Jawaharlal Nehru
(
14 Novemba
1889
-
27 Mei
1964
) alikuwa
waziri mkuu
na
kiongozi
wa kwanza wa
Uhindi
ya kisasa. Alitawala miaka 17 tangu
uhuru
wa
mwaka
1947
hadi 1964.
Alizaliwa
mjini
Allahabad
(
jimbo
la
Uttar Pradesh
) katika
familia
ya
Brahmin
kutoka
Kashmir
.
Baba
yake,
wakili
Motilal Nehru, alikuwa kati ya viongozi wa kwanza wa
chama cha
Indian National Congress
.
Kijana
Jawaharlal alipewa
elimu
kufuatana na mtindo wa
magharibi
na
shule
ya
sekondari
alisoma
Uingereza
. Akaendelea kusoma
biolojia
kwenye
chuo kikuu cha Cambridge
halafu
sheria
huko
London
.
Baada ya kurudi Uhindi
alimwoa
Kamala Kaul aliyemzalia
mtoto
wake pekee,
Indira Priyadarshini
. Indira alimfuata baadaye kuwa waziri mkuu wa Uhindi na baada yake
mjukuu
wake Nehru,
Rajiv Gandhi
. Katika miaka ya mwisho ya
utawala
wa Kiingereza Nehru alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Edwina Mountbatten,
mke
wa mfalme mdogo
Louis Mountbatten
.
Baada ya kumaliza masomo yake huko London alikubaliwa kuwa wakili na mwaka
1917
alirudi Uhindi alipokuwa
karani
yake
Mahatma Gandhi
. Kwa njia hiyo Motilal Nehru na Gandhi walijuana na Ghandi alijiunga na chama cha Congress.
Mwaka
1922
alikamatwa mara ya kwanza na
serikali
ya kikoloni ya Kiingereza na katika miaka iliyofuata alirudi
gerezani
mara nyingi. Tangu mwaka
1929
alikuwa kiongozi wa Congress pamoja na Gandhi akawa
mwenyekiti
wake kuanzia mwaka
1930
.
Katika serikali ya muda iliyoandaa uhuru alihudumia kama
makamu wa rais
. Siku ya
15 Agosti
1947
ilipoleta uhuru, Nehru akawa waziri mkuu na kiongozi wa kisiasa wa Uhindi wote na muda huohuo waziri wa mambo ya nje. Nehru alishindwa kuzuia
ugawaji wa Uhindi
ulioleta nchi mbili za pekee za Uhindi na
Pakistan
.
Nehru alirudishwa mwaka
1952
katika
uchaguzi
huru wa kwanza wa nchi hiyo. Alirudishwa mara mbili, miaka
1957
na
1962
akafariki akiwa madarakani.
Nehru alijenga uhusiano mwema na
makoloni
mengi ya awali yaliyopata uhuru katika
miaka ya 1950
na
1960
. Katika
mazingira
ya
vita baridi
alianzisha harakati ya kutofungamana na
Marekani
wala
Umoja wa Kisovyeti
akakusanya
mataifa
mapya mengi katika
ushirikiano
huo.
Ndani ya Uhindi aliunda
uchumi
wenye
tabia
za kijamaa kwa sekta ya
viwanda
. Alimaliza mabaki ya utawala wa
kikabaila
wa
maraja
na utawala wa kikoloni katika maeneo madogo ya
Goa
na
Pondicherry
yaliyokuwa yamebaki chini ya
Ureno
na
Ufaransa
.
Mwishoni mwa utawala wake aliona
vita ya China na Uhindi
iliyomlazimisha kutumia
silaha
alizozichukia.
Wikimedia Commons ina media kuhusu: