Uswidi
(kwa
Kiswidi
: "Sverige") ni nchi ya
Skandinavia
katika
Ulaya ya Kaskazini
. Imepakana na
Ufini
(Finland) na
Norwei
.
Nchi imegawiwa katika mikoa mitatu:
Norrland
katika kaskazini,
Svealand
katikati na
Gotaland
katika kusini.
Ina
pwani
ndefu kwenye
bahari ya Baltiki
. Kuna daraja la kuvukia
mlango wa bahari
ya
Oresund
ya kuunganisha Uswidi na
Denmark
.
Kuna misitu mikubwa sana na ma
ziwa
mengi.
Hali ya hewa
ya sehemu kubwa ya Uswidi si
baridi
kutokana na
athira
ya
mkondo wa Ghuba
. Kuna tofauti kati ya
urefu wa mchana
katika miezi ya Mei hadi Julai na
giza
wakati wa Desemba. Tarehe
21 Juni
ni siku ndefu: hakuna giza kabisa na
usiku
wake Waswidi hufanya
sherehe
kubwa ya "midsommar" kwa
ngoma
na
dansi
kote nchini.
Mji mkuu
ni
Stockholm
, nao unaongoza kwa wingi wa wakazi.
Vilele vya juu kwa kila "landskap" ni kama ifuatavyo. Kumbuka kwamba "landskap" katika Uswidi ni sahihi kidogo tu. Basi maoni mengine kuwepo.
Wakazi wa kwanza kujilikana walikuwa
makabila
ya
Kigermanik
kama wakazi wote waliowafuata. Huko
Roma
Tacitus
aliandika juu yao mwaka
98
BK
.
Kati ya
karne ya 8
hadi
ya 11
waliitwa mara nyingi "
Waviking
" wakiogopwa na wenyeji wa
Ulaya
bara
kwa sababu Waviking walivamia mara kwa mara maeneo ya
pwani
kwa
jahazi
zao ndogo. Lakini Waviking au
Wanormani
ni neno la kutaja watu wa Kaskazini waliovamia na kufanya
ujambazi
kwenye nchi za Ulaya bara si namna jinsi wenyewe walivyojiita.
Malkia
Margarete I
wa
Udani
aliolewa na mfalme wa
Norway
. Baada ya kifo cha
mumewe
alitawala nchi zote mbili na baadaye pia
Uswidi
. Mwaka
1397
wawakilishi wa falme tatu zilikutana katika mji wa
Kalmar
(Uswidi ya kusini) na kuelewana juu ya "
Umoja wa Kalmar
" yaliyounganisha nchi zote za
Skandinavia
chini ya mfalme wa Denmark ilhali kila nchi iliendelea kujitawala. Wakati ule
Ufini
(Finland) ilikuwa chini ya Uswidi.
Iceland
na
Visiwa vya Faroe
ziliingia pia kwa sababu zilikuwa chini ya Norway wakati ule.
Umoja
huo uliendela hadi mwaka
1521
. Waswidi walianza kuchoka na
utawala
wa Kidenmark wakaondoka katika umoja huu mwaka
1521
pamoja na
Ufini
. Lakini Norway iliendela kuwa chini ya Denmark hadi mwaka
1814
.
Uswidi ulijiunga na
Matengenezo ya Kiprotestanti
na
kanisa la Kilutheri
likawa
dini rasmi
nchini hadi mwaka
2000
. Hivyo Uswidi ikawa kati ya nchi muhimu sana ya Ulutheri.
Uswidi ulistawi na kueneza himaya yake kuanzia
karne ya 17
hadi mwanzo wa
karne ya 18
kama mojawapo kati ya nchi zenye nguvu zaidi Ulaya.
Baadaye ilirudi nyuma hadi kunyang'anywa kwa
Ufini
na
Warusi
(
1809
).
Kati ya miaka
1814
na
1905
ililazimisha Norwei kukubali mfalme wa Uswidi kama mfalme wa Norwei pia.
Tangu hapo Uswidi umeshika msimamo wa
amani
na wa kutoshikamana na nchi yoyote.
Kwa sasa Uswidi ni
ufalme wa kikatiba
yaani Mkuu wa Dola ni
mfalme
(kwa sasa
Carl XVI Gustaf
), lakini huyu mfalme anapaswa kufuata
sheria
ya
katiba
ya nchi. Utawala umo mikononi mwa
serikali
iliyochaguliwa ki
demokrasia
.
Katika
karne ya 20
Uswidi umefaulu vizuri kujenga
uchumi
ili kuondoka katika
umaskini
na kuwa moja kati ya
nchi tajiri
za
dunia
(ikiwa na nafasi ya 8 kwa pato la kichwa).
Nchi ilijiunga na
Umoja wa Ulaya
mwaka
1995
lakini haikukubali
pesa
ya
Euro
ikaendelea na
Krona ya Uswidi
.
Uswidi ni nchi kubwa yenye wakazi wachache: mwaka 2017 kwa mara ya kwanza wamezidi milioni 10, wengi wao wenye asili ya
makabila ya Kijerumani
, lakini kwa sasa 32.2% wana
damu
tofauti au mchanganyiko.
Lugha rasmi
ni
Kiswidi
, ambacho kinafanana sana na
Kidani
na
Kinorwe
.
Lugha
ya pili kati ya tano zilizokubalika kwa makundi madogo ya asili ni
Kifini
(5%), lakini siku hizi
uhamiaji
umefanya
Kiarabu
kiwe na watumiaji wengi zaidi.
Asilimia
89 wanaweza kuongea
Kiingereza
pia.
Upande wa
dini
, 57.7% ni
Walutheri
, lakini kati yao 2% tu wanashiriki
ibada
ya kila wiki.
Waprotestanti
wengine ni 275,000,
Waorthodoksi wa Mashariki
100,000 na
Wakatoliki
92,000.
Waislamu
ni kama 600,000, lakini wengi hawashiriki, na 25,000 tu wanafuata
swala tano
.
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
- Tovuti rasmi
- Habari
- Biashara
- Utalii
|
---|
Nchi huru
| |
---|
Nchi zisizokubaliwa
na umma wa kimataifa
| |
---|
Maeneo yanayojitawala
chini ya nchi nyingine
| |
---|
|
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Ulaya
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Uswidi
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|