Salome Joseph Mbatia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Salome Joseph Mbatia

Salome Joseph Mbatia ( 27 Disemba 1952 24 Oktoba 2007 ) alikuwa naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, nchini Tanzania .

Maisha ya Mwanzo [ hariri | hariri chanzo ]

Mbatia alipata elimu ya msingi katika shule ya St. Anna kuanzia mnamo mwaka 1959 mpaka 1966 .

Aliendelea na masomo ya sekondari katika shule ya St. Joseph mnamo mwaka 1967 hadi 1970 na baadaye kidato cha tano na sita katika shule ya Wasichana ya mjini Korogwe ( Tanga ) mwaka 1971 hadi 1972 . Alisomea shahada yake ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia mwaka 1973 hadi 1976 .

Kati ya mwaka 1982 hadi 1983 alisomea Shahada ya Uzamili kuhusu Menejimenti huko nchini Marekani na baadaye akasomea Diploma ya Uzamili katika Utawala na Menejimenti huko nchini Uholanzi , hiyo ilikuwa mwaka 1993 .

Shughuli za Kiserikali [ hariri | hariri chanzo ]

Aliteuliwa kuwa Naibu Waziri mnamo Januari ya mwaka 2006 katika Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji, kabla ya kupelekwa katika Wizara ya Maendeleo ya Wanawake, Watoto na Jinsia.

Kifo Chake [ hariri | hariri chanzo ]

Salome Mbatia na dereva wake walikufa baada ya gari walilokuwamo aina ya Nissan Patrol kugongana na gari lingine kubwa aina ya Fuso lililokuwa limebeba mbao eneo la Kibena , wilayani Njombe mkoani Iringa , Tanzania .

Tazama pia [ hariri | hariri chanzo ]

Viungo vya Nje [ hariri | hariri chanzo ]