Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
|
|
|
Mwanzo wa utawala wa kikoloni
|
1885
|
Makao ya serikali ya kikoloni
|
Bagamoyo
hadi 1891 halafu
Dar es Salaam
|
Eneo
|
km² 995,000
|
Wakazi
|
7,665,234 (1-1-1913)
|
Wakazi Wajerumani
|
4,100 (1913)
|
Pesa
|
1
Rupie
= 64 Pesa,
kuanzia 1904
1 Rupie = 100
Heller
|
Nchi huru za leo
|
1961
Tanganyika
, tangu 1964
Tanzania
Ruanda
Burundi
|
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
(au: ya
Kidachi
; kwa
Kijerumani
Deutsch-Ostafrika -DOA-
; kwa
Kiingereza
German East Africa
) ilikuwa
jina
la
koloni
la
Ujerumani
huko
Afrika ya Mashariki
kati ya miaka
1885
na
1918
/
1919
.
Eneo lake lilijumlisha nchi za kisasa za
Tanzania
bara (yaani bila
Zanzibar
),
Burundi
na
Rwanda
. Ilikuwa koloni kubwa kabisa la
Dola la Ujerumani
.
Eneo la koloni lilikuwa na
kilomita za mraba
997,000 pamoja na sehemu za
maziwa makubwa
kama
Ziwa Tanganyika
na
Ziwa Viktoria
. Eneo hili lilikuwa karibu mara
mbili
kuliko eneo la Ujerumani wenyewe kabla ya mwaka
1914
.
Mipaka iliamuliwa katika mapatano na
Uingereza
,
Ubelgiji
na
Ureno
zilizotawala makoloni ya jirani ya
Afrika ya Mashariki ya Kiingereza
(leo
Kenya
na
Uganda
),
Kongo ya Kibelgiji
(leo
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
),
Rhodesia
(leo
Zambia
na
Zimbabwe
),
Nyasaland
(leo
Malawi
) na
Msumbiji
. Mipaka hii ni pia mipaka ya Tanzania, Rwanda na Burundi hadi leo hii.
Katika mapatano baina ya Uingereza na Ujerumani ya Novemba 1886 pande zote mbili ziliahidi kuheshimu utawala wa Sultani wa Zanzibar juu ya visiwa pamoja na kanda la maili 10 kwenye pwani baina ya
mto Tana
na
Mto Minengani
(
Msumbiji
). Pamoja na hayo walielewana kuhusu maeneo ya maslahi yao, wakipatana kuhusu mstari uliokuwa baadaye mpaka baina ya Tanzania na Kenya hadi leo.
[1]
Katika
mkataba wa 1890 kuhusu mipaka katika Afrika
Uingereza iliahidi kumshawishi Sultani wa Zanzibar kuuza maeneo yake kwenye pwani la bara pamoja na
kisiwa cha Mafia
[2]
kwa Ujerumani
[3]
.
Upande wa Kenya mstari ulichorwa kuanzia
Bahari Hindi
kwa
mdomo
wa
mto Umba
hadi
Ziwa Jipe
, halafu kufuata mitelemko ya
kaskazini
ya
mlima Kilimanjaro
na kutoka hapa hadi
Ziwa Viktoria
. Mipaka na Uganda ilifuata
latitudo
ya kwanza ya kusini ya
ikweta
hadi mpaka na Kongo. Upande wa Kongo mpaka ulifuata sehemu za chini za
bonde la Ufa
na katikati ya
maziwa
kama
Kivu
na Tanganyika.
Upande wa kusini ulifuata mstari kati ya ncha ya kusini ya ziwa Tanganyika hadi mdomo wa
Mto Songwe
katika
Ziwa Nyasa
. Eneo lote la ziwa lenyewe lilibaki upande wa Nyasaland ya Kiingereza, halafu mstari kutoka Ziwa Nyasa kwa kufuata
mto Ruvuma
hadi
Rasi ya Delgado
kwenye Bahari Hindi.
Jinsi ilivyo na mipaka ya kikoloni mistari hii ilikata mara nyingi maeneo ya
makabila
ya wenyeji.
