Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Vladimir Vladimirovich Putin
, (kwa
Kirusi
Владимир Владимирович Путин; alizaliwa
7 Oktoba
1952
) ni
mwanasiasa
wa nchini
Urusi
. Mara nne alichaguliwa kuwa
Rais
wa
Shirikisho la Urusi
, mara ya mwisho kwenye mwaka
2018
; awamu za kwanza zilikuwa kutoka
2000
hadi
2008
. Kuanzia
Agosti
1999
hadi
Mei
2000, tena kuanzia 2008 hadi 2012 alikuwa
waziri mkuu
wa Urusi. Baadaye aligombea tena uraisi aliporudishwa mwaka 2018.
Alikaimu
kiti
cha Urais tarehe
31 Desemba
1999
, pale rais
Boris Yeltsin
alipojiuzulu kwa ghafla. Kisha Putin akashinda
uchaguzi
wa rais mnamo mwaka wa 2000. Mnamo mwaka wa
2004
, alichaguliwa upya na kushinda, hivyo aliendelea na kipindi chake cha pili hadi tarehe
7 Mei
2008
.
Putin ni Mrusi wa
Kanisa la Kiorthodoksi
;
mama
yake alikuwa
Mkristo
wa kujitolea aliyekuwa akihudhuria katika
kanisa
wakati
baba
yake hakuamini
Mungu
. Mama yake hakuweka usaidizi wowote nyumbani lakini alihudhuria kanisani mara kwa mara japokuwa
serikali
ilinyanyasa
dini
yake kwa wakati huo. Mama yake
alimbatiza
kwa
siri
akiwa mdogo na mara kwa mara alimpeleka kuabudu.
Katika
michezo
Putin ameonekana mara kwa mara akiendeleza tasnia ya michezo kama vile kuendesha
baiskeli
, kutereza kwa
ski
,
badminton
.
|
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Vladimir Putin
kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|