Mtakatifu Yohane wa Avila.
Mtakatifu Yohane wa Avila.
Yohane wa Avila
(
Almodovar del Campo
,
Hispania
,
6 Januari
1499
au
1500
-
Montilla
, Hispania,
10 Mei
1569
) alikuwa
padri
mwanajimbo
wa
Hispania
aliyeathiri sana
Kanisa Katoliki
la nchi hiyo na
urekebisho wa Kikatoliki
katika
karne ya 16
hasa kwa njia ya mahubiri yake yaliyotegemea
Biblia
, ya
uongozi wa kiroho
na ya vyuo alivyovianzisha.
Kwa namna ya pekee mkoa wa
Andalusia
na watakatifu
Teresa wa Yesu
,
Yohane wa Mungu
na
Fransisko Borja
walifaidika na
utume
wake.
Papa Leo XIII
alimtangaza
mwenye heri
tarehe
6 Aprili
1894
, halafu
Papa Paulo VI
akamtangaza
mtakatifu
tarehe
31 Mei
1970
.
Hatimaye
Papa Benedikto XVI
akamtangaza
mwalimu wa Kanisa
wa 34 tarehe
7 Oktoba
2012
.
[1]
Sikukuu
yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 10 Mei
[2]
.
Yohane wa Avila alizaliwa huko
Almodovar del Campo
(Ciudad Real, katika
Jimbo Kuu
la
Toledo
, Hispania) tarehe 6 Januari 1499 au 1500 katika
familia
tajiri
na yenye
imani
ya
Kikristo
[3]
ingawa yenye asili ya
Kiyahudi
.
[4]
Baba
yake aliitwa Alonso Avila na
mama
Katalina Gijon.
Akiwa mtoto pekee, alipofikia umri wa miaka 14 alitumwa masomoni kwenye
chuo kikuu
cha
Salamanca
ili ajifunze
sheria
, lakini baada ya miaka miwili akarudi nyumbani kutokana na
wongofu
wa dhati akatumia miaka mitatu kufanya
toba
kali, kusali na kutafakari.
Utakatifu
wake ulimvutia
Mfransisko
ambaye alipitia Almodovar, akamshauri aanze masomo ya
falsafa
na
teolojia
kwa ajili ya
upadri
huko
Alcala de Henares
, alipofundishwa na
Mdominiko
maarufu,
Domingo de Soto
.
Chuo
hicho kilikuwa wazi kwa mitazamo mbalimbali ya wakati ule na kwa
tapo
la
Renaissance
lililojali sana
binadamu
na mambo yake yote.
Wakati wa masomo hayo alifiwa wazazi; hivyo baaada ya
upadrisho
wake (
1526
) aliuza mali ya familia na kuwagawia
maskini
mapato yake.
Yeye aliona vifo hivyo kuwa ishara ya
Mungu
kumwita awe
mmisionari
akajiandaa kwenda
Mexico
.
Mwaka
1527
, akiwa
Seville
ili kupata nafasi nzuri ya kusafiri baharini, alijitosa kuhubiri mjini na kandokando yake. Namna yake bora ya kuishi, kuadhimisha
Misa
na kuhubiri ilimshangaza
padri
Hernando de Contreras,
mwalimu
wa Alcala maarufu upande wa
katekesi
, ambaye alimuarifu
Askofu mkuu
wa Seville, na pia
Hakimu mkuu
Alonso Manrique de Lara
.
Askofu
alitambua kwamba huyo padri kijana anafaa sana kuchochea imani mkoani
Andalusia
, na baada ya kumshauri sana alimfanya akubali kuacha mpango wa kwenda
Amerika
.
Basi, akabaki na Hernando, akishiriki naye maisha ya
ufukara
na
sala
na kuendelea na masomo yake katika Chuo cha
Mtume Thoma
. Labda ndipo alipopewa jina “Mwalimu”, lililoendelea kutumika kwa ajili yake hata kisha kufa.
Alianza kuhubiri tarehe
22 Julai
1529
, akapata mara umaarufu.
Katika miaka tisa aliyofanya utume huko Andalusia, mahubiri yake yote yalisikilizwa na umati wa watu waliobanana.
