Uhindi
(pia:
India
) ni
nchi
kubwa ya
bara
la
Asia
, upande wa
kusini
, ikienea hasa katika
rasi
kubwa ya
Bahari ya Hindi
.
Kwa eneo ina nafasi ya saba
duniani
, lakini kwa
idadi
ya wakazi (1,352,642,280 mwaka
2018
) ni nchi ya pili baada ya
China
. Kati ya nchi za ki
demokrasia
ndiyo yenye watu wengi zaidi duniani. Tena inakadiriwa kwamba miaka ya hivi karibuni itapiku China.
Imepakana na
Pakistan
,
China
,
Nepal
,
Bhutan
,
Bangladesh
na
Myanmar
.
Kiutawala Uhindi ni
shirikisho
la
jamhuri
lenye majimbo ya kujitawala 29 pamoja na maeneo ya shirikisho 7.
Mji mkuu
ni
New Delhi
, lakini
mji
mkubwa zaidi ni
Mumbai
.
Historia
Historia ya awali
Binadamu
walifika India kutoka
Afrika
kabla ya miaka 55,000 iliyopita. Uwepo wao wa muda mrefu, kwanza kama
wawindaji-wakusanyaji
waliozagaa
barani
, umefanya watu wa eneo hilo wawe na tofauti kubwa kati yao upande wa
urithi wa kibiolojia
, ambayo inapitwa na Waafrika tu.
Makazi ya kudumu yalianza
magharibi
, katika
beseni
la
mto Indus
, miaka 9,000 iliyopita, hata kuzaa
ustaarabu
maalumu (Indus Valley Civilisation) katika
milenia ya 3 KK
.
Kabla ya ukoloni
Kufikia
mwaka
1200 KK
,
Kisanskrit cha Kale
, mojawapo kati ya
lugha za Kihindi-Kiulaya
, kilikuwa kimeenea India kutoka
Kaskazini
-Magharibi, kikawa
lugha
ya
Rigveda
, mwanzoni mwa
dini
ya
Uhindu
. Hivyo
lugha za Kidravidi
zikakoma kaskazini.
Kufikia mwaka
400 KK
,
matabaka
ya kudumu katika
jamii
yalikuwa yamejitokeza katika Uhindu. Hapo dini za
Ubuddha
na
Ujaini
zilitokea, zikipinga taratibu hizo za kibaguzi. Katika
bonde
la
mto
Gange
yalianza
madola
ya
Maurya
na
Gupta
. Ndani yake hadhi ya
wanawake
ilirudi nyuma, na mtazamo wa kwamba baadhi ya watu hawatakiwi hata kuguswa ukaimarika. Huko India
Kusini
, Falme za Kati zilieneza
maandishi
na
tamaduni
vya lugha za Kidravidi kwa
falme
za Asia Kusini
Mashariki
.
Kati
karne
za kwanza baada ya
Kristo
, dini za
Ukristo
,
Uislamu
,
Uyahudi
na
Uzoroastro
pia zilitia mizizi katika
pwani
za Kusini.
Majeshi
kutoka
Asia ya Kati
yalivamia kwa
kwikwi
mabonde ya India, hata kuunda
usultani
wa
Delhi
na kuingiza India Kaskazini katika
umma
wa Kiislamu.
Katika
karne ya 15
BK
,
Dola la Vijayanagara
liliunda utamaduni wa kudumu wa Kihindu kusini mwa India. Katika
Punjab
,
Usikh
ulianzishwa, ukipinga
dini rasmi
.
Dola la Mughal
, mwaka
1526
, liliwezesha karne mbili za
amani
na kuacha
urithi
wa
usanifu majengo
bora.
Wakati wa ukoloni
Uhindi wa Kiingereza
ni kipindi cha
historia
ambapo nchi za
Bara Hindi
ama zilitawaliwa na
Uingereza
moja kwa moja ama zilikuwa chini ya usimamizi wa Uingereza kama
nchi lindwa
.
Utawala huo ulienea juu ya Uhindi wa leo pamoja na
Pakistan
,
Bangladesh
,
Nepal
na kwa muda pia juu ya
Burma
(
Myanmar
).
