Usultani wa Omani
(kwa
Kiarabu
:
????? ?????
Saltanat ?Um?n
) ni nchi ya
Bara Arabu
katika
Asia ya Magharibi
.
Imepakana na
Maungano ya Falme za Kiarabu
,
Saudia
na
Yemen
, halafu
Bahari Hindi
na
Ghuba ya Omani
.
Utawala
wa nchi hufuata muundo wa kifalme usiobanwa na masharti ya
katiba
.
Mji mkuu
ni
Maskat (Omani)
.
Omani imekaliwa na watu kwa zaidi ya miaka 100,000.
Omani ilikuwa kituo muhimu cha
biashara
kwenye Bahari Hindi na
Ghuba ya Uajemi
tangu
milenia
mbili
KK
.
Tangu kuja kwa
Uislamu
Omani ilikuwa ama chini ya
Uajemi
au chini ya
khalifa
wa
Baghdad
na baadaye
Dola la Seljuki
.
Kati ya miaka
1507
na
1650
mji
wa Maskat na
pwani
ya Omani vilitawaliwa na
Ureno
.
Ma
kabila
ya
bara
yaliunganika chini ya
maimamu
wa
madhehebu
ya Kiislamu ya
Waibadiya
na Imam
Nasir ibn Murshid
(†
1649
) alifaulu kupunguza eneo la Wareno. Mfuasi wake
Sultan ibn Saif
aliwafukuzwa kabisa Wareno na kushambulia vituo vyao kwenye pwani ya
Afrika ya Mashariki
.
Masultani wa Omani walitawala pwani ya
Afrika ya Mashariki
katika
karne ya 19
.
Mwaka
1830
Sultani
Sayyid Said
alihamisha mji mkuu wake kutoka Omani kuja
mji wa Zanzibar
(
Unguja
). Baada ya
kifo
chake mwaka
1856
dola
liligawiwa kuwa nchi mbili:
Tangu mwaka 1891 sultani alikuwa kabisa chini ya mamlaka ya mwakilishi Mwingereza hata kama kwa jina nchi haikuwa koloni. Kati ya makabila ya Omani bara ulikua upinzani dhidi ya utawala wa Sultani mjini Maskat na athira kubwa ya Uingereza katika serikali yake. Hali halisi kanda ya pwani ilikuwa chini ya sultani wa Maskat lakini katika sehemu za ndani, yaani Oman yenyewe, makabila yalijitawala au kuungana kumchagua imamu kama mkuu wao wa pamoja. Kwenye mwezi wa Mei mwaka 1913 viongozi wa makabila ya ndani pamoja na vongozi wa dini walikutana wakamchagua tena imamu.
Baada ya vita ya miaka 7 pande mbili zilipatana mwaka 1920 kugawa nchi: upande wa imamu ulikubali kutoshambulia tena miji ya vijiji vya pwani, sultani alikubali kuheshimu hali ya kujitawala ya maeneo ya ndani chini ya imamu
[1]
. Sehemu za ndani ziliendelea kujitawala chini ya imamu hadi mwaka 1954.
Maungano chini ya Sultani Taimur
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Amani ilivunjwa mwaka 1954 wakati Sultani Said bin Taimur alitoa kibali kwa kampuni ya Kiingereza kutafuta mafuta ya petroli katika maeneo ya imamu. Kuingia kwa kikosi cha sultani kilichoongozwa na maafisa Waingereza kulikuwa chanzo cha vita iliyoendelea kwa miaka 5 hadi ushindi wa upande wa sultani aliyepata usaidizi wa jeshi la Uingereza. Hivyo Maskat na Omani iliunganishwa kwa nguvu ya kijeshi.
Sultani
Said bin Taimur
alipeleka mji mkuu wake kwenda
Salalah
akaendelea kutawala kutoka pale. Said bin Taimur alianza utawala wake akirithi madeni makubwa akalenga kumaliza deni na kutoingia madeni mapya. Hivyo alikataa
uwekezaji
katika
miundombinu
kama vile ba
rabara
au taasisi za
elimu
na
afya
. Hadi mwaka 1970 Omani ilikuwa na kilomita tu 10 za barabara za lami, hospitali 1 pekee na shule 3. Matumizi ya
baisikeli
na
miwani
ya Jua yalikatazwa na hapakuwa na
simu
kwa
raia
binafsi. Mageti ya miji iliyozungukwa bado na kuta zilifungwa wakati wa
machweo
. Wakati wa
usiku
kila raia alitakiwa kutembea akishika
koroboi
. Sultani mwenyewe aliangalia maombi yote ya
viza
kwa wageni waliotaka kuingia nchini, na vilevile vibali kwa wananchi waliotaka kutoka nje ya nchi.
Kuanzia mwaka
1965
kulitokea uasi katika jimbo la Dhofar uliopanuka kati ya makabila ya
milimani
ukiongozwa na
wanamapinduzi
Wakomunisti
kutoka nchi jirani ya
Yemen Kusini
. Jeshi la sultani lililoongozwa na maafisa Waingereza lilipambana na uasi huu na Waingereza walielewa kwamba sultani Taimur hakuwa na siasa ya kukomesha uasi. Hapo waliandaa mapinduzi ya kijeshi baada ya kuwasiliana na
Qaboos bin Said al Said
mwana pekee wa Taimur aliyewahi kusoma Uingereza lakini baada ya kurudi aliwekwa na baba yake chini ya ulinzi ndani ya
kasri
ya kifalme. Tarehe 23 Julai 1970 wanajeshi chini ya Waingereza walimkamata sultani Taimur aliyepelekwa mara moja uhamishoni Uingereza, Qabus alitangazwa kuwa sultani mpya.
Tangu 1970 hadi 2019 Omani ilitawaliwa na sultani Qabus aliyeanzisha mara moja mabadiliko mengi ya kuifanya kuwa nchi ya kisasa.
Utumwa
ulifutwa na mapato ya serikali, pamoja na
hazina
ya sultani, vilitumiwa kuwekeza katika miundombinu,
ujenzi
wa barabara, shule na hospitali. Vijana walitumwa ng'ambo ili wasome elimu ya kisasa.
Tangu
miaka ya 1980
, uwekezaji umelenga zaidi upande wa kuanzisha
viwanda
na kuanzisha kilimo cha kisasa ilhali nchi iliendelea kutegemea mapato ya uuzaji wa mafuta. Katika miaka 50 ya utawala wake nchi ilisogea mbele na mapato ya wananchi yaliongezeka mara 50.
Wakazi wengi ni
Waarabu
,
Wabaluchi
,
Wahindi
,
Waafrika
n.k. Zaidi ya
asilimia
40 ni
wahamiaji
.
Wenyeji karibu wote ni
Waislamu
, wakati wageni ni wa
dini
tofautitofauti. Kwa jumla Waislamu ni 85.9%,
Wakristo
6.5%,
Mabanyani
5.5% n.k.
Lugha rasmi
na ya kawaida ni
Kiarabu
, lakini
Kiingereza
,
Kibaluchi
,
Kiurdu
na
Kiswahili
pia vinatumika sana.
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Asia
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Omani
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|