Mapambano kati ya Israeli na Palestina
ni
ugomvi
baina ya nchi ya
Israeli
na wakazi wa
Palestina
unaoathiri pia uhusiano na nchi jirani. Ugomvi huu ulianza katika
karne ya 20
baina ya wakazi
Wayahudi
na
Waarabu
wa maeneo ambayo leo hii yako chini ya Israeli na
Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina
. Ulisababisha tayari
vita
sita kati ya nchi ya
Israeli
tangu kuundwa kwake mwaka
1948
na jirani zake za
Kiarabu
. Mapambano yanaendelea, hayajapata
suluhisho
hadi sasa.
Mapambano yalianza wakati wa kuongezeka kwa
uhamiaji
wa Wayahudi katika maeneo ya
Palestina
yaliyokaliwa na Waarabu. Kuundwa kwa Dola la Israeli kulisababisha vita ya kwanza baina ya Israeli mypa na nchi zote za jirani. Hivyo ilikuwa pia chanzo cha
mgongano kati ya Israeli na nchi za Waarabu
kwa jumla.
Mapambano hayo si ya kijeshi tu, bali yanaanza upande wa
siasa
na pia upande wa
dini
.
Wayahudi wa
Ulaya
waliokuwa wahamiaji wa kwanza kuja Palestina waliona uhamiaji wao kama kurudi kwenye nchi ya ma
babu
wao kwenye mahali ambako
taifa
lao litazaliwa upya. Sehemu ya Wayahudi waliona mwendo wao si kurudi tu kwenye ardhi ya mababu kama taifa lakini pia
utimiaji
wa
sala
ya Kiyahudi yenye ombi la "kuonana katika
Yerusalemu
mwaka
ujao". Mpaka leo wengine wanaona jambo hilo kutokana na ahadi za
Mungu
kwa taifa lao kadiri ya
Tanakh
(yaani
Biblia ya Kiebrania
).
Kumbe wakazi Waarabu wa Palestina waliona uhamiaji wa wageni kutoka Ulaya kama
harakati
ya ki
koloni
iliyolenga kutwaa
ardhi
yao. Tena
Waislamu
kadhaa wanaona ya kwamba, tangu itwaliwe na
jeshi
la
Uislamu
katika
karne ya 7
ardhi ya Palestina - Israeli imekuwa nchi ya Kiislamu inayopaswa kutawaliwa na
serikali
ya Waislamu daima.
Wakristo
hawakuwa wengi, tena wamezidi kupungua kwa kuhama kutokana na ugumu wa hali yao wanaojisikia kubaguliwa kama kundi dogo hata kati ya Wapalestina.
Historia
Utangulizi: Pogromu, Uhamiaji na Uzayuni
Katika
karne ya 19
idadi kubwa ya Wayahudi waliishi katika maeneo kadhaa ya
Milki ya Urusi
[1]
yaliyotwaliwa na
milki
hiyo mnamo
1800
.
Uadui
dhidi ya Wayahudi ulitokea dhidi ya utawala wa Kirusi
[2]
Kuanzia mwaka
1880
kulitokea
ghasia
mbalimbali ambako Wayahudi walishambuliwa katika miji ya Urusi.
Wimbi
la pili la ghasia hizo zilizoitwa
pogromu
likatokea mwaka
1905
, ambapo Wayahudi zaidi ya 2000 waliuawa mjini
Odessa
[3]
. Wakati ule Wayahudi wa Urusi walianza kuhamia nje: wengi wao walikwenda
Marekani
, lakini wachache walielekea Palestina.
Mapogromu yalikuwa pia chanzo cha harakati mpya ya
Uzayuni
(
Zionism
) kati ya Wayahudi wa Ulaya. Uzayuni ulilenga kuwapa Wayahudi eneo maalum ili wapate kujenga upya taifa katika dola lao wenyewe, ambako wangekuwa
wenyeji
, si kundi la pekee katikati ya watu waliowadharau.
Mwaka
1896
Theodor Herzl
(
1860
-
1904
) aliandika kitabu "
Dola la Wayahudi
" alimodai kuundwa dola la pekee kwa ajili ya Wayahudi.
Mkutano
wa kwanza wa wafuasi wake ulichagua
jina
la "Zayuni" ambalo lilikuwa jina asilia la
mlima
wa
hekalu
mjini Yerusalemu; wakachagua jina hilo kwa sababu linataja mahali patakatifu zaidi pa
Uyahudi
. Mkutano huo uliazimia kuwa "Uzayuni unalenga kuunda
makazi
salama yaliyokubaliwa
rasmi
kwa ajili ya taifa la Kiyahudi katika nchi ya Palestina".
