Umoja wa Mataifa
(
UM
) (
Kiingereza
:
United Nations
, UN) ni shirika la kiserikali ambalo malengo yake ni kudumisha
amani
na
usalama
wa kimataifa, kuendeleza uhusiano wa kirafiki kati ya mataifa, kufikia ushirikiano wa kimataifa, na kuwa kituo cha kuoanisha matendo ya mataifa. Ni
umoja
wa
nchi
zote
duniani
isipokuwa zile zisizotambuliwa kuwa
dola huru
.
Umoja huo ulianzishwa na nchi washindi wa
Vita Kuu ya Pili ya Dunia
kuchukua nafasi ya
Shirikisho la Mataifa
(
1919
-
1946
). Makubaliano yalifikiwa
tarehe
24 Oktoba
1945
huko
San Francisco
,
California
.
Mwanzoni nchi zilikuwa 51 lakini kufikia mwaka
2017
kulikuwa na nchi wanachama 193, mbali ya
Ukulu mtakatifu
(
Vatikani
) na
Palestina
ambazo zinashiriki kama
watazamaji wa kudumu
, zikiwa na
haki
karibu zote isipokuwa kupiga
kura
.
Dhumuni la umoja huu ni kuratibu mahusiano ya kimataifa kupitia
sheria
na mikataba ya kimataifa kwenye maeneo kama
usalama
,
amani
,
maendeleo ya jamii
na ya
uchumi
,
haki za binadamu
,
uhuru
,
demokrasia
n.k.
Toka mwanzo
makao makuu
ya Umoja wa Mataifa yako
Manhattan
,
New York City
,
New York
nchini
Marekani
na hayako chini ya
mamlaka
ya nchi hiyo.
Ofisi
nyingine ziko
Geneva
(
Uswisi
),
Nairobi
(
Kenya
) na
Vienna
(
Austria
).
Lugha rasmi
za UM ni
sita
:
Kiarabu
,
Kichina
,
Kifaransa
,
Kihispania
,
Kiingereza
na
Kirusi
.
Katibu Mkuu wa UM
anachaguliwa kwa miaka mitano; kwa sasa ni
Antonio Guterres
kutoka
Ureno
, aliyechaguliwa kuwa Katibu Mkuu mwaka
2016
akichukua nafasi ya
Ban Ki-moon
.
Muundo wa UM
UM una vyombo vitano:
Cha sita kilikuwa
Baraza la Wafadhili la UM
(Trusteeship Council), ambacho kimesimama mwaka
1994
.
Baraza la Usalama linaamua kutuma
walinzi wa amani wa UM
penye maeneo ya ugomvi.
Mashirika ya pekee ya UM
- UNICEF
(United Nations Children's Fund) - Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa
- WHO
(World Health Organization) Taasisi ya Afya ya Ulimwengu
- FAO
(Food and Agriculture Organization) - Taasisi ya Chakula na Kilimo
- UNESCO
(United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization) - Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi, na Utamaduni
- ILO
(International Labour Organization) Taasisi ya Kimataifa ya Kazi
- IMF
(International Monetary Fund) - Mfuko wa Fedha wa Kimataifa
- UNCTAD
(United Nations Conference on Trade and Development) - Mkutano wa Kimataifa kuhusu Biashara na Maendeleo
- ITC
(International Trade Centre (UNCTAD/WTO) -
- UNDCP
(United Nations Drug Control Programme) - Taasisi ya Kimataifa ya Mpango wa Kusimamia Madawa
- UNDP
(United Nations Development Programme) - Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo
- UNIFEM
(United Nations Development Fund for Women) Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Wanawake
- UNV
(United Nations Volunteers)
- UNEP
(United Nations Environment Programme) Mpango wa Kimataifa wa Mazingira
- UNFPA
(United Nations Fund for Population Activities)
- UNHCR
(Office of the United Nations High Commissioner for Refugees)
- UN-HABITAT
(United Nations Human Settlements Programme)
- UNRWA
(United Nations Relief and Works Agency for Palestine Refugees in the Near East)
- IAEA
(Shirika la Kimataifa la Nishati ya Nyuklia) inashirikiana na UM na kutoa taarifa kwa Baraza la Usalama hata kama si chini ya katiba ya UM
- UNDIO
( United Nations Data and Information Organization)
Viungo vya nje
Tovuti rasmi
Tanbihi