Korea ya Kusini
(jina rasmi: Jamhuri ya Korea) ni nchi ya
Asia ya Mashariki
iliyopo kusini mwa
rasi ya Korea
.
Upande wa
kaskazini
imepakana na
Korea ya Kaskazini
. Korea zote mbili zilikuwa nchi moja hadi mwaka
1945
chini ya utawala wa kikoloni wa
Japani
.
Ng'ambo ya
bahari
iko
Uchina
upande wa
magharibi
na Japani upande wa
kusini
-
mashariki
.
Mji mkuu
, pia
mji
mkubwa, ni
Seoul
ambako karibu nusu ya wakazi wote huishi ama mjini ama katika
mazingira
yake. Seoul ni kati ya miji muhimu ya
biashara
na
uchumi
kimataifa.
Utamaduni
wa Korea ni kati ya zile za kale zaidi duniani.
Tangu maungano ya kitaifa ya Korea yote mwaka
668 KK
ilikuwa nchi moja hadi mwaka
1910
ilipofanywa
koloni
la Japani.
Uhuru baada ya mwaka 1945 ulifuatwa na mgawanyiko wa nchi na kuundwa kwa Korea Kusini.
Awali ilikuwa
nchi maskini
yenye uchumi wa
kilimo
, lakini iliendelea kuwa
nchi ya viwanda
iliyofaulu kusogea mbele na kujenga
demokrasia
imara.
Siku hizi imekuwa moja ya
nchi tajiri
ya Asiaː ina nafasi ya 13
duniani
kati ya mataifa matajiri. Iko kati ya nchi kumi duniani zinazouza
bidhaa
nyingi nje.
Hali ya maisha ni ya juu na
viwanda
vyake vinatengeneza bidhaa za kisasa kabisa kama
motokaa
,
meli
,
mashine
, vifaa vya
kompyuta
na nyinginezo.
Kuna mikoa tisa nchini Korea Kusini, zikiwemo:
Wakazi karibu wote (99 %) ni Wakorea asili. Wachina ni 1.8 %, lakini wengi wao wana asili ya Korea.
Idadi
ya watu inaelekea kupungua kutokana na
uzazi
kuwa wa nadra mno (watoto 9 kwa watu 1,000?).
Lugha rasmi
na ya kawaida ni
Kikorea
.
Kiasili watu wa Korea walifuata
dini ya jadi
iliyoheshimu mapepo mbalimbali na kutoa
sadaka
kama njia za kuyapatanisha.
Tangu
karne ya 4
Ubuddha
uliingia kutoka China ukawa
dini rasmi
.
Ukonfusio
ulifuata tangu
karne ya 13
.
Ukristo
ulingia pia kutoka China ukaanza kukua zaidi tangu
karne ya 19
.
Siku hizi takriban
nusu
ya Wakorea wa kusini wasema hawana dini. Sehemu kubwa wanakadiriwa kuwa wafuasi wa
Konfusio
lakini hawajiiti "wanadini".
Ukristo ni kundi kubwa la kidini ukiwa na 29
%
za Wakorea wa Kusini, wakiwemo
Waprotestanti
(18.3 %) na
Wakatoliki
(10.9 %). Wabuddha ni kama 22.8 %. Kuna pia wafuasi wachache wa
dini
nyingine mbalimbali.