Kijapani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kijapani (日本語 "nihon-go" au "nippon-go" ) ni lugha rasmi nchini Japani . Kinatumiwa na Wajapani karibu wote isipokuwa kundi dogo la Waainu wana lugha yao.

Idadi ya wasemaji [ hariri | hariri chanzo ]

Kwa jumla kuna wasemaji milioni 124, karibu wote wakiishi nchini Japan. Kutokana na uhamiaji kuna takriban wasemaji 420,000 nchini Marekani (zaidi ya nusu wako Hawaii ) na 380,000 huko Brazil .

Uainishaji [ hariri | hariri chanzo ]

Wataalamu hawakubaliani kuhusu historia ya lugha. Lugha ya karibu ya pekee ni lugha za visiwa vya Ryukyu .

Kijapani kinafanana kiasi na Kikorea na kwa kawaida nyingi kimepangwa katika jamii ya lugha za Kialtai . Lakini kuna tabia kadhaa katika Japani ya kale zisizolingana na Kialtai , hivyo majadiliano ya kitaalamu yaendelea.

Lugha imepokea maneno mengi kutoka Kichina .

Mwandiko [ hariri | hariri chanzo ]

Kuna namna tatu ya kuandika:

  • hiragana (ひらがな) ni mwandiko wa kawaida. Alama zake zinaonyesha silabi . Watoto wote wanaanza kujifunza kuandika na kusoma kwa hiragana.
Silabi "MU" kwa katakana
  • katakana (カタカナ) ni mwandiko wa silabi pia lakini inatumiwa wa njia maalumu. Kama neno linatakiwa kuangaliwa hasa inaoanyeshwa kwa kutumia alama za katakana (kama maandishi manene au ya kiitaliki). Vilevile hutumiwa kwa maneno yasiyo kawaida kama maneno ya kisayansi au maneno ya kigeni.
  • kanji (漢字) ni alama za asili ya kichina na kila alama ni neno zima si silabi tu. Kijapanai inatumia alama 2,000 za aina hii.

Inawezekana kuandika Kijapani kwa njia mbili:

a) kama Kiswahili cha kisasa kuanzia upande wa kushoto kwenda kulia

b) Kuanzia juu kwenda chini kwa kutumia nhuzo.

Mifano [ hariri | hariri chanzo ]

Inayofuata ni mifano ya maneno ya Kijapani:

  • こんにちは ( konnichiwa ) : Habari zako! (wakati wa mchana)
  • さようなら ( say?nara ) : kwa heri
  • はい ( hai ) : ndiyo
  • いいえ ( ?e ) : hapana
  • キリスト? ( Kirisuto-ky? ) : Ukristo
  • イスラム? ( Isuramu-ky? ), イスラ?ム?( Isur?mu-ky? ) : Uislamu
  • ?? ( Bu-kky? ) : Ubuddha
  • 神道 ( Shint? ) : Shinto
  • ヒンドゥ?? ( Hindw?-ky? ), ヒンズ?? ( Hinz?-ky? ) : Uhindu
  • 日本 ( Nihon au Nippon ), 日本? ( Nihon koku au Nippon koku ) : Ujapani , Japani
  • アメリカ(?米利加) ( Amerika ), 米? ( B?-koku ), アメリカ合衆? ( Amerika gassh?koku ) : Marekani , Muungano wa Madola ya Amerika
  • 中? ( Chuugoku ), 中華人民共和? ( Ch?ka jinmin ky?wakoku ) : Jamhuri ya Watu wa China
  • フランス(?蘭西) ( Furansu ), ?? ( Futsu-koku ), フランス共和? ( Furansu ky?wakoku ) : Jamhuri ya Kifaransa
  • イギリス(英吉利) ( Igirisu ), 英? (?-koku), グレ?トブリテンおよび北アイルランド連合王? ( Gur?to Buriten oyobi Kita Airurando reng? ?koku ) : Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini
  • ロシア(露西?) ( Roshia ), ロシヤ ( Roshiya ), ロシア連邦 ( Rosia renp? ) : Shirikisho la Urusi

Viungo vya nje [ hariri | hariri chanzo ]