Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Robert Mugabe
|
Robert Mugabe
2009
|
|
Tarehe ya kuzaliwa
|
21 Februari 1924
|
Tarehe ya kifo
|
6 Septemba 2019
|
Chama
|
ZANU
|
Kazi
|
Rais
|
Robert Gabriel Mugabe
(
21 Februari
1924
-
6 Septemba
2019
) alikuwa
kiongozi
mkuu wa
Zimbabwe
tangu
1980
hadi
2017
. Alikuwa
mwenyekiti
wa
chama tawala
cha
ZANU
.
Mwaka 1980 alikuwa
waziri mkuu
na mwaka
1987
Rais wa Zimbabwe
. Kabla ya wakati ule aliongoza upinzani wa ZANU dhidi ya
serikali
ya
walowezi
Waingereza
nchini waliofuata
siasa
ya
ubaguzi wa rangi
.
Mugabe alirudia kushinda katika
uchaguzi
mara kadhaa. Tangu mwaka 2000 chaguzi hizo zilitiwa shaka kutokana na matishio na matumizi ya mabavu dhidi ya wapinzani.
Utawala
wa Mugabe umeitwa wa
kidikteta
tangu mwaka
2002
. Kutokana na mashtaka dhidi ya serikali ya Mugabe ya kudharau
haki za binadamu
, nchi ya Zimbabwe ilisimamishwa ndani ya
Jumuiya ya Madola
. Mugabe pamoja na
mawaziri
wake na viongozi wa chama chake hawakuruhusiwa kusafiri kwenda nchi za
Umoja wa Ulaya
na
Marekani
.
Mwanzoni mwa utawala wake Mugabe alisifiwa kujenga
uchumi
na sera ya
elimu
nchini. Zimbabwe ilikuwa nchi iliyouza
chakula
kwa wingi nje. Tangu mwanzo wa
milenia
mpya pamoja na mashtaka ya udikteta hali ya uchumi ilirudi nyuma. Takriban
raia
milioni
mbili
wa Zimbabwe wameondoka nchini wakakaa kama
wakimbizi
Afrika Kusini
.
Tuhuma za mauaji na ukandamizaji
Nchi hiyo ilikuwa tayari imegawanyika kikabila hata katika uchaguzi wa kwanza wa 1980, Mashona wote walimchagua Mugabe na
Wandebele
na
wabunge
kutoka chama cha ZANU. Wakati Wandebele walichagua viongozi kutoka chama cha
ZAPU
kilichoongozwa na
Joshua Nkomo
.
Baada tu ya kushika
madaraka
, Mugabe aliamua kukandamiza upinzani dhidi yake aliyoona kati ya wanachama wa ZAPU na wanajeshi wake wa ZIPRA waliowahi kurudi. Alishinda majaribio ya uasi wa askari wa
ZIPRA
1980 kwa msaada wa vikosi vya Rhodesian Defence Force. 1981 Mugabe aliunda kikosi kipya cha "Brigedi ya Tano" kilichofanywa na wanamgambo wa
ZANLA
wa awali (jeshi la chama chake ZANU) na kufundishwa na washauri kutoka Korea Kaskazini. Brigedi hii ilitumwa katika maeneo ya Wandebele katika kusini ya Zimbabwe (mazingira ya
Bulawayo
) kutafuta askari wa ZIPRA mafichoni; katika mauaji ya
Gukurahundi
yaliyoendelea hadi 1984 ni Wazimbabwe 20,000 wanakadiriwa waliuawa.
Ingawa
mauaji
hayo hayakufikia kiwango cha yale ya
Rwanda
na
Burundi
, waliuawa
wanawake
,
wanaume
,
watoto
na hata vichanga vilivyokuwa matumboni.
Kuanzia enzi hizo rais Mugabe amejaribu kushinda kila uchaguzi nchini huko kwa kutumia nguvu za kikabila na mabavu.
|
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Robert Mugabe
kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|