kwa historia, Jeshi la anga lilikuwa pamoja na Jeshi la ardhini, hasa kwa historia ya
Uchina
ama
Jeshi la ukombozi wa umma wa Uchina
ilichanganya (jeshi la ardhi, jeshi la majini, jeshi la anga, divisheni za makombora na usayari) kwa tawi moja.
Majeshi ya kisasa yaitwa pia
huduma
, ama
askari watawala
). Hii inaweza kuhusu pia matawi ya
Vita
:
jeshi la nchi kavu
,
vifaru
,
makombora
, na
mhandisi wa jeshi
, na pia
Wasafirishaji
wa matawi kama:
mawasiliano
,
watambuzi
,
daktari
,
wapeleka vifaa
, na
Jeshi la ndege
(tofauti na jeshi la anga).