Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gallia
ni jina la kihistoria kwa ajili ya
Ufaransa
pamoja na maeneo ya jirani.
Gallia ilikuwa jina la
kilatini
kwa ajili maeneo yaliyokaliwa na "Wagallia". Hili ilikuwa namna jinsi
Waroma wa Kale
walivyowaita majirani wao
Wakelti
.
Kijiografia eneo hili lilijumlisha
Ufaransa
,
Uswisi
,
Ubelgiji
na
Italia
ya Kaskazini ya leo. Wakelti au Wagallia walikalia pia
Uingereza
ya Kusini (=
Britania
) na
Hispania
(=
Iberia
) lakini maeneo haya hayakuhesabiwa kuwa sehemu ya "Gallia" na Waroma. Wakelti walikuwa pia kati ya wakazi wa kale wa
Ujerumani
kabla ya uvamizi huko wa
Wagermanik
wenyewe.
Karibu habari zote za kimaandishi kuhusu Gallia na Wagalli zimetokana na Waroma wa kale. Sehemu kubwa ya habari zinapatikana katika kitabu cha
Caesar
"Vita ya Gallia".
Kuna pia mabaki ya
kiarkolojia
hasa makaburi pamoja na vitu vya maisha ya kila siku vilivyoweka makaburini kwa imani ya kwamba vitawasaidia marehemu katika ahera. Arkiolojia ya makaburi inaonyesha ya kwamba Wakelti (Wagallia) walikuwa sehemu ya biashara ya kimataifa pia walikuwa na mafundi wenye uwezo wa kutengeneza vitambaa na nguo, pia na wahunzi na wafinyanzi.
Mnamo mwaka 390
KK
kabila fulani la Wagallia chini ya kiongozi Brennus lilivamia Italia na mji wa Roma lakini walishindwa kuteka boma la mji. Kwa muda mrefu Waroma walihofia majirani ya kaskazini.
Kuanzia mwaka 200 KK Waroma walikuwa waliendelea kisiasa, kiuchumi na kijeshi wakafaulu kuteka "
Gallia Cisalpina
" (Gallia upande wa kusini wa milima ya Alpi) ambayo leo hii ni Italia ya Kaskazini. Ikawa jimbo la Kiroma.
Kuanzia mwaka 125 KK Waroma walianza kuvamia sehemu za pwani la Gallia pamoja na bonde la mto wa
Rhone
. Ikawa jimbo la
Gallia Narbonensis
. Mji mkuu ulikuwa mji wa Narbo (leo:
Narbonne
).
Sehemu nyingine ya Gallia imebaki nchi huru ya makabila yaliyojitawala. Mwaka 58 KK mwanasiasa na jenerali Mroma
Caesar
akawa gavana wa Gallia Cisalpina pia Narbonensis. Alichukua nafasi ya vita kati ya makabila ya Wagallia katika eneo la Uswisi kuingilia ndani ya mambo ya Gallia huru. Katika vita ya miaka nane alishinda wapinzani wote. Mwaka 51 KK Gallia yote ikawa chini ya utawala wa Kiroma.
Katika karne zilizofuata Gallia imekuwa sehemu halisi ya
Dola la Roma
. Inaonekana Wagallia wenyewe walikubali utawala wa Kiroma hasa baada ya kupewa
uraia wa Kiroma
. Lugha ya
Kilatini
ilitumika kwa ajili ya habari za kiutawala ikapokelewa polepole na wenyeji. Kilatini hiki kilikuwa msingi wa lugha ya
Kifaransa
kilichotokea baadaye.