Mwaka
1913
takwimu
ya Wajerumani ilihesabu wakazi Waafrika 7,645,000, Waasia (
Wahindi
na
Waarabu
) 14,898 na
Wazungu
5,336, kati yao Wajerumani 4,107.
Nusu
ya wakazi wote waliishi katika eneo la
maziwa makubwa
ambako
serikali
ya kikoloni iliacha maeneo ya Rwanda (wakazi 2,000,000), Burundi (1,500,000) na
Bukoba
(275,000) kama
maeneo lindwa
chini ya watawala wa kienyeji waliosimamiwa na
afisa mkazi
Mjerumani.
[4]
Koloni hilo halikuanzishwa kwa azimio la kisiasa upande wa serikali ya Ujerumani bali lilianzishwa kama mradi wa watu binafsi waliotafuta makoloni katika Afrika.
Historia ya koloni ilikuwa na awamu tatu:
- mwanzo kama maeneo yaliyotawanyika ambako kampuni binafsi (
Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki
) ilifaulu kushawishi watawala wa kienyeji kutia sahihi kwenye mikataba; kipindi hiki kilianza
1885
hadi kuporomoka kwa utawala wa kampuni mnamo
1890
- koloni la
Dola la Ujerumani
(kwa Kijerumani
Deutsches Reich
) lililoamua kuchukua mamlaka mkononi mwake kuanzia
1891
, ambako Ujerumani iliweza kupanusha utawala wake juu ya maeneo yote
- mwisho wa utawala wa Kijerumani wakati wa
Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia
kuanzia mwaka
1916
wakati jeshi kubwa la
Uingereza
na
Afrika Kusini
pamoja na
Ubelgiji
lilivamia, hadi kusalimu amri kwa jeshi la
Schutztruppe
kwenye Novemba
1918
Katika mapatano baada ya vita koloni liligawiwa kati ya Uingereza (iliyopata Tanganyika) na Ubelgiji (iliyopata Rwanda na Burundi). Kwa historia ya baadaye ilikuwa na maana ya kwamba walikabidhiwa maeneo ya koloni la Kijerumani la awali si kama
mali
kamili lakini kama
maeneo ya kudhaminiwa
kwa niaba ya
shirikisho la Mataifa
(mtangulizi wa
Umoja wa Mataifa
(UN).
Hadi mnamo mwaka
1880
serikali
ya
Ujerumani
chini ya
chansella
Otto von Bismarck
ilikataa kuanzisha makoloni. Sehemu ya
wafanyabiashara
Wajerumani walidai koloni. Walisikitika kuona
faida
za wenzao
Waingereza
waliopata mara nyingi msaada kutoka kwa
wanajeshi
na serikali za koloni za Uingereza hasa
Asia
. Waliona pia faida ya
viwanda
vya Uingereza vilivyokuwa na
soko
la kulindwa katika nchi kama
Uhindi
kwa sababu serikali ya kikoloni ilidai
kodi
kali kwa
bidhaa
zisizotoka
Uingereza
.
Bismarck hakuamini ya kwamba koloni lingeleta faida kwa
taifa
kulingana na
gharama
kubwa kwa serikali. Lakini wapigania koloni walikuwa na
wabunge
muhimu kwa serikali na polepole Bismarck alianza kukubali hatua za kwanza.
Mwenyewe aliamini mwanzoni ya kwamba itatosha kuwapa wafanyabiashara
ulinzi
kwa shughuli zao kwa kuwaruhusu matumizi ya
bendera
ya Ujerumani na kuwa na
askari
wao wa ulinzi kama wamepatana na viongozi wazalendo katika eneo fulani kuanzisha shughuli huko. Kwa njia hii alifungua
mlango
kwa
harakati
iliyoendelea kuwa mchango wa Ujerumani katika
mbio
wa kugawa
dunia
, hasa
Afrika
.
Koloni hili lilianzishwa na kijana Mjerumani
Karl Peters
mwaka 1885 kwa niaba ya "
Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki
".