Utawala wa Kiingereza ulikuwa na vipindi viwili vifuatavyo:
Tarehe
31 Desemba
1600
malkia
Elizabeth I
alitoa hati ya ulinzi wa kifalme kwa
biashara
kati ya Uingereza na "Uhindi wa Mashariki".
Kampuni iliyopokea hati hii ilikuwa kundi la
wafanyabiashara
na
matajiri
wa
London
waliovutwa na
utajiri
wa nchi za mashariki na hasa na
faida
kubwa mikononi mwa wafanyabiashara
Wareno
na
Waholanzi
waliotangulia katika biashara kati ya
Ulaya
na nchi za
Asia ya Kusini
.
Kampuni ilishindana kibiashara na kivita na wafanyabiashara wa
Ureno
, wa
Uholanzi
na wa
Ufaransa
. Iliweza kununua au kuvamia vituo vya biashara na kujenga maboma yake kuanzia mwaka
1644
huko
Bombay
,
Madras
na penginepo.
Mwaka
1717
kampuni ilipata kibali cha mtawala wa
Moghul
cha kusamehewa
kodi
kwa biashara katika
Ubengali
.
Tangu mwaka
1680
kampuni ilianzisha
jeshi
lake la
maaskari
Wahindi na kuwa mshiriki katika
siasa
ya Uhindi.
Kati ya miaka
1756
na
1763
Uingereza pamoja na mataifa mengine ya Ulaya ilishiriki katika
Vita vya miaka saba
viliyokuwa vita vya kwanza vya kimabara. Waingereza walipigana pamoja na
Prussia
dhidi ya
Austria
,
Ufaransa
,
Urusi
na
Uswidi
. Jeshi la kampuni liliendesha vita hivyo dhidi ya maeneo ya Ufaransa katika Uhindi. Wafaransa walishindwa wakabaki na vituo vidogo tu katika miji kama
Pondicherry
na
Mahe
lakini kampuni iliongeza maeneo yake katika Uhindi.
Baada ya mwaka
1757
Kampuni ya Kiingereza ilikuwa enzi muhimu, iliweza kushindana hata na nguvu ya Moghul. Ilianza kutawala sehemu kubwa za Uhindi wa Kusini pamoja na Ubengali.
Kampuni ilitumia mbinu mbili:
- mikataba na madola ya watawala wa Kihindi waliokubali kupokea
mabalozi
wa kampuni kwao waliokuwa kama washauri wakuu wa
Maharaja
au
Nawab
wa eneo; siasa ya nje na mambo ya jeshi ziliwekwa chini ya kampuni
- uvamizi na utawala wa moja kwa moja, maeneo yale yalikuwa mali ya kampuni.
Mafaniko makubwa ya kampuni yalisababisha mgogoro huko Uingereza na
sheria
mbalimbali za
bunge la Uingereza
zililenga kuongeza athira ya
serikali
ya Uingereza juu ya shughuli za kampuni.
Katika
karne ya 19
kampuni ikawa mtawala wa sehemu kubwa za Uhindi, ama kwa njia ya mikataba na watawala wa kienyeji au kwa utawala wa moja kwa moja. Kampuni ilianza kubadilisha uso wa India kujenga
reli
na kuanzisha
mawasiliano
wa kisiasa kwa huduma ya
posta
na pia
simu
za
telegrafi
.
Mwaka
1857
ilitokea uasi wa wanajeshi Wahindi wa jeshi la kampuni uliosababisha na mkasi wa mabadiliko na dharau ya viongozi Waingereza kwa
utamaduni
wa wenyeji. Utawala wa kampuni ulianza kuporomoka; uliokolewa tu kwa kupeleka Uhindi wanajeshi kutoka Uingereza. Uasi ulikomeshwa kwa mabavu.
Lakini kuingilia kati kwa serikali ya Uingereza kulikuwa mwisho wa utawala wa kampuni. Mwaka
1858
serikali ya London ilichukua
madaraka
yote ya kampuni ikafanya Uhindi kuwa
koloni
la
taji
la Uingereza.
Utawala wa kiserikali kati ya
1858
hadi
1947
Kuanzia mwaka
1858
Uhindi ulitawaliwa kama
koloni
la Uingereza.
Kaisari
wa mwisho wa Moghul
Bahadur Shah Zafar II
aliondolewa nchini.