Wazayuni walikusanya
pesa
kote Ulaya wakanunua ardhi katika Palestina na kuanzisha vijiji kwa ajili ya Wayahudi waliohima huko.
Tamko la Balfour na chanzo cha mapambano
Vita ya Kwanza ya Dunia
ilikwamisha mipango yote kwa sababu Palestina ilikuwa sehemu ya
Milki ya Osmani
iliyoshiriki katika vita pamoja na
Ujerumani
na
Austria
dhidi ya Urusi,
Ufaransa
na
Uingereza
.
Mwaka
1917
wakati ambapo jeshi la Uingereza lilifaulu kusogea mbele kutoka
Misri
na kuingia Palestina,
waziri wa mambo ya nje
Arthur James Balfour
alitoa
tamko la Balfour
yaani
tamko
rasmi kuwa Uingereza inataka kusaidia mipango ya kuanzisha makazi ya Kiyahudi katika Palestina. Wakati uleule Waingereza waliwaahidi Waarabu kuundwa kwa dola la Kiarabu kwenye maeneo yaliyokaliwa nao katika Milki ya Osmani. Lakini wakati huohuo walipatana na Ufaransa kuhusu ugawaji wa maeneo ya Kiarabu ya Milki ya Osmani.
Kwenye
mkutano wa amani wa Paris
wa mwaka
1919
, ulioandaa
Mkataba wa Versailles
,
mwakilishi
wa Waarabu,
Faisal bin Hussein bin Ali al-Hashimi
, alipatana na mwakilishi wa
Wazayuni
,
Chaim Weizmann
, kuwa anakubali
uhamisho
wa Wayahudi kuja Palestina, na Palestina kuwa eneo la pekee tofauti na Dola la Waarabu ambayo Faisal alilenga kujenga
Uarabuni
pamoja na
Syria
na
Irak
.
Haki
za wakazi Waarabu zilitakiwa kulindwa na
maendeleo
ya pamoja kati ya wakazi Waarabu na Wayahudi kujengwa. Lakini Uingereza na Ufaransa waliendelea kugawa
Mashariki ya Kati
, hivyo Waarabu wengi hawakusikia ya kwamba mapatano ya Faisal yalikuwa na
umuhimu
tena.
Baada ya vita Uingereza ilichukua utawala wa Palestina kama
eneo la kudhaminiwa
kwa
niaba
ya
Shirikisho la Mataifa
. Idadi ya Wayahudi waliofika kutoka nchi za Ulaya iliongezeka, lakini bado Wayahudi wengi walihamia Marekani, si Palestina. Hata hivyo shirika za Uzayuni ziliendelea kununua ardhi, kuanzisha vijiji vya
Ujamaa
vilivyoitwa
Kibbutz
hata
Tel Aviv
ilikua kama mji wa Kiyahudi kandokando ya
Yafo
ya Kiarabu. Mnamo 1931 asilimia 17 ya wakazi wa Palestina walikuwa Wayahudi.
Katika Palestina
mufti
mkuu wa Yerusalemu,
Mohammed Amin al-Husseini
, alichukua
uongozi
wa Waarabu akapinga kufika kwa Wayahudi wapya. Serikali ya Kiingereza ilisitasita kuamua juu ya msimamo wake - haikuzuia kufika kwa Wayahudi, lakini haikuwasaidia kujiimarisha nchini.
Ma
shambulio
dhidi ya Wayahudi yalianza mwaka
1921
. Mwaka
1929
Wayahudi 67 waliuawa mjini
Hebron
.
Kati ya
1936
na
1939
kulitokea ghasia kubwa ya Waarabu dhidi ya
polisi
na jeshi la Kiingereza na dhidi ya makazi ya Wayahudi. Uingereza ulifaulu kukandamiza ghasia hii kwa jeshi lake. Kati ya Wayahudi vikundi vyenye
silaha
vilianzishwa vilivyolenga kutetea vijiji vya Kiyahudi na kulipiza
kisasi
kwa mashambulio. Vikundi hivyo viliendelea baadaye kuwa
chanzo
cha
jeshi la Israeli
.
Siasa ya chuki dhidi ya Wayahudi iliyoendeshwa na
Chama cha Nazi
chini ya
dikteta
Adolf Hitler
katika Ujerumani na nchi nyingine za Ulaya iliongeza namba ya Wayahudi waliopaswa kuondoka kwao Ulaya. Miaka baada ya
1933
takriban
wakimbizi
Wayahudi 250,000 walifika Palestina - hii ilikuwa
sababu
moja ya ghasia ya Waarabu miaka
1936
-
1939
. Hadi mwaka
1945
Wayahudi walikuwa asilimia 33 ya wakazi wote wa Palestina.