Peters, aliyewahi kusoma
chuo
Uingereza, aliona
wivu
juu ya ukoloni wa Uingereza, akiamini ya kwamba Ujerumani ungestahili nafasi hiyo pia. Hivyo alianza kudai koloni katika mikutano, akaanzisha "
Shirika kwa Ukoloni wa Kijerumani
" mwaka
1884
iliyokuwa kitangulizi cha kampuni.
Shirika hii ilimtuma pamoja na wenzake wawili kwenda Afrika na kutafuta nafasi ya kuanzisha koloni. Kiasili walilenga maeneo mpakani mwa Msumbiji na Zimbabwe ya leo lakini hatimaye waliamua kwenda Afrika ya Mashariki. Peters alifika
Zanzibar
alipoambiwa na
konsuli
ya Ujerumani ya kwamba hawezi kuendelea: serikali ya nyumbani iliogopa ugomvi na Uingereza ilikataa mipango yake. Aliamua kuvuka
barani
hata hivyo akafika
Saadani
tarehe
10 Novemba
1884
na kufuata njia kando ya
mto Wami
ili apite kanda la Kizanzibari kwenye
pwani
na kutembelea
machifu
na
masultani
ndani ya bara.
Hapo alifaulu kushawishi watawala wa maeneo yaliyojulikana kama
Usagara
,
Nguru
,
Useguha
na
Ukami
kutia
sahihi
kwenye mikataba iliyoandikwa kwa Kijerumani ambayo hawakuielewa. Mikataba hii ilisema ya kwamba
mtawala
alikabidhi kwa kampuni nchi yake pamoja na
haki
juu ya
ardhi
na
mali
yote.
Mwaka 1885 Peters alirudi
Berlin
na kuonyesha mikataba yake kwa
magazeti
na serikali.
Chansela Bismarck
alikataa, akacheka mikataba kama
karatasi
bila maana.
Peters alitumia
mbinu
: akatisha kupeleka mikataba yake kwa mfalme
Leopold II wa Ubelgiji
aliyekuwa kununua haki zake. Hapa Bismarck aliogopa kilio cha wapenda koloni akakubali kumpa Peters
hati ya ulinzi
ya tarehe
27 Februari
1885
kwa maeneo yaliyokuwa ya kampuni kufuatana na mikataba.
Peters na wawakilishi wake walirudi wakaendelea kutafuta machifu waliokuwa tayari kutia
saini
mikataba yake.
Sultani wa Zanzibar
alipinga juhudi hizi. Zanzibar ilisimamia pwani ya
Afrika ya Mashariki
na tangu
karne
watu wa
miji
ya pwani walikuwa na
mawali
wa Sultani.
Zanzibar ilidai pia utawala ya bara hadi
Ziwa Tanganyika
na
Kongo
, ingawa hali halisi
athira
yake haikwenda mbali na
njia
za misafara ambako
ndovu
na
watumwa
walipelekwa pwani.
Tarehe
27 Aprili
1885 serikali ya Zanzibar ilituma barua
Berlin
kupinga
kazi
na madai ya kampuni na kutangaza maeneo ya Tanzania ya leo kama
milki
yake. Iliongeza pia wanajeshi wake barani zilizokuwa chini ya
amri
ya
mwanajeshi
mstaafu Mwingereza
Matthews
. Hapo serikali ya Berlin ilituma kikosi cha
manowari
kwenda
Bahari Hindi
.
Mwezi Agosti manowari za Kijerumani chini ya amri ya
admirali
Eduard von Knorr
zilifika mbele ya
Unguja
zikalenga
mizinga
yao kwa
ikulu
ya sultani. Akishauriwa na
balozi
wa Uingereza,
Sultani Bargash
alipaswa kutoa tamko kuwa, "Kutokana na madai tunayopelekewa kwa matishio na
Kaisari
wa Ujerumani, tunatambua ulinzi wa Ujerumani juu ya nchi za Usagara, Nguru, Useguha, Ukami na juu ya
wilaya
ya
Witu
. Mipaka yake itaelezwa baadaye na sisi tunatambua ulinzi wa Kaisari juu ya mahali palipotajwa."
[5]
.
Sultani alipaswa pia kutia sahihi
mkataba
wa
biashara
na Ujerumani alipokubali haki nyingi kwa Wajerumani katika milki yake.
[6]
Mwaka
1886
Uingereza na Ujerumani walipatana juu ya "maeneo ya masilahi" yao katika Afrika ya Mashariki; hapa walielewana kuhusu mstari kati ya mdomo wa
mto Umba
(kati ya
Tanga
na
Mombasa
) hadi nukta ambako
latitudo
ya 1 kusini inakata mwambao wa
Ziwa Viktoria Nyanza
[7]
. Sultani alipaswa kukubali tena. Katika mapatano hayo Sultani alibaki na
visiwa
vya
Unguja
,
Pemba
,
Mafia
na
funguvisiwa ya Lamu
pamoja na kanda la pwani barani lenye
upana
wa
maili
10 kati ya
mto Ruvuma
upande wa
Kusini
na
mto Tana
upande wa
Kaskazini
, halafu miji ya
Kismayu
,
Barawa
,
Merka
na
Mogadishu
upande wa kaskazini zaidi.
[8]
.
Mkataba kati ya Zanzibar na Kampuni juu ya kofo na pwani
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Mapatano ya 1886 yaliwapa Wajerumani nafasi ya kuendeleza upanuzi barani nyuma ya kanda la pwani la Kizanzibari na
mstari
wa
mpaka
ulichorwa kuanzia
mdomo
wa
mto Umba
kupitia
mlima Kilimanjaro
hadi
Ziwa Viktoria
. Lakini kwa ajili ya matumizi ya kibiashara suala la
mabandari
bado lilibaki wazi. Hapo Peters na kampuni yake walianza kujadiliana na Sultani
Seyyed Bargash
(alitawala 1870 hadi 1888) kuhusu utawala wa pwani katika sehemu ya
Tanganyika
.
Mnamo mwaka
1887
Bargash alikuwa amechoka: alitafuta
pesa
tu kwa ajili yake binafsi; alikuwa tayari kukodisha utawala wa kanda la pwani ya Tanganyika kwa Wajerumani. Wajerumani walidai kuongezeka haki na Bargash alikufa bila kumaliza mapatano.
Lakini mwandamizi wake
Sultani Seyyed Khalifa
aliwapa Wajerumani walichotaka. Tarehe
15 Agosti
1888
wawakilishi wa kampuni ya Kijerumani walifika kwenye mabandari yote wakatangaza utawala wao kwa niaba ya sultani.
Vita ya Abushiri na mwisho wa utawala wa Kampuni
[
hariri
|
hariri chanzo
]
tazama
Vita ya Abushiri
Badiliko hili lilisababisha
upinzani
na hatimaye
ghasia
ya wenyeji. Vipengele vya mkataba vilisema mali isiyokuwa na
hati
za kimaandishi haiwezi kutambuliwa. Wenye mali kama
mashamba
walitakiwa kununua hati kutoka kwa watawala wapya. Hapo
Waswahili
wa pwani walijisikia wamesalitiwa na sultani asiyekuwa na haki ya kuchukua mali zao na kuzipa kwa
wageni
.
Mara baada ya kufika kwa Wajerumani kwenye miji ya pwani ghasia ilianza mjini
Pangani
na kuenea haraka kote pwani kati ya
Tanga
na
Lindi
.
Kampuni ilikuwa na Wajerumani wachache tu walioshindwa kujitetea. Walipaswa kukimbia au wakauawa.
Bagamoyo
pekee palikuwa na kikosi cha askari kutoka manowari ikatetewa.