Malkia
Viktoria wa Uingereza
alichukua
cheo
chake akaitwa "
Kaisari
wa Uhindi" (kwa
Kiingereza
: "Empress of India"; kwa
Kihindi
: "Padishah-e-Hind") akamuachia
utawala
gavana
wake aliyepewa cheo cha "
makamu wa mfalme
" (Vice-Roy).
Muundo wa utawala uliendelea: maeneo ya kampuni yalikuwa makoloni ya Uingereza. Maeneo ya watawala Wahindi yalibaki yalivyo lakini kila
Maharaja
au
Nawab
alipaswa kula
kiapo
cha
utii
kwa malkia kama Kaisari au malkia mkuu wa Uhindi na kumkubali mshauri Mwingereza katika
jumba
lake kama mwakilishi wa Uingereza.
Mwisho wa
karne ya 19
harakati
za kutafuta
uhuru
zilianza upya. Mwaka
1885
chama
cha INC (
Indian National Congress
) kiliundwa na
Wahindu
na
Waislamu
pamoja waliodai uhuru. Mwaka
1906
viongozi Waislamu walitoka katika INC na kuunda "
Shirikisho la Waislamu
".
Mwaka
1917
Uingereza ulitamka ya kwamba ulitaka kuelekea polepole hali ya kujitawala kwa Wahindi. Viongozi wa wenyeji hawakuridhika na mkasi wa mabadiliko. Chini ya
uongozi
wa
Mahatma Ghandi
mwendo wa kupigania uhuru bila mabavu ulipata nguvu. Ghandi alipigania hasa
umoja
wa Wahindu na Waislamu lakini alipingwa na viongozi wenye
itikadi kali
wa pande zote mbili.
Baada ya
Vita Kuu ya Pili ya Dunia
Waingereza walikubali kujiondoa katika Uhindi. Swali kubwa lilikuwa kama nchi itabaki kama nchi moja au kama maeneo ya Waislamu yatajitenga.
Baada ya uhuru
Tarehe 14/
15 Agosti
1947
utawala wa Uingereza ulikwisha. Bara Hindi iligawanywa katika nchi mbili za
Uhindi
na
Pakistan
. Mgawanyo ulikuja na
vita
na kumwaga kwa
damu
nyingi.
Tarehe
30 Januari
1948
Ghandi mwenyewe aliuawa na Hindu mkali aliyemchukia kwa sababu alitaka
usawa
wa Waislamu na Wahindu.
Mgawanyiko wa kiutawala
Hii ni orodha ya
majimbo ya
Uhindi
:
Majimbo
Maeneo ya Muungano:
Watu
Lugha ya taifa
ni
Kihindi
, ambacho ni
lugha ya Kihindi-Kiulaya
, pamoja na
Kiingereza
ambacho pia ni
lugha rasmi
. Kuna
lugha
21 kubwa na lugha nyingi zisizo na wasemaji wengi sana.
Kusini mwa Uhindi watu husema
lugha za Kidravidi
kama
Kikannada
,
Kitelugu
,
Kitamil
na
Kimalayalam
.
Kaskazini
husema hasa
Kipunjabi
,
Kibengali
,
Kigujarati
na
Kimarathi
.
Lugha ndogo chache ambazo si lugha za Kihindi-Kiulaya (74 %) wala za Kidravidi (24 %) ni
lugha za Kisino-Tibeti
,
lugha za Kiaustro-Asiatiki
na
lugha za Kitai-Kadai
.
Visiwani
mwa
Andaman
, kulikuwa na
lugha za Kiandamani
lakini nyingi zao zimeshatoweka kabisa.
Wakazi walio wengi (79.8 %) hufuata
dini
ya
Uhindu
. Takriban 14.2 % ni
Waislamu
; hivyo Waislamu wa Uhindi ni jumuiya ya tatu katika
umma
wa Kiislamu duniani baada ya Waislamu wa
Indonesia
na Pakistan.
Dini nyingine ni
Ukristo
(2.3 %),
Usikh
(1,7 %),
Ubuddha
(0.7 %),
Ujain
(0.4 %),
Uzoroastro
na
Bahai
.
Tazama pia
Viungo vya nje
|
---|
Majimbo
| | |
---|
Union territories
| |
---|
Maeneo yanayodaiwa
na nchi jirani
pamoja na Uhindi
| |
---|
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Uhindi
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Uhindi
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|