Baada ya
vita kuu ya pili
kulikuwa na
laki
za Wayahudi waliowekwa huru kutoka
makambi ya KZ
na wengi wao walielekea Palestina. Hapo Serikali ya Uingereza, iliyosita kuamua kama ilitaka kutekeleza
ahadi
zake kwa Waarabu au kwa Wayahudi, iliomba
Umoja wa Mataifa
kuamua juu ya
hatua
zijazo kwa ajili ya Palestina, maana ilikuwa eneo la kudhaminiwa na
asili
ya mamlaka hii ilikuwa imepita kutoka Shirikisho la Mataifa kwenda
Umoja wa Mataifa
.
[4]
.
Kuundwa kwa Dola la Israeli
Mwaka
1947
Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa
ulipigia
kura
mpango
wa
ugawaji
wa Palestina. Mataifa 33 yalipiga kura ya
ndiyo
, 13
hapana
, 10 hayakusimama upande wowote. Hivyo eneo la Palestina lilitakiwa kugawiwa kwa dola la Kiyahudi, dola la Kiarabu na mji wa Yerusalemu. Mamlaka ya Uingereza yalitakiwa kwisha tarehe
14 Mei
1948
.
Waarabu walipinga ugawaji kwa kudokeza ya kwamba mpango wa ugawaji haukuwa
adili
kwa sababu zifuatazo. Mwaka 1947 Palestina ilikuwa na wakazi 1,845,000. Watu 1,237,000 au
theluthi
mbili walikuwa Waarabu, wakati watu 608,000 tu au theluthi moja walikuwa Wayahudi. Kumbe Dola la Kiyahudi lilitakiwa kupokea
asilimia
56 cha ardhi, pamoja na maeneo yaliyofaa zaidi kwa
kilimo
ingawa
mali
ya Kiyahudi wakati ule ilikuwa asilimia 7 tu ya ardhi yote ya Palestina. Katika eneo la Dola la Kiyahudi takriban 40% ya wakazi wangekuwa Waarabu. Sehemu kubwa ya ardhi katika sehemu ya Dola la Kiarabu ilikuwa mlimani na haikufaa vema kwa ajili ya kilimo.
Wawakilishi wa Kiyahudi walisema idadi ya Wayahudi itaongezeka
haraka
kutokana na uhamiaji wa Wayahudi wengine - wakati ule walikuwa bado laki za Wayahudi katika makambi katika nchi za Ulaya, ni hao ambao hawakuuawa na Wajerumani katika
Holocaust
.
Mara baada ya azimio la UM, mapigano yalianza katika Palestina na kuwa
vita ya wenyewe kwa wenyewe
nchini. Vikundi vya
wanamgambo
wa Kiarabu vilishambulia makazi ya Kiyahudi kote nchini. Wayahudi pia walikuwa na vikundi vya wanamgambo.
Tarehe
14 Mei
mkutano wa wawakilishi Wayahudi ulitangaza Dola la Israeli kama nchi mpya. Waingereza waliondoa jeshi lao.
Tarehe
15 Mei
1948 majeshi ya Misri,
Yordani
,
Lebanoni
, Syria na Irak yaliingia Palestina yakatwaa maeneo ya Kiarabu na kushambulia makazi ya Kiyahudi. Katika vita ya miezi 10 jeshi la Israeli lilifaulu kusimamisha wapinzani na kuwarudisha nyuma. Jeshi la Kiarabu pekee lenye
uwezo
lilikuwa Kikosi Arabu cha Yordani. Wakati wa kusimamisha mapigano Israeli ilikuwa imeongezeka maeneo yake ikatawala asilimia 78 za eneo la kukabidhiwa la awali yaani maeneo yote yaliyowahi kukusudiwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Dola la Kiyahudi pamoja na nusu ya maeneo yaliyokusudiwa kwa ajili ya Dola la Kiarabu.
Ukanda wa Gaza
ulitawaliwa na Misri na
Ukingo wa Magharibi
wa
Yordani (mto)
pamoja na mji wa kale wa Yerusalemu ukawa chini ya milki ya Yordani.