Serikali ya Ujerumani iliona lazima kuingia kati na kutuma manowari pamoja na askari waliokandamiza ghasia. Bismarck alitumia mbinu wa kupata kura za bunge alizohitaji kwa ajili ya gharama ya vita hiyo. Alipeleka sheria bungeni kuwa Ujerumani unatoa
mark
milioni 2 kwa kupambana na biashara ya watumwa na ulinzi wa manufaa ya Kijerumani. Sasa alimtuma afisa wa jeshi mwenye maarifa ya Afrika,
Hermann von Wissmann
aliyeajiri maafisa na wanajeshi Wajerumani, kwa jumla watu 87 wakaelekea Afrika ya Mashariki. Njiani walipopita
Misri
waliajiri askari waliostaafishwa Wasudani 650; waliongeza baadaye askari Wazulu 350 kutoka Msumbiji na kuwaunganisha kuwa "
kikosi cha Wissmann
" kilichofaulu kushinda upinzani wote kwa msaada wa silaha za kisasa na manowari za Ujerumani
[9]
.
Baada ya upinzani wa wenyeji wa pwani mwaka
1889
/
1890
wakiongozwa na
Abushiri
na
Bwana Heri
serikali ya Ujerumani iliamua kutwaa
mamlaka
kutoka kwa kampuni na kufanya eneo lote kuwa koloni la Dola la Ujerumani badala ya shirika.
Maeneo ya kampuni yalikuwa rasmi koloni la serikali tarehe
1 Januari
1891
. Koloni lilisimamiwa na gavana.
Magavana wa Kijerumani walikuwa wafuatao:
[10]
Utawala wa Kijerumani ulikwisha katika
Vita Kuu ya Dunia ya Kwanza
(
1914
- 1918) kutokana na uvamizi wa
Uingereza
na
Ubelgiji
.
Katika
Mkataba wa Versailles
mwaka 1919 eneo la koloni la Kijerumani liligawiwa. Sehemu ya
Tanganyika
ilikabidhiwa kwa Uingereza na maeneo ya Rwanda na Burundi yaliwekwa chini ya
Ubelgiji
.
Eneo lote la koloni liligawiwa katika mikoa 21 na maeneo matatu yaliyokuwa bado chini ya watawala wenyeji kwa mfumo wa
maeneo lindwa
. Hadi 1913 mikoa 19 ilikuwa chini ya utawala wa kiraia, yaani chini ya maafisa wa serikali ya kikoloni. Mikoa miwili ya
Iringa
na
Mahenge
ilikuwa bado chini ya utawala wa kijeshi yaani hapo walikuwa maafisa wa Schutztruppe waliotekeleza majukumu yote ya serikali.
Mikoa chini ya usamimizi wa maafisa Wajerumani wa kiraia ilikuwa:
1.
Tanga (DOA)
2.
Pangani (DOA)
pamoja na ofisi ndogo
Handeni
3.
Bagamoyo (DOA)
pamoja na ofisi ndogo
Saadani
4. Daressalam pamoja na ofisi ndogo ya polisi
Kisangire
5.
Rufiji (DOA)
, makao makuu
Utete
6.
Kilwa (DOA)
pamoja na ofisi ndogo za Kilindoni, Kibata na
Liwale
7.
Lindi (DOA)
pamoja na ofisi ndogo za
Mikindani
,
Newala
und
Tunduru
8.
Langenburg (DOA)
(Tukuyu) pamoja na ofisi ndogo Itaka na Mwakete na kituo cha polisi Muaja
9.
Wilhelmstal (DOA)
(
Lushoto
)
10.
Morogoro (DOA)
pamoja na ofisi ndogo za
Kilossa
na Kissaki
11.
Songea (DOA)
pamoja na ofisi ndogo
Wiedhafen
12.
Moshi (DOA)
13.
Arusha (DOA)
pamoja na ofisi ndogo Umbulu
14.
Kondoa-Irangi (DOA)
pamoja na ofisi ndogo Mkalama
15.
Dodoma (DOA)
pamoja na kituo cha polisi
Mpapwa
na kituo cha kijeshi
Singida
16.
Mwanza (DOA)
pamoja na ofisi ndogo Shirati na kituo cha kijeshi Ikoma
17.
Tabora (DOA)
pamoja na ofisi ndogo za
Shinyanga
na Ushirombo
18.
