Malta
ni nchi ndogo kwenye
funguvisiwa
katikati ya
bahari
ya
Mediteranea
.
Malta iko
km
93
kusini
kwa
kisiwa
cha
Sisilia
(
Italia
), upande wa
mashariki
kwa
Tunisia
na
kaskazini
kwa
Libya
.
Funguvisiwa la Malta lina
visiwa
saba. Visiwa vikubwa viwili ni Malta (
km²
246) na
Gozo
(km² 70). Kuna kisiwa cha tatu kinachokaliwa na watu, ndicho
Comino
(km² 3). Vingine ni vidogo, havina watu. Jumla la eneo ni km² 316.
Visiwa vya Malta ni mabaki ya kanda la nchi kavu lililokuwa linaunganisha
Afrika
na
Ulaya
na lililokatwa na kupanda kwa
usawa wa bahari
tangu
mwaka
11000 KK
hivi.
Sehemu za juu ni
vilima
vya
Dingli Cliffs
vyenye
kimo
cha
mita
245 juu ya
UB
.
Tatizo kubwa la Malta ni uhaba wa
maji baridi
. Siku hizi vituo vinne vya kuondoa
chumvi
kwenye
maji
ya bahari kwa njia ya
osmosi
vinatengeneza
maji ya kunywa
.
Maji machafu
husafishwa na
mvua
kukusanywa.
Miji mikubwa zaidi ni:
St. Paul's Bay
(29,097),
Birkirkara
(wakazi 21,676),
Qormi
(wakazi 18,230),
Mosta
(wakazi 17,789),
Zabbar
(wakazi 15,030),
Victoria
(wakazi 12,914) na
San Gwann
(wakazi 12,346).
Mji mkuu
,
Valletta
, una wakazi 7,173 tu.
Malta ilikaliwa na
watu
tangu
milenia ya 4 KK
. Kuna ma
gofu
ya
hekalu
la
mwaka
3200 KK
hivi.
Baadaye
funguvisiwa
lilitawaliwa na
Wafinisia
,
Karthago
na
Dola la Roma
.
Malta inatajwa katika
Biblia
kwa sababu
Mtume Paulo
aliponea huko baada ya kuzama kwa
merikebu
alimosafiri baharini kuelekea
Roma
(
Mdo
27:39 n.k.).
Waarabu
walivamia
visiwa
hivyo mwaka
870
na kuvitawala hadi
1091
.
Baadaye vilitawaliwa na
Wanormandi
wa
Italia Kusini
, halafu na
Wahispania
chini ya
mamlaka
ya
Dola Takatifu la Kiroma
la
Ujerumani
.
Tangu mwaka
1530
visiwa vilikabidhiwa na
Kaisari
kwa
askari
wa
Vita vya msalaba
wa
Chama cha Wanahospitali wa Mt. Yohane wa Yerusalemu
.
Wanamisalaba
hao walitawala visiwa hivyo hadi
Napoleoni
alipoteka Malta mwaka
1799
akiwa
safarini
kwenda
Misri
.
Uingereza
ulitwaa visiwa kutoka kwa
Ufaransa
ukatawala Malta hadi
uhuru
wake
tarehe
21 Septemba
1964
.
Tarehe
13 Desemba
1974
Malta ikatangazwa kuwa
jamhuri
ndani ya
Jumuiya ya Madola
.
Tarehe
1 Mei
2004
nchi ikajiunga na
Umoja wa Ulaya
.
Kwa jumla kuna wakazi 404,039: wa kiume 200,715 (49.7
%
) na wa kike 203,324 (50.3%).
Msongamano
wa watu ni 1,282 kwa
kilomita ya mraba
ambao ni msongamano mkubwa kati ya nchi zote za Ulaya. Katika
karne ya 21
nchi imepokwa wahamiaji wengi, ambao kwa sasa ni 23.17% za wakazi wote.
Lugha
ya
Kimalta
ni lugha ya pekee.
Asili
yake ni
lahaja
ya
Kiarabu
iliyopokea maneno mengi ya
Kiitalia
,
Kisisili
,
Kiingereza
,
Kihispania
na
Kifaransa
. Ni lugha pekee ya
Kisemiti
inayoandikwa rasmi kwa
alfabeti ya Kilatini
.
Lugha rasmi
ya pili ni
Kiingereza
kutokana na miaka 150 ya
ukoloni
wa
Uingereza
. Wamalta wengi sana (66%) huelewa pia lugha ya nchi kubwa jirani, Italia.
wakazi wengi (90%) ni
Wakristo
, hasa wa
Kanisa Katoliki
(83%), ambalo
imani
yake ndiyo
dini rasmi
ya nchi.
Waislamu
ni
asilimia
2.
- Serikali
- Taarifa za jumla
- Vyombo vya habari
- Safari
|
---|
Nchi huru
| |
---|
Nchi zisizokubaliwa
na umma wa kimataifa
| |
---|
Maeneo yanayojitawala
chini ya nchi nyingine
| |
---|
|
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Ulaya
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Malta
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|