Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Marudio
(
ing.
frequency
, alama yake ni
f
) ni kipimo kichachosema ni mara ngapi tukio linatokea tena na tena kila baada ya kipindi fulani.
Kwa mfano ukikaa kando la bwawa au bahari penye
mawimbi
unaweza kuhesabu ni mawimbi mangapi yanayopita kwako katika dakika moja. Namba hii ni marudio ya mawimbi haya.
Kipimo cha SI
kwa marudio ni
Hezi
(alama Hz).
Vitu vingi katika dunia hutokea kwa marudio maalumu. Kutambua marudio ya
mawimbi
ya
nuru
,
sauti
,
mawimbi ya sumakuumeme
na kadhalika kumekuwa msingi kwa sehemu kubwa ya teknolojia tunayotumia, kuanzia
redio
,
televisheni
hadi
simu
na
kompyuta
.
Kwa hiyo marudio ni kipimo muhimu sana katika sayansi na teknolojia ya kisasa.
Marudio yanaweza kutajwa kwa matukio yote ambayo yanatokea mara kwa mara kufuatana na mfumo maalumu.
- Marudio ya badiliko la mchana na usiku ni
- Moyo
wa binadamu ina mapigo 50-90 kila dakika hii inalingana na marudio ya 0.83?1.5 Hz).
- katika bendi au okestra wapiganaji wote wanahitaji kupanga ala zao kwa sauti ya marudio yaleyale, mara nyingi kwa 440 Hz.
- Sikio
la kibinadamu hutambua sauti zenye marudio baina ya 20 Hz na 20.000 Hz, ilhali kiwango cha juu hupungua kuluingana na kuzidi kwa umri wa msikiliziaji.
- Jicho
la kibinadamu huona nuru kati ya 400 THz na 750 THz (
terahezi
).
- Mawimbi ya sumakuumeme
(
ing.
electromagnetic waves)
hutumiwa kwa mawasiliano kwa redio au simu bila waya kuanzia 100 kHz na GHz kadhaa.
Wikamusi
ya Kiswahili ina dictionary definitions (word meanings):