Kuwait
(kwa
Kiarabu
: ?????? ?) ni nchi ndogo ya
Uarabuni
kwenye
Ghuba ya Uajemi
.
Imepakana na
Irak
na
Saudia
.
Karibu nchi yote ni
jangwa
, lakini kuna
pwani
na
visiwa
vidogo.
Historia
ya Kuwait ilianza kama
utemi
mdogo chini ya
familia
ya Al-Sabah iliyokuwa chini ya
Sultani wa Uturuki
aliyetawala nchi jirani ya Irak hadi
vita kuu ya kwanza ya dunia
.
Tangu kuingia kwa
Waingereza
katika nchi za ghuba, mwaka
1899
watawala
wa Kuwait walijiweka chini ya
ulinzi
wa
Uingereza
kwa sababu waliuona afadhali kuliko ukuu wa Uturuki.
Waingereza walitetea hali yake ya pekee dhidi ya
Waosmani
na baadaye dhidi ya Saudia.
Baada ya kuporomoka wa
dola la Uturuki
Kuwait iliendelea kama
nchi lindwa
chini ya Uingereza hadi kupata
uhuru
wake tarehe
19 Juni
1961
.
Katika miaka iliyofuata Kuwait iliona madai ya
Irak
ya kuwa tangu zamani Kuwait ni
mkoa
wake uliotengwa na
ukoloni
.
Tarehe
2 Agosti
1990
dikteta
wa
Irak
Saddam Hussein
alivamia Kuwait na kuiteka. Katika
vita ya pili ya ghuba
Marekani pamoja na nchi nyingine ilishambulia
jeshi
la Irak katika Kuwait na kurudisha serikali ya
Emir
al Sabah.
Kati ya wakazi 4,044,500
asilimia
30 pekee ni wananchi au Wakuwait wenyewe. Wengine wote ni watu waliokuja kufanya kazi na kuishi hapo. Pamoja na wahamiaji kutoka nchi jirani, 60% ya wakazi ni
Waarabu
. Zaidi ya 30% tena wana asili ya
India
au nchi nyingine za
Asia
.
Waafrika
ni 76,698.
Lugha rasmi
ni Kiarabu; wananchi wanakiongea kwa
lahaja
maalumu. Kiingereza pia kinatumika hasa, hasa katika
biashara
.
Upande wa
dini
, wananchi karibu wote ni
Waislamu
, hasa
Wasuni
(70%), lakini pia
Washia
(30%). Ndiyo
dini rasmi
.
Wakristo
ni zaidi ya 10%, lakini karibu wote ni wahamiaji.
Wahindu
kutoka India ni wengi zaidi kidogo (karibu 15%).
Wabuddha
ni 2%.
Nchi ni
tajiri
kutokana na wingi wa
mafuta ya petroli
yaliyopo chini ya ardhi yake. Akiba zake ni kama 10% za akiba za
dunia
yote. Kabla ya kupatikana kwa mafuta mwaka
1938
nchi ilikuwa
maskini
lakini sasa ni kati ya
nchi tajiri
zaidi duniani.
Kabla ya kugunduliwa kwa mafuta palikuwa na
kilimo
kidogo sana, halafu
ufugaji
na hasa
uvuvi
baharini
.
- Abu-Hakima, Ahmad Mustafa, mhariri (1983). [[[:Kigezo:Google books]]
The Modern History of Kuwait: 1750-1965
]. London: Luzac & Company.
ISBN
9780718902599
.
- Abu-Hakima, Ahmad Mustafa, mhariri (1965). [[[:Kigezo:Google books]]
History of Eastern Arabia, 1750-1800: The rise and development of Bahrain and Kuwait
]. Bahrain: Khayats.
- Tetreault, Mary Ann, mhariri (2000). [[[:Kigezo:Google books]]
Stories of Democracy: Politics and Society in Contemporary Kuwait
]. New York: Columbia University Press.
ISBN
0231114885
.
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Asia
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Kuwait
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|