Zaidi ya wakazi Waarabu 700.000 walilazimika kuondoka au walimkimbia kutoka miji na vijiji vyao, wakikaa nje ya maeneo yaliyotawaliwa sasa na Israeli. Waarabu 150,000 hivi walibaki ndani ya maeneo haya sasa kama
raia
Waarabu wa Israeli. Baada ya vita Israeli ilikataa kurudi kwa waliokuwa nje. Ndiyo asili ya Wakimbizi Wapalestina wanaoishi Syria, Lebanoni, Yordani na Misri, pamoja na hao wanaoendelea kukaa katika ma
kambi
katika maeneo ya Gaza na Ukingo wa Magharibi.
Madola yote ya Waarabu isipokuwa milki ya Yordani yalikataa kuwapa wakimbizi hao haki za
uraia
, na kwa hiyo hadi leo wajukuu wamebaki kama wakimbizi katika nchi za kigeni bila uraia; wakisafiri wanatumia vitambulisho vilivyotolewa na
UM
, wanakosa haki ya kutafuta kazi au kushiriki katika siasa kama raia wa kawaida, hata kama
familia
zimeshaishi katika nchi hizo hadi
kizazi
cha tatu au nne.
Wapalestina baada ya 1948
Jumuiya ya Nchi za Kiarabu
ilianzisha
taasisi
iliyoitwa "Serikali kwa Palestina yote" (
ing.
All-Palestine Government,
ar.
????? ???? ??????
hukumat 'umum Filastin
) wakati wa vita (1948) iliyotambuliwa na nchi za Kiarabu isipokuwa milki ya Yordani. Ilikuwa na
mamlaka
fulani katika Ukanda wa Gaza pekee, ikafanya kazi chini ya
usimamizi
wa Misri na mwisho wa 1948 ilipelekwa
Kairo
ikafutwa na serikali ya Misri mwaka
1959
.
Taasisi mpya ikaundwa mwaka
1964
kwa
azimio
la Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ikaitwa PLO (Palestine Liberation Organization,
ar.
: ????? ??????? ??????????? [[muna??amat at-ta?r?r al-filas??niyyah) ambayo ni maungano ya vikundi mbalimbali ya Kipalestina.
Shabaha
yake ilikuwa "ukombozi wa Palestina". Serikali ya Misri ilikuwa na
athira
kubwa katika PLO. Harakati ya
Fatah
mwanzoni haikushiriki. PLO iliendesha vikundi vya wanamgambo ya
Fedayin
Wapalestina walioshambulia mipaka ya Israel mara kwa mara.
Yordani na Israeli (kwa Wapalestina walioweza kubaki kwao) zilikuwa nchi pekee zilizowapa Wapalestina uraia, lakini katika nchi nyingine walibaki kama wakimbizi bila uraia. Makambi yao yaliangaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa linaloitwa
UNRWA
.
Israel na majirani hadi 1973
Baada ya vita ya 1948-1949 nchi jirani zilikataa kutambua dola la Israeli. Hali ya vita ikaendelea ingawa bila mapigano kati ya majeshi makubwa. Wanamgambo wa Wafedayin Wapalestina waliendelea kuvuka
mpaka
kutoka makambi ya wakimbizi na kushambulia vijiji vya Kiyahudi. Wanamgambo hao walipata mara nyingi silaha na mafunzo kutoka kwa majeshi ya Misri na Syria.
Vita ya 1948-1949 ilisababisha ghasia na mashambulio dhidi ya Wayahudi walioishi katika nchi za Kiarabu. Nchi kadhaa za Kiarabu ziliweka sheria za ubaguzi dhidi ya Wayahudi. Hivyo katika miaka baada ya kuundwa kwa Israeli karibu Wayahudi wote waliondoka au walifukuzwa katika nchi za Kiarabu na kufika kama wakimbizi katika Israel, Marekani au Ulaya. Jumla ya wakimbizi hao Wayahudi karibu ililingana na idadi ya Waarabu waliofukuzwa kutoka Palestina. Hivyo idadi ya wananchi Wayahudi wa Israeli iliongezeka sana.
Uhusiano
mbaya kati ya Israeli na majirani Waarabu ulisababisha vita zaidi.
Mwaka
1956
Israeli ilishambulia Misri katika
vita ya Suez
kufuatana na mpango wa pamoja na Ufaransa na Uingereza baada ya kuona
ununuzi
wa silaha nyingi na Misri.
