Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lugha za ishara
(pia
lugha za alama
) ni
lugha
zinazohusisha miendo ya
mikono
,
uso
,
kichwa
,
mabega
na pia sehemu nzima ya juu ya
mwili
badala ya kuhusisha
sauti
. Lazima lugha za aina hiyo zionekane kwa sababu hazisikiki. Lugha hizo zinatumiwa hasa na watu
viziwi
, lakini vilevile wanaosikia wanaweza kujifunza hizo.
Lugha za
alama
ni lugha za asili na za kawaida zenye
cheo
cha
kiisimu
sawa na lugha za sauti. Hizo si mifumo tu ya kuleta msaada kwenye
mawasiliano
.
Duniani
kuna mamia mengi ya lugha za alama.
Idadi
sahihi haijulikani. Lugha hizo vilevile si nakala tu za lugha ya sauti inayozungumzwa kwenye eneo hilohilo. Kwa sababu ya mwanzo wake na
maendeleo
yake visivyotegemea lugha za sauti, zina
sarufi
zake zenyewe zinazotofautiana na zile za lugha nyingine (za sauti) zinazozungumzwa na walio wengi. Kwa mfano, katika
Kiitalia
(lugha ya sauti)
kitenzi
kikuu kipo kwa kawaida baada ya
kiima
na kabla ya
yambwa
. Katika Lugha ya Alama ya
Italia
, ambayo inazungumzwa nchini humohumo, kitenzi kikuu kipo kwa kawaida mwishoni mwa
sentensi
.
Vilevile lugha za alama zinaweza kutumia mielekeo na mahali pa
ishara
ili zifikishe
taarifa
muhimu kama vile kuhusu kiima na yambwa. Kwa mfano, katika lugha nyingi za ishara, alama inayomaanisha "kuuliza" inabadilika ikitegemea ni nani anayemuuliza nani: "ninakuuliza" inafikishwa kwa mwendo mmoja tu wa mbele kutoka mahali panapowakilisha "mimi" kuelekea panapowakilisha "wewe", ilhali alama inayomaanisha "unaniuliza" ina mwendo wa kinyume ulioelekea "mimi". Pia inawezekana kufikisha taarifa nyingine wakati huohuo, kama vile kwa ishara maalumu ya uso inayoweza kubadili ishara inayomaanisha "kuendesha gari" ikamaanishe "kuendesha gari
kwa purukushani
".
Zinazuka bila kupangwa wakati wowote watu wengi viziwi (hasa
watoto
) wanapokusanyika na kutumia muda mwingi wao kwa wao wakijaribujaribu kuwasiliana. Kwa kawaida, viziwi wasiojua lugha ya ishara (k.m. kwa sababu ya kukua kwenye
familia
ambapo wengine hawaijui) wamezoea kutumia ishara wanazozibuni ili wawasiliane na wengine. Ishara hizo zinazobuniwa zinajaribiwa kufahamika waziwazi kadiri iwezekanavyo. Viziwi hao wengi wanapokusanyika, baada ya muda wanaanza kutumia ishara zilezile. Hivi
msamiati
unajengwa. Kwa matumizi mengi inazuka pia sarufi. k.m. ambapo
shule
mpya ya viziwi inafunguliwa).
|
Makala hii kuhusu mambo ya
lugha
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Lugha ya ishara
kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|