Hata hivyo, nguvu ya maneno yake kwa ajili ya
urekebisho
na dhidi ya mwenendo wa ma
tabaka
ya juu katika
jamii
ilisababisha mwaka
1531
afikishwe mbele ya Hakimu mkuu wa
Seville
.
Shtaka
lilikuwa kwamba alizidisha
hatari
ya kiroho inayotokana na
utajiri
na hivyo kuwafungia matajiri milango ya
mbinguni
. Lakini aliweza kujitetea vizuri na kuachiliwa mwaka
1533
baada ya kufungwa
gerezani
zaidi ya mwaka mmoja, akateuliwa kuhubiri tena
[5]
kwa watu wa kawaida na kwa wale wenye
mamlaka
.
Akiwa gerezani alianza kuandika
kitabu
chake bora; pia alijaliwa kuzama katika
fumbo
la
upendo
wa
Mungu
uliofunuliwa kumpitia
Yesu Kristo
na katika
fadhili
ambazo binadamu wamepata kutoka kwa
Mkombozi
huyo.
Tangu hapo hizo mbili zikawa
nguzo
za maisha yake ya Kiroho na
mada
kuu za mahubiri yake, pamoja na kutangaza nafasi ya kwanza ya
neema
, inayohimiza matendo mema, na kuhamasisha
tumaini
kwa Mungu na
itikio
kwa upendo wake unaoita wote wawe watakatifu.
Kama
wanasala
wengine wa
Hispania
wakati huo, alishukiwa mara kadhaa kuhusika na
Alumbrados
, waliotazamwa kama
wazushi
.
Urekebisho wa mapadri nchini Hispania
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Pamoja na kwamba Yohane aliwahi kuelekeza wote kwenye
utakatifu
, alichangia sana
ustawi
wa teolojia ya upadri, akisababisha kati ya wanajimbo
juhudi
kubwa za Kiroho na kuathiri waandishi waliofuata. Kiini cha mafundisho yake kuhusu jambo hilo ni kwamba “wakati wa
Misa
sisi (mapadri) tunajiweka juu ya
altare
katika
nafsi
ya
Kristo
ili kutekeleza kazi ya Mkombozi mwenyewe”; hiyo inadai kutimiza kwa
unyenyekevu
upendo wa kibaba na wa kimama wa Mungu, kwa hiyo kuwa na mtindo wa maisha wa pekee.
Hivyo anakumbukwa hasa kwa kurekebisha
Kanisa
kwa kuboresha maisha ya mapadri nchini Hispania, ingawa hakuanzisha shirika lolote kwa ajili yao.
[5]
Wakleri
watakatifu ni
haja
ya msingi kwa
urekebisho
wa Kanisa, na hilo linadai
uchambuzi
makini na
malezi
ya kufaa kwa walioelekea upadri. Hivyo alihimiza uanzishaji wa
seminari
na wa vyuo maalumu kwa
elimu
ya Biblia. Mapendekezo hayo yalikuja kuathiri Kanisa lote.
Ni kwamba, kwa kutia maanani sana malezi, alianzisha mwenyewe vyuo kadhaa ambako wanafunzi wake walijitosa kufundisha vijana.
[6]
Baada ya
Mtaguso wa Trento
, hivyo vikawa seminari kadiri ya maagizo ya
mtaguso
huo.
Umuhimu wa pekee kati ya mafanikio yake unacho
Chuo kikuu cha Baeza
kilichoanzishwa naye mwaka
1538
kwa
hati
ya
Papa Paulo III
[7]
na ambacho akawa
gombera
wake wa kwanza
[8]
hata bila kufundisha mwenyewe, isipokuwa Biblia kwa
walei
,
watawa
na wakleri, kwa sababu alitamani sana ijulikane na wote.
Chuo hicho katika
karne
zilizofuata kikawa kielelezo kwa
seminari
na kwa
shule
za
Wajesuiti
, ambao wanamheshimu kwa pekee kwa kuwasaidia kustawi Hispania hasa kwa kuelekeza kwao wanafunzi wake bora 30 hivi.
