Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Moscow
(
Kirusi
:
Москва - Moskva
) ni
mji mkuu
wa
Urusi
. Ina wakazi
milioni
10.5 na hivyo ni
mji
mkubwa wa
Ulaya
.
Iko katika sehemu ya kiulaya ya Urusi kwa 55°75'N na 37°62'E. Eneo lake ni kwa kimo cha 156 m juu ya
UB
. Mazingira ni ya vilima vidogo kando la
mto Moskva
unaobeba maji yake kwa mto Okra unaoishia katika
Volga
.
Mji ulianzishwa mwaka mnamo
1147
. Kuanzia 1326 ilikuwa kitovu cha utemi wa kujitegemea. Watemi wa Moscow waliendelea kuwa watawala wa maeneo makubwa zaidi hadi kusimamia Urusi wote.
Iwan III.
alimwoa binti kutoka familia ya ma
kaisari
wa
Bizanti
na baada ya Bizanti kutwaliwa na
Waturuki
Moscow ilijaribu kuchukua nafasi yake kama mji mkuu wa
Ukristo wa Kiorthodoksi
("Roma ya Tatu").
Mwaka
1703
mji mkuu wa Urusi ulihamishwa kwenda
Sankt Petersburg
. Baada ya mapinduzi ya kikomunisti mwaka
1918
serikali ikarudi Moscow iliyokuwa tena mji mkuu na kubaki hivyo.
Jengo kuu la Moscow ni boma la
Kremlin
(Кремль) lenye makanisa na majengo mengine mazuri pamoja na makumbusho muhimu. Nje ya
Kremlin uko
uwanja mwekundu
ambao ni uwanja mkubwa mjini unaotumiwa kwa ajili ya maandamano na paredi.
Makumbusho ya Moscow yanasifiwa kote duniani. Pia nyumba zake za maigizo na taasisi za sanaa zinajulikana kimataifa.
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Urusi
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Moscow
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|
|
---|
Wakazi zaidi ya 1.000.000
| |
---|
Wakazi 500.000-1.000.000
| |
---|
Wakazi 250.000-500.000
| |
---|
Miji mikuu mingine ya maeneo ya Shirikisho la Urusi
| |
---|
Makao makuu
ya maeneo ya shirikisho yanaonyeshwa na
herufi zilizokozwa
|