Mwaka
1967
jeshi la Misri lilikusanya vikosi vingi vya jeshi lake katika
rasi ya Sinai
ikafukuza
walinzi wa amani wa UM
na kufunga
mlango wa Tiran
hivyo kuzuia
usafiri
wa
meli
baina ya Israeli na
Bahari Hindi
. Israeli ikajibu kwa kushambulia Misri tarehe
5 Juni
1967 katika
Sinai
ikaharibu jeshi la Misri katika
muda wa siku 6
. Wakati huohuo milki za Yordani na Syria ziliamua kushikamana na Misri zikashambulia eneo la Israeli. Tokeo lake lilikuwa ya kwamba jeshi la Israeli likatwaa
Ukingo wa Magharibi wa Yordani
na pia
milima ya Golan
hadi maadui walisalimisha amri tarehe
10 Juni
. Pia eneo lote la Sinai likatwaliwa na Israel na
Mfereji wa Suez
ulifungwa.
Vita ya Yom Kippur
iliyofuata ilikuwa mashambulio ya Misri na Syria dhidi ya Israeli katika mwezi wa Oktoba
1973
. Mashambulio yalianza kwenye
sikukuu
ya Kiyahudi ya
Yom Kippur
. Jeshi la Misri lilifaulu kuingia kwenye rasi ya Sinai na Syria kwenye milima ya Golan. Lakini Syria ilirudishwa nyuma haraka na Waisraeli walifikia
kilomita
40 tu kutoka
Dameski
. Jeshi la Misri lilifeli zaidi hadi Israeli iliweza kuvuka mfereji wa Suez na kufunga
kikosi
kikubwa cha Wamisri nyuma ya mstari wa mapigano na kuingia katika mji wa Suez na hata kukaribia
Kairo
. Mnamo
23 Oktoba
pande zote zilikubali kusimamisha mapigano kwa ombi la UM. Baada ya majadiliano marefu, kila upande ulirudisha wanajeshi wake kilomita kadhaa kwa kusudi la kuwa na
umbali
kati ya majeshi.
Misri na Israeli zikaendelea kuwa na majadiliano na kupatana kufanya
amani
mwaka 1978. Israeli iliondoka katika Sinai na nchi zote mbili zikafungua
ubalozi
katika nchi ya pili. Ukanda wa Gaza ulibaki chini ya Israeli.
Uamsho wa Wapalestina na PLO
Vita ya siku 6 ya 1967 ilileta
uamsho
kati ya Wapalestina katika makambi ya wakimbizi. Kundi la Fatah lililoundwa mwaka 1959 nchini
Kuwait
liliongeza sifa zake kutokana na kupigana na jeshi la Israeli mwaka
1968
katika kambi la Karame (Yordani). Fatah lilijiunga na PLO na
mwenyekiti
wake
Yasser Arafat
akawa mwenyekiti wa PLO. Alileta
mwelekeo
mpya kuwa Wapalestina wanapaswa kujikomboa badala ya kutegema nchi za Waarabu wengine. Vikundi vya PLO viliendelea na mashambulio pamoja na kutumia
mbinu za kigaidi
dhidi ya wananchi raia wa Israeli.
Tangu 1968 vikundi vya PLO viliteka
nyara
ndege
au watu raia kwa shabaha ya kuwabadilisha na wafungwa Wapalestina katika Israeli. Hadi mwaka
1970
PLO ilikua kuwa na mamlaka kubwa nchini Yordani hadi jeshi la nchi hiyo iliwafukuza vikosi vya PLO kutoka milki ya Yordani.
Hapo Arafat na sehemu ya askari wake walihamia Lebanoni. Wakati wa
vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Lebanoni
PLO ilichukua upande na kushiriki lakini sehemu nyingine za vikundi vya Kipalestina vilishikamana na serikali za nchi za Waarabu zilizoshiriki pia katika vita hiyo ndani ya Lebanoni. Baada ya mashambulio ya Israeli PLO ilifukuzwa kutoka Lebanoni na kuhamia
Tunisia
mwaka
1982
.
Intifada ya kwanza
Katika miaka iliyofuata Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Yordani walisikia maisha kuwa vigumu zaidi. Wengi wao walikuwa
vijana
waliozaliwa chini ya utawala wa Israeli. Vijana wengi walikosa
kazi
. Hawakuwa na matumaini katika jitihada za PLO iliyokuwa mbali nao.
Basi, baada ya
ajali
ya barabarani ambako Wapalestina wanne waliuawa na
gari la kijeshi
la Israeli, mnamo Disemba
1987
ililipuka ghasia ya
ghafla
iliyoitwa
intifada
. Wapalestina waliandamana barabarani,
watoto
na vijana walitupa mawe dhidi ya askari wa Israeli. Kundi jipya la
Hamas
lilichokoza mwendo huu na kuongoza upinzani. Katika miezi iliyofuata Wapalestina 1,551 na Waisraeli 422 waliuawa.
