Istanbul
(kwa
Kituruki
unatajwa
?stanbul
) ni
mji
mkubwa zaidi katika nchi ya
Uturuki
, ukiwa na wakazi wanaokadiriwa kuwa kati ya
milioni
11 na 15, ambao wanaufanya kuwa miongoni mwa miji mikubwa ya
dunia
. Huu ndio
mji mkuu
wa
Mkoa wa ?stanbul
.
Eneo la Istanbul linaelekea pande zote mbili za
mlangobahari
wa
Bosporus
unaotenganisha
Ulaya
na
Asia
. Hivyo ni mji pekee duniani uliopo katika
mabara
mawili.
Kiini cha
kihistoria
kipo upande wa Ulaya kwenye sehemu yenye
umbo
la
rasi
baina ya
Bahari ya Marmara
na
Pembe ya Dhahabu
ambayo ni mkono wa bahari unaoingia ndani ya nchi na hivyo mahali pa mji ulikingwa na
bahari
pande
tatu
.
Mji huu umebadilishiwa
jina
mara kadhaa katika historia yake ya zaidi ya miaka 2,600. Awali
jiji
hilo liliundwa na
Wagiriki
mnamo mwaka
660 KK
kwa jina la
Bizanti
. Mnamo mwaka
330
BK
Kaisari
Konstantino Mkuu
aliufanya kuwa mji mkuu wa
Dola la Roma
akaupanua ukajulikana kama
Konstantinopoli
(yaani mji wa Konstantino).
Konstantinopoli uliendelea kama mji mkuu wa
Dola la Roma
na baadaye
Roma ya Mashariki
uliojulikana pia kama
Milki ya Bizanti
hadi mwaka
1453
ambapo mji ulitwaliwa na
Waturuki
. Tangu mwaka ule uliendelea kama mji mkuu wa
Milki ya Osmani
hadi mwaka
1923
. Baadaye
serikali
ya Uturuki ilihamia
Ankara
.
Wakati wa
Waosmani
majina mbalimbali yalitumiwa: Konstantinopoli au kwa kifupi "Konstantiniye", halafu tangu
karne ya 18
pia "Istanbul". Tangu mwaka
1873
jina rasmi
kwa Kituruki limekuwa "Istanbul".
Kuwepo kwa
bandari
kumepelekea mji huo kuwa
kitovu
cha
biashara
katika
Uturuki
.
Katika
Ukristo
ni muhimu kama makao ya
Askofu
wa pili kwa
heshima
kati ya Maaskofu wote duniani, kadiri ya orodha iliyotolewa na
mitaguso mikuu
ya
karne ya 4
.
Hadi
vita vya kwanza vya dunia
Istanbul ilikuwa na wakazi wengi Wakristo, hasa
Wagiriki
na
Waarmenia
, lakini wakati ule Waarmenia waliteswa wakapungua na baada ya
vita
Wakristo walibaguliwa kwa jumla, hivyo wengi walihamia
Ugiriki
. Leo hii Wagiriki waliobaki ni 2000 - 3000 pekee na Waarmenia ni takriban 50,000.
Istanbul huwa na
majengo
mengi ya kihistoria kama vile
Mjini Istanbul kuna
vyuo vikuu
mbalimbali, kati yake:
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
|
---|
| |
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Uturuki
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Istanbul
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|