Rene Descartes

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rene Descartes

Rene Descartes ( 31 Machi 1596 ? 1 Februari 1650 ) alikuwa mwanafalsafa , mwanahisabati na mwanafizikia mashuhuri katika Ufaransa .

Katika falsafa alijulikana kwa tamko lake "cogito ergo sum" ( Kilatini : Ninafikiri hivyo niko; au: Nina hakika ya kwamba niko kwa sababu najikuta nikitafakari).

Alieleza nadharia yake katika kitabu "Discours de la methode pour bien conduire sa raison et chercher la verite dans les sciences" ( tafsiri kamili: "Majadiliano juu ya mbinu jinsi gani kutumia akili vizuri na kutafuta ukweli katika sayansi") .

Katika hisabati akumbukwa kama mwanzilishaji wa mfumo majira .

Athira yake ilikuwa kubwa kwa karne nyingi hata pale ambako matokeo ya nadharia zake yalifutwa baadaye.