Kutangazwa kwa "Dola la Palestina" na majadiliano kati ya PLO na Israeli
Mwaka moja baada ya intifada ya kwanza PLO katika mji wa Tunis ilitoa tamko la kutangaza "Dola la Palestina". Katika tamko hili PLO ilitambua kwa mara ya kwanza kuwepo kwa Israeli. Tamko hili lilikuwa msingi kwa nchi kama Marekani kutambua pia PLO kama mwakilishi wa Wapalestina na baadaye kwa majadiliano ya kwanza kati ya PLO na Israeli.
Wakati wa
Vita ya Ghuba ya 1990/91
Arafat aliamua kuwa upande wa
Saddam Hussein
aliyeshambulia
Kuwait
. Hii ilisababisha kufukuzwa kwa Wapalestina wengi kutoka Kuwait baada ya vita na kushindwa kwa
Iraq
. Nchi za Kiarabu kama Misri na
Saudia
zilizowahi kusaidia PLO lakini zilichukua msimamo dhidi ya Saddam Hussein zilikata misaada yao kwa PLO. Kudhoofishwa kwa PLO kwa njia hii ilisaidia pia kuanzisha majadiliano ya moja kwa moja. Katika mkutano wa amani wa
Madrid
,
Hispania
, Wapalestina walishiriki kwa mara ya kwanza katika majadiliano na Israeli.
Mapatano ya Oslo na kuanzishwa kwa mamlaka ya kitaifa ya Palestina
Tangu Januari
1993
wawakilishi wa PLO na Israeli walikutana kwa
siri
mjini
Oslo
,
Norwei
. Arafat alitamka kutambua Israeli na kuachana na mbinu za kigaidi katika barua kwa kiongozi wa Israeli
Yitzhak Rabin
. Rabin na Arafat walikutana
Washington, D.C.
na kutia
sahihi
mapatano ya kwanza yaliyokuwa mwanzo wa mfuatano wa majadiliano marefu yaliyolenga kuleta amani kati ya Wapalestina na Israeli katika muda wa miaka 5.
Kwa jumla mapatano hayakuweza kufikia mwisho. Lakini katika hatua za kwanza
Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina
yaliundwa kama
mbegu
ya serikali kamili. Jeshi la Israeli ilijiondoa katika Gaza na sehemu za Ukingo wa Magharibi wa Yordani zilizowekwa chini ya mamlaka mpya.
Mwaka
1995
uongozi wa PLO ulihamia Palestina na kuanzisha
ofisi
kuu ya Mamlaka ya Palestina huko
Ramallah
.
Kukwama kulisababishwa na shaka kama ifuatavyo:
- katika jamii ya Israeli kama Arafat na upande wa Kipalestina walitaka kweli kujenga amani na kusimamisha
ugaidi
wakati mashambulio dhidi ya askari na wananchi raia wa Israeli yalipoendelea kutokea. Kilele cha upinzani ndani ya Israeli kilikuwa
uuaji
wa
waziri mkuu
Rabin mwaka 1995 uliofanywa na mpinzani Mwisraeli.
- Katika jamii ya Wapalestina kama Israeli ilitaka kweli amani kwa sababu kujengwa kwa makazi kwa
walowezi
Waisraeli nje ya mipaka ya Israeli ya 1967 kuliendelea.
- Sehemu ya vikundi vya kisiasa upande wa Palestina, hasa Hamas, ilikataa kukubali mapatano yaliyofikiwa.
- Swali la pekee lilihusu hali ya Yerusalemu ya
Mashariki
ambayo Wapalestina wanaidai kama mji mkuu wao ambayo iko nje ya mipaka ya Israeli ya 1967. Lakini Israeli iliwahi kutangaza kuunganishwa kwa mji huu wote na kuitawala sehemu ya magharibi na ya mashariki kama mji mmoja wa Israeli usioweza kutengwa tena.
- Tatizo ni pia suala la "haki ya kurudi" kwa ajili ya watoto na wajukuu wa wakimbizi Wapalestina wa mwaka 1948 wanaotaka kurudi kwenye makazi ya mababu yaliyo sasa ndani ya eneo la Israeli.
Katika uchaguzi wa mwaka
1996
chama cha
Benyamin Netanyahu
kilishinda kura ya bunge la Israeli. Netanyahu hakukubali majadiliano; alidai kuwa yaliimarisha tu wapinzani wakali wa Israeli upande wa Wapalestina na kusabisha mashambulio na ugaidi zaidi.
Mwaka
2005
jeshi la Israeli lilitoka kabisa katika Ukanda wa Gaza na kubomoa vijiji vya walowezi Wayahudi kule.
