Myanmar
(pia: Myama; Myamari)
ni nchi ya
Asia ya Kusini-Mashariki
inayojulikana pia kwa jina la
Burma
au
Bama
.
Imepakana na
China
upande wa
kaskazini
,
Laos
upande wa
mashariki
,
Uthai
kusini
-mashariki,
Bangladesh
na
Uhindi
magharibi
.
Kuna pwani kwenye
Bahari Hindi
yenye urefu wa
km
2,000.
Kaskazini mwa nchi kuna
milima
mingi.
Safu
tatu za
Rakhine Yoma
,
Bago Yoma
na
Nyanda za Juu za Shan
zimeanza katika
Himalaya
na kuelekea kusini. Milima ya
Hengduan Shan
iko mpakani kwa China. Mlima mkubwa ni
Hkakabo Razi
kwenye jimbo la Kachin wenye
kimo
cha mita 5,881.
Mito
mitatu mikubwa ya Myanmar inavuka kati ya safu za milima; niː
Mto Ayeyarwady ni mto mkubwa wa Myanmar wenye urefu wa km 2,170.
Bonde
lake ni la
rutuba
na lina wakazi wengi.
Karibu
nusu
ya nchi imefunikwa na
misitu
.
Nafasi mwaka 2006
|
Mji
|
Sensa ya 1983
|
Kadirio kwa 2006
|
Dola / Mkoa
|
1.
|
Yangon
(Rangoon)
|
2,513,023
|
4,572,948
|
Mkoa wa Yangon
|
2.
|
Mandalay
|
532,949
|
1,237,028
|
Mkoa wa Mandalay
|
3.
|
Naypyidaw
(Nay Pyi Taw) *
|
0
|
924,608
|
Eneo la Kitaifa Naypyidaw
|
4.
|
Mawlamyaing
|
219,961
|
451,011
|
Dola la Mon
|
5.
|
Bago
|
150,528
|
248,899
|
Mkoa wa Bago
|
6.
|
Pathein
|
144,096
|
241,624
|
Mkoa wa Ayeyarwady
|
7.
|
Monywa
|
106,843
|
185,783
|
Mkoa wa Sagaing
|
8.
|
Meiktila
|
96,492
|
181,744
|
Mkoa wa Mandalay
|
9.
|
Sittwe
|
107,621
|
181,172
|
Dola la Rakhine
|
10.
|
Mergui
|
88,600
|
177,961
|
Mkoa wa Tanintharyi
|
11.
|
Taunggyi
|
108,231
|
162,396
|
Dola la Shan
|
Tangu
karne ya 9
BK
nchi iliona falme mbalimbali zilizotawala kutoka mji mkuu wa
Pagan
.
Katika
karne ya 19
Uingereza
ulianza kujishughulisha na habari za Burma (Myanmar) baada ya kutawala maeneo jirani ya Uhindi. Kwa
vita
tatu kati ya miaka
1826
na
1885
Uingereza ulieneza utawala wake.
Burma ilikuwa sehemu ya
Uhindi wa Kiingereza
tangu 1885.
Mwaka
1937
Waingereza walianza kutawala Burma kama
koloni
la pekee.
Wakati wa
Vita Kuu ya Pili ya Dunia
Japan
ilitwaa karibu nchi yote.
Baada ya vita Burma ikapata
uhuru
wake tarehe
4 Januari
1948
.
Serikali
iliyochaguliwa
kidemokrasia
ilipinduliwa na jeshi
mwaka
1962
.
Mtawala mpya hadi mwaka
1988
alikuwa
jenerali
Ne Win
aliyetangaza
siasa
ya "Ujamaa wa Kiburma".
Upinzani
ulikandamizwa vikali mara kadhaa.
Nchi iliona
harakati
kwa ajili ya demokrasia na dhidi ya
udikteta
mwaka 1988; hapo Ne Win alijiuzulu.
Baada ya
maandamano
yaliyokandamizwa mara kadhaa, Jenerali
Saw Maung
alichukua utawala kwa nguvu ya kijeshi.
Uchaguzi
huru wa mwaka
1989
ulileta
ushindi
wa
chama
cha NLD, chini ya
Aung San Suu Kyi
, lakini kamati ya kijeshi ilikataa kukabidhi
madaraka
.
Burma ilibadilishiwa jina kuitwa "Myanmar" ikaendelea kutawaliwa na
serikali ya kijeshi
hadi mwaka
2011
. Upinzani haukuruhusiwa.
Myanmar imegawiwa kwa kusudi la utawala katika ma
dola
7 na
mikoa
7. "Madola" ni maeneo yanayokaliwa na jumuiya na makabila ambayo ni tofauti na kundi kubwa la taifa linaloitwa
Bamar
. Maeneo ya Bamar huitwa mikoa.
Madola ya jumuiya ndogo yapo zaidi karibu na mipaka ya nchi. Kuanzia kusini-magharibi ni haya yafuatayo:
Halafu kuna mikoa 7:
Mazingira ya
mji mkuu
Naypyidaw
ni eneo la kitaifa la Naypyidaw.
Madola na mikoa imegawiwa katika
wilaya
,
tarafa
,
kata
na
vijiji
.
Myanmar ni nchi ya ma
kabila
mengi (135 yametambulika rasmi) na
lugha
nyingi (angalia
orodha ya lugha za Myanmar
). Kundi kubwa (68%) ni
Waburma
wenye asili katika milima ya
Tibet
walikotokea mababu wao miaka 1000 hivi iliyopita.
Lugha
kubwa ni
Kiburma
, ambacho ndicho
lugha rasmi
.
Wakazi walio wengi (80%) hufuata
dini
ya
Ubuddha
, hasa ya
madhehebu
ya
Theravada
.
Wakristo
ni 7%, wafuasi wa
dini za jadi
ni 6%,
Waislamu
ni 4%,
Wahindu
ni 2%.
- Taarifa za jumla
- Uchumi
- Kilimo
- Biashara
22°N
96°E
/
22°N 96°E
/
22; 96
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Asia
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Myanmar
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|