Ujiji (DOA)
pamoja na kituo cha kijeshi Kasulo
19.
Bismarckburg (DOA)
(Kasanga (Ufipa)
Mikoa ya kijeshi (jer.
Militarbezirke
) chini ya usimamizi wa maafisa wa Kijerumani wa kijeshi:
21.
Iringa (DOA)
pamoja na kituo cha kijeshi Ubena
22.
Mahenge (DOA)
Maeneo lindwa
(jer.
Residentur
) chini ya watawala wenyeji waliopaswa kufuata ushauri wa afisa mkazi Mjerumani (jer.
Resident
):
Bukoba
pamoja na vituo vya kijeshi Usuwi na Kifumbiro, kwa ajili ya watawala wa
Wahaya
Rwanda
, mji mkuu
Kigali
, kituo cha kijeshi Mruhengeri
Burundi
, mji mkuu
Gitega
, pamoja na ofisi ndogo Usumbura (
Bujumbura
).
- ↑
No. 123 Agreement between the British and German Governments, respecting the Sultanate of Zanzibar and the opposite East African Mainland, and their Spheres of Influence - 1st November, 1886
(in: Map of Africa by Treaty Vol II, p. 617 and p. 620) "3. Both powers agree to establish a delimitation of their respectives spheres of influence on this part of the East African Continent" "Line of Demarcation. The line of demarcation starts from the mouth of the River Wanga or Umbe, runs direct to Lake Jipe, passes thence along the eastern and round the northern side of the lake and crosses the Lumi River; After which it passes midway between the territories of Taveita and Chagga, skirts the northern base of the Kilimanjaro range, and thence is drawn direct to the point on the eastern side of Lake Victoria Nyanza which is intersected by the 1st degree of south latitude"
- ↑
"Great Britain shall bring to bear her full influence on the Sultan of Zanzibar to facilitate an amicable agreement by which the Sultan unconditionally cedes to Germany the Island of Mafia and his territories on the mainland (including dependencies) that are referred to in the existing concessions of the German East Africa Company. It is understood that His Highness shall receive fair compensation for the loss of revenue resulting from this cessation." (
Anglo-German Treaty (Heligoland-Zanzibar Treaty), July 1, 1890 online hapa
kwa
http://germanhistorydocs.ghi-dc.org
)
- ↑
Wakati ule bado kwa
Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki
, kwa sababu serikali haikumaliza bado kutwaa haki au zaidi madai ya kampuni katika Afrika
- ↑
Kamusi ya Koloni za Kijerumani
, makala "Deutsch-Ostafrika", fungu 9. Bevolkerungsstatistik.
- ↑
nukuu ya Kiingereza katika
Franz Kotrba: William Astor Chanler (1867-1934) und Ludwig von Hohnel (1857-1942) und Afrika, Vienna 2008
- ↑
Mkataba wa urafiki na biashara kati Dola la Ujerumani na Sultani wa Zanzibar
(Kijerumani + Kiingereza)
- ↑
Nukta hii ilisogezwa kidogo kusudi la kutokata rasi ya Muhuru inayoingia ziwani kwa umbo la pinde
- ↑
Februari 1887 Sultani aliendelea kupungukiwa maeneo alipopatana na Mwingereza
William Mackinnon
kumkodisha pwani ya
Kenya
pamoja na haki za utawala kwa malipo ya kila mwaka. Kisheria kanda hili lilibaki mali ya Zanzibar hadi
uhuru
wa Kenya mwaka
1964
- ↑
Makala "Araberaufstand" katika
Kamusi ya Koloni za Kijerumani
, Berlin 1920
- ↑
A. J. Dietz.
"A postal history of the First World War in Africa and its aftermath - German colonies: II Kamerun"
. African Studies Centre, Repository, Leiden University
. Iliwekwa mnamo
17 January
2018
.
- Pugu Hadi Peramiho - kimehaririwa na P. Gerold Rupper, OSB, BPNP, Peramiho 1988,
ISBN 9967 67 031 1
|
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|