Mafarakano kati ya Wapalestina yaliendelea kuongezeka kati ya Fatah na Hamas. Mwaka
2007
Chama cha Hamas kilichukua mamlaka juu ya Gaza kikaendelea kushambulia Israeli kwa ma
kombora
. Israeli ilijibu kwa kufunga mipaka ya Gaza na kungilia ndani ya Ukanda wa Gaza kijeshi mara kadhaa.
Kutokana na mashambulio dhidi ya wananchi wa Israeli yaliyoendelea Waisraeli walianza kujenga
fensi
na
ukuta
wa kutenganisha Ufuko wa Magharibi na Israeli yenyewe. Ukuta huu wenye
urefu
hadi
mita
nane umesaidia kupunguza sana mashambulio dhidi ya raia, lakini umejengwa zaidi kwenye ardhi ya Kipalestina na kuongeza matatizo kwa wananchi.
Israeli inaendelea kujenga makazi na vijiji kwa walowezi wa Kiyahudi ndani ya eneo la Kipalestina. Jeshi lake linashika vituo vingi katika ufuko wa magharibi na kutawala mwendo wa watu huko na kuzuia usafiri mara kwa mara kwa kulinda usalama wake.
Farakano kati ya Hamas upande wa Gaza na Mamlaka ya Kipalestina mkononi mwa PLO-Fatah upande wa Ramallah haijapata suluhisho.
Tazama pia
Tanbihi
- ↑
katika nchi za kisasa za
Poland
,
Belarus
na
Ukraine
zilizokuwa chini ya
Tsar
wa
Urusi
wakati ule
- ↑
Maeneo penye Wayahudi wengi yalikuwa chini ya milki ya Poland hadi
kugawanyika kwa Polandi
kati ya majirani yake. Wayahudi waliowahi kuwa na
uhuru
fulani katika Poland walijikuta chini ya
utawala
wa Kirusi. Warusi ambao hawakuzoea Wayahudi wengi waliwabana
wananchi
wapya hao kwa
sheria za ubaguzi
.
- ↑
Ukraine ya leo
- ↑
Umoja wa Mataifa uliundwa wakati wa Vita Kuu ya Pili kama maungano ya mataifa yote yaliyopiga vita dhidi ya Ujerumani na
Japani
. Shirikisho la Mataifa lilijifuta yenyewe mwaka
1946
na kukabidhi
shughuli
zake zote kwa UM
Marejeo
- Associated Press
, comp. (1996).
Lightning Out of Israel: [The Six-Day War in the Middle East]: The Arab-Israeli Conflict
. Commemorative Ed. Western Printing and Lithographing Company for the Associated Press. ASIN B000BGT89M.
- Bard, Mitchell
(1999).
Middle East Conflict
. Indianapolis: Alpha Books.
ISBN 0-02-863261-3
.
- Barzilai, Gad
(1996).
Wars, Internal Conflicts and Political Order: A Jewish Democracy in the Middle East
. Albany: State University of New York Press.
ISBN 0-7914-2944-X
- Brown, Wesley H. & Peter F. Penner (ed.):
Christian Perspectives on the Israeli-Palestinian Conflict
. Neufeld Verlag, Schwarzenfeld 2008.
ISBN 978-3-937896-57-1
.
- Carter, Jimmy
(2006).
Palestine: Peace Not Apartheid
. New York:
Simon and Schuster
.
ISBN 0-7432-8502-6
.
- Casper, Lionel L. (2003).
Rape of Palestine and the Struggle for Jerusalem
. New York & Jerusalem: Gefen Publishing House.
ISBN 965-229-297-4
.
- Citron, Sabina
(2006).
The Indictment: The Arab-Israeli Conflict in Historical Perspective
. New York & Jerusalem: Gefen Publishing House.
ISBN 965-229-373-3
.
- Cramer, Richard Ben (2004).
How Israel Lost: The Four Questions
. New York:
Simon and Schuster
.
ISBN
0-7432-5028-1
.
- Dershowitz, Alan
(2004).
The Case for Israel
. New York: John Wiley & Sons.
ISBN 0-471-67952-6
.
- Falk, Avner
(2004).
Fratricide in the Holy Land: A Psychoanalytic View of the Arab-Israeli Conflict.
Madison: U of Wisconsin P.
ISBN 0-299-20250-X
- Gelvin
, James L. (2005).
The Israel-Palestine Conflict: 100 Years of War
. New York & Cambridge, Eng.: Cambridge UP.
ISBN
0-521-61804-5
.
- Gold, Dore
(2004).
Tower of Babble: How the United Nations Has Fueled Global Chaos
. New York: Crown Forum.