[5]
Mwenyewe alitamani kujiunga nao, asiweze ingawa alikaribishwa na
Ignasi wa Loyola
aliyemheshimu sana.
Kati ya watakatifu
rafiki
zake kuna pia padri
Mfransisko
Petro wa Alcantara
na maaskofu
Thoma wa Villanova
na
Yohane wa Ribera
.
Baada ya utume wake wa miaka tisa mkoani Andalusia, alirudi Seville, ambako aliondoka tu kwa kazi kubwa zaidi huko
Cordoba
, alipojiunga na
jimbo
moja kwa moja,
Granada
(
1536
), alipohitimu masomo ya
chuo kikuu
,
Baeza
,
Montilla
na
Zafra
.
Miaka kumi na nane ya mwisho aliugua mfululizo, kutokana na ugumu wa maisha na wa kazi alizofanya kwa miaka arubaini. Mwaka
1554
alihamia nyumba ndogo ya Montilla, alipoendeleza
utume
wake kwa kuandika
barua
nyingi na vitabu kadhaa.
Askofu mkuu wa Granada alitaka aende naye kama
mtaalamu
wa teolojia kwenye vikao vya mwisho vya Mtaguso wa Trento, lakini
afya
haikumruhusu kusafiri. Hata hivyo “Memoriales” (“Kumbukumbu”) alizoziandika kwa ajili hiyo, ziliathiri sana mtaguso huo.
Alifariki tarehe
10 Mei
1569
asubuhi
huko
Montilla
akishika
msalaba
na kuzungukwa na wafuasi na marafiki.
Kati ya mengineyo, Yohane alipendekeza ianzishwe
mahakama ya kimataifa
ya
usuluhishi
ili kuepa
vita
, pia alibuni na kusajili vifaa kadhaa vya
uhandisi
.
Akiishi kifukara sana, alijitosa hasa kuhimiza maisha ya Kikristo kati ya wale waliomfuata kila mahali ili kumsikiliza.
Wale wote walioongozwa naye kiroho walitambua mapema kipaji chake cha pekee cha kupenya
fumbo la Kristo
, kwamba
baraka
zote zinatujia kwa njia yake; kwamba tunachuma matunda ya
ukombozi
kadiri tunavyoungana naye; kwamba
muungano
huo unaanza na
imani
na
ubatizo
na kukamilishwa na
ekaristi
; na kwamba kujitoa kabisa kwake kunazaa ndani mwetu
tumaini
na
furaha
.
“Fungua
moyo
wako mdogo upokee ile
pumzi
ya upendo ambao kwao
Baba
anatupatia Mwanae, na kwa njia yake anajitoa kwetu pamoja na
Roho Mtakatifu
na vingine vyote”.
Maandishi yake yalikusanywa huko
Madrid
miaka
1618
,
1757
,
1792
na
1805
; yote yanang’aa kwa kufafanua mada kwa dhati, kwa
mbinu
rahisi na kwa mifano mingi; kati yake, maarufu zaidi ni:
"Audi Filia, et vide"
(“Sikiliza, binti, na uone”) kuhusu
ukamilifu
wa Kikristo, na
"Barua za Kiroho"
kwa wafuasi wake
[9]
zilizotafsiriwa mapema katika
lugha
mbalimbali.
Pia kuna
katekisimu
kwa
watoto
na
watu wazima
inayoitwa “Mafundisho ya Kikristo”, “
Insha
juu ya Upendo wa Mungu”, inayoshirikisha dhati ya fumbo la Kristo, “Insha juu ya Upadri”, “Maelekezo kuhusu Urekebisho”, “
Hotuba
”, “
Maongezi
” na
ufafanuzi
wa vitabu mbalimbali vya Biblia, kama vile
barua kwa Wagalatia
na
ile ya kwanza ya Yohane
.
Katika kusoma Biblia alitumia na kulinganisha
tafsiri
mbalimbali, alichunguza maneno yenyewe na maana yake ya Kiroho, pamoja na kutegemea sala na kuwa na
uzoefu
na maelezo ya ma
babu wa Kanisa
.
Pengine hakuandika zaidi kwa kuogopa
hukumu
kali za
Mahakama ya Imani
ya wakati ule.
WikiMedia Commons