Mongolia
(kwa
Kimongolia
:
Монгол Улс
,
mongol uls
) ni nchi ya
bara
la
Asia
.
Imepakana na nchi za
Urusi
na
Uchina
.
Ni nchi kubwa ya 19
duniani
lakini kuna wakazi wachache tuː jumla
milioni
2.6 hivyo
msongamano
wa watu ni mdogo sana.
Sehemu za
kusini mwa Mongolia
ya kihistoria ziko ndani ya
Jamhuri ya Watu wa China
.
Mongolia ni nchi ya
mbuga
yabisi
, ma
jangwa
na
milima
inayofikia
kimo
cha
mita
4,374
juu ya UB
(Nayramadlin Orgil).
Kaskazini mwa nchi kuna ardhi yenye hali ya
sakitu ya kudumu
yaani yenye
halijoto
chini ya 0 C° ndani yake isiyopoa hata wakati wa
majira ya joto
.
Kusini
kuna
jangwa kubwa la Gobi
.
Asilimia
10 pekee za nchi ina
misitu
hasa mlimani na ardhi inayolimika ni 1 % tu.
Hali ya hewa ni ya kibara na ina tofauti kubwa.
Majira
hubadilishana kuwa na
joto
pia
baridi
kali.
Wastani
wa siku ni kati ya ?25 °C na +20 °C. Hali halisi wakati wa joto
mchana
kuna joto kali lakini usiku huwa baridi.
Usimbishaji
una tofauti kubwa kati ya kaskazini na kusini mwa nchi. Kusini ni yabisi zaidi hadi kushuka kwa
mm
100 za mvua pekee kwa mwaka katika jangwa la
Gobi
.
Miji
mikubwa ni
mji mkuu
Ulaanbaatar
(Улаанбаатар) (takriban wakazi milioni moja - zaidi ya
theluthi
ya watu wote wa taifa), halafu
Erdenet
(wakazi 79,649),
Darchan
(72,386) na
Choibalsan
(44,367).
Miaka 800 iliyopita nchi hii ilikuwa chanzo cha moja kati ya
milki
kubwa kabisa katika
historia
wakati ambako
Chingis Khan
alipounda
Milki ya Wamongolia
iliyoenea kuanzia
China
hadi
Mashariki ya Kati
na
Ulaya
.
Hadi mwaka
1992
nchi iliitwa Jamhuri ya Watu wa Mongolia na kufuata sera za
ukomunisti
.
Wakazi ni hasa
Wakhalkhas
(82%),
Wakazaki
(4%) na wengineo.
Lugha rasmi
na ya kawaida ni
Kimongolia
.
Upande wa
dini
,
Wabuddha
ni 53%,
Waislamu
ni 3%, wafuasi wa
dini za jadi
ni 2.9%,
Wakristo
ni 2.2%, lakini 38.6% hawana dini yoyote.
Uchumi
wa Mongolia hutegemea hasa
migodi
na
ufugaji
. Kihistoria Wamongolia walikuwa wafugaji waliohamahama na
wanyama
wao na kuishi katika
hema
. Tangu
mapinduzi
ya mwaka
1921
sekta ya migodi na
viwanda
ilijengwa.
Sekta ya kisasa ya
biashara
iko hasa kwenye mji mkuu.
Hadi leo karibu
nusu
ya wakazi huishi nje ya miji wakifuatana na wanyama wao ambao ni hasa
kondoo
,
mbuzi
,
ng'ombe
,
farasi
na
ngamia
.
Kilimo
kipo mahali pachache kufuatana na tabia yabisi ya nchi. Wakati wa baridi sehemu kubwa ya wafugaji hukaa
vijijini
walipojenga
nyumba
.
Migodi ni hasa
makaa mawe
,
shaba
,
bai
na
dhahabu
.
- Serikali
- General information
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Asia
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Mongolia
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|