ISBN
1-4000-5475-3
.
- Finkelstein, Norman G.
(2003).
Image and Reality of the Israel-Palestine Conflict
. Verso Books.
ISBN 1-85984-442-1
.
- Goldenberg, Doron (2003).
State of Siege
. Gefen Publishing House.
ISBN 965-229-310-5
.
- Gopin, Marc
. (2002).
Holy War, Holy Peace: How Religion Can Bring Peace to the Middle East
. Oxford University Press.
ISBN 0-19-514650-6
.
- Hamidullah, Muhammad
(January 1986). "Relations of Muslims with non-Muslims".
Journal of Muslim Minority Affairs
7
(1): 9.
doi
:
10.1080/13602008608715960
.
- Howell, Mark (2007).
What Did We Do to Deserve This? Palestinian Life under Occupation in the West Bank
, Garnet Publishing.
ISBN 1-85964-195-4
- Israeli, Raphael
(2002).
Dangers of a Palestinian State
. New York & Jerusalem: Gefen Publishing House.
ISBN 965-229-303-2
.
- Katz, Shmuel
(1973).
Battleground: Fact and Fantasy in Palestine
. Shapolsky Pub.
ISBN 0-933503-03-2
.
- Khouri, Fred J. (1985).
The Arab-Israeli Dilemma
(toleo la 3rd). Syracuse, NY: Syracuse University Press.
ISBN
0-8156-2339-9
.
- Lewis, Bernard
(1984).
The Jews of Islam
. Princeton, NJ: Princeton UP.
ISBN
0-691-05419-3
.
- Lesch, David (2007).
The Arab-Israeli Conflict A History
. Oxford University Press, USA.
ISBN
0-19-517230-2
.
- ???. (September 1990). "The Roots of Muslim Rage."
The Atlantic Monthly
.
- Maoz, Zeev
(2006).
Defending the Holy Land
. Ann Arbor: University of Michigan.
ISBN 0-472-11540-5
- Morris, Benny
(1999).
Righteous Victims: A History of the Zionist-Arab Conflict, 1881?2001
. New York: Knopf.
ISBN
0-679-42120-3
.
- Morris, Benny (2009).
1948: A History of the First Arab-Israeli War
, Yale University Press.
ISBN 978-0-300-15112-1
- Reiter, Yitzhak
(2009).
National Minority, Regional Majority: Palestinian Arabs Versus Jews in Israel (Syracuse Studies on Peace and Conflict Resolution)
, Syracuse Univ Press (Sd).
ISBN 978-0-8156-3230-6
- Rogan, Eugene L., ed., and
Avi Shlaim
, ed. (2001).
The War for Palestine: Rewriting the History of 1948
. Cambridge: Cambridge UP.
ISBN 978-0-521-79476-3
.
- Segev, Tom
(1999).
One Palestine Complete: Jews and Arabs Under British Mandate
. New York: Henry Holt & Co.
ISBN 0-8050-6587-3
.
Viungo vya nje
Vyanzo rasmi
Vyanzo vya kieneo
- Israeli
- Arab
Uchunguzi wa kitaalamu
Mapendekezo ya amani
Ramani
Vyanzo vya jumla
- Crisis Guide: The Israeli-Palestinian Conflict from the Council on Foreign Relations
Archived
5 Juni 2010 at the
Wayback Machine
.
- The State of Israel
Archived
1 Agosti 2014 at the
Wayback Machine
. The Jewish History Resource Center, Project of the Dinur Center for Research in Jewish History, The Hebrew University of Jerusalem
- Daily digest of commentary about the Arab-Israeli conflict from around the world
- Israel and the Palestinians
Archived
26 Februari 2009 at the
Wayback Machine
.
- Encarta Encyclopedia on the Arab-Israeli Conflict
(
Archived
28 Oktoba 2009 at the
Wayback Machine
. 2009-10-31)
- Guide to the Arab-Israeli Conflict
Archived
11 Juni 2010 at the
Wayback Machine
., includes links to historical sources, as well as sources representing the Arab and Israeli sides of the conflict.
- The Guardian (UK) A Brief History of Arab-Israeli Conflict
(flash)
- Israel-Palestine Conflict
katika Open Directory Project
- Information (articles, reports, maps, books, links, ...) on the israeli palestinian conflict (middle east conflict)
- Holy Land, Unholy War
Archived
9 Januari 2007 at the
Wayback Machine
. Independent coverage of the Middle East conflicts by the news agency
Inter Press Service
- "A Brief History of the Arab-Israeli Conflict"
by Jeremy Pressman