Gazeti
(kupitia
Kiingereza
kutoka
Kiitalia
gazzetta
) ni
karatasi
zilizochapishwa
habari
na kutolewa mara kwa mara ama kila
siku
au kila
wiki
; kuna pia magazeti yanayotolewa mara moja au mbili kwa
mwezi
tu.
Aina za habari
Mara nyingi gazeti huwa na habari za
siasa
,
uchumi
,
utamaduni
,
michezo
pamoja na
hali ya hewa
na programu za
TV
na
burudani
mbalimbali kama
vibonzo
,
hadithi
an
vitendawili
.
Sehemu nyingine muhimu ni matangazo ya
biashara
ambako
kampuni
au watu hununua nafasi gazetini na kutangaza biashara, mikutano na mengineyo.
Uhuru wa habari
Pamoja na
vyombo vingine vya habari
kama
TV
,
redio
au
blogu
, magazeti yanastahili
uhuru
wa maoni. Lakini katika nchi nyingi
serikali
zinajaribu kuzuia habari zisizopendezwa nazo. Kwa sababu hii
Tangazo kilimwengu la haki za binadamu
ya
Umoja wa Mataifa
linatetea uhuru wa magazeti.
Pia kwa nchi ya Tanzania na nyinginezo vyombo vya habari vinahitaji uhuru wa kusikilizwa kwa kuunda misingi iliyo kamili katika kutetea haki zao ndipo wataweza kusikilizwa zaidi.
Chombo cha habari ni muhimu sana kwa jamii zetu za Kiafrika kwa vyombo hivi pia ndipo elimu mbalimbali hutolewa kwao. Hata hivyo magazeti yamekuwa pia chanzo kikubwa sana cha vijana kuchafuana majina na kuzushiana taarifa zisizokuwa rasmi kwa jamii, hasa pale ambapo wanakoseana heshima na kudharauliana. Jambo hili ni baya sana kwa taifa na kwa jamii kwa ujumla, kwani kukosekana kwa maadili yaliyo muhimu kwa jamii ni chanzo kikubwa cha kuonekana kuwa magazeti hayana faida kwa kizazi cha baadaye, japo magazeti ni kitu muhimu sana kwa dunia ya leo, iwe ya mtandaoni au ya kuchapishwa kwenye karatasi.
Magazeti ya kuuzwa na magazeti ya bure
Magazeti huuzwa
madukani
au na wauzaji
barabarani
. Katika nchi nyingi kuna pia
mashine
zinazotoa gazeti baada ya kuingiza
sarafu
. Mengine huagizwa na wasomaji na kupelekwa kwao nyumbani, kwa mfano kwa njia ya
posta
.
Kuna pia magazeti yanayotolewa bure;
gharama
zao zinalipiwa na matangazo pekee.
Katika mazingira ya kisasa magazeti yanapatikana pia kwa njia ya
mtandao
yakionekana kwenye
tarakilishi
. Njia hii mara nyingi ni bure vilevile, ila kuna baadhi za magazeti yanayoweka sehemu ya makala tu mtandaoni kwa watu wote, lakini makala mengine yanaonekana kwa wasomaji waliowahi kulipa
ada
na kuwa na
neno la siri
linalowaruhusu kutazama kurasa zote.
Magazeti yenye nakala nyingi
Magazeti ya
Japani
huwa na wasomaji wengi kuna tatu za kila siku zinazotolewa kwa nakala kati ya
milioni
5 hadi 14 kila siku. Gazeti kubwa la
Ujerumani
"Bild" hutoa nakala milioni 3.8 kwa siku, gazeti kubwa la
Marekani
"America Today" milioni mbili. Gazeti kubwa la
Afrika ya Mashariki
ni
Daily Nation
wa
Kenya
yenye nakala 200,000 kila siku. Upande wa
Tanzania
ni gazeti "Mwananchi"
[1]
.
Magazeti ya kitaifa, kimataifa au kimahali
Nchi nyingi huwa na magazeti kadhaa yanayouzwa kote taifani. Kuna machache yanayoandaliwa kwa solo la kimataifa hasa, kwa mfano
International Herald Tribune
.
Lakini kuna pia magazeti mengi yanayokusanya habari za eneo au
mji
fulani hasa. Mifano yake katika Afrika ya Mashariki ni
Arusha Times
au
Coastweek
ya
Mombasa
. Katika nchi kama Marekani au Ujerumani sehemu kubwa ya magazeti ni ya eneo au miji fulani hasa.
Matumizi baada ya kusomwa
Magazeti huwa tena na matumizi baada ya kusomwa hasa kwa kufunga vitu
sokoni
au kurudishwa
kiwandani
kwa kutengeneza karatasi mpya.
Tanbihi
Viungo vya nje
- www.nationmedia.co.ke Nation Media Group, Nairobi Kenya