Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Panama
ni nchi ya mwisho
kusini
mwa
Amerika ya Kati
.
Shingo ya nchi
ya Panama hutazamwa kuwa
mpaka
kati ya
bara
la
Amerika ya Kaskazini
na lile la
Amerika ya Kusini
.
Imepakana na
Kosta Rika
na
Kolombia
; pwani ya
Bahari ya Karibi
iko upande wa
kaskazini
na pwani ya
Pasifiki
upande wa kusini.
Nchi iko kwenye sehemu nyembamba kabisa ya Amerika ya Kati.
Mfereji wa Panama
hukata shingo la nchi na kufanya jina la Panama kujulikana kote duniani.
Baada ya
ukoloni
wa
Hispania
Panama ilikuwa sehemu ya kaskazini ya
Kolombia
. Majaribio mbalimbali ya
uasi
dhidi ya Kolombia kwa
shabaha
ya kuwa nchi ya pekee katika
karne ya 19
hayakufaulu.
Ma
badiliko
makubwa yalikuja na
ujenzi
wa mfereji wa Panama.
Utangulizi wake ulikuwa
reli
kutoka
Colon
upande wa Karibi kwenda
mji wa Panama
upande wa Pasifiki iliyojengwa mwaka
1855
. Reli hii ilirahisisha
safari
kati ya Atlantiki na Pasifiki kwa watu na
bidhaa
kuelekea
Kalifornia
. Watu wengi walikwenda Kalifornia miaka ile kwa sababu ya
dhahabu
iliyopatikana kule tangu mwaka
1848
na hapakuwa na reli kati ya pwani zote mbili za
Marekani
wakati ule.
Wakati wa mwisho wa karne ya 19 Marekani ilianza kujenga
mfereji
kati ya
bahari
mbili wa kukata shingo la nchi.
Serikali
ya Marekani iliona umuhimu wa kutawala njia hii. Ikasaidia Wapanama waliotaka kujitenga na Kolombia kwa kutuma
manowari
Colon iliyozuia
jitihada
za Kolombia za kukandamiza
ghasia
hiyo.
Tarehe
3 Novemba
1903
Panama ilitangaza
uhuru
wake na kufanya
mkataba
na Marekani. Panama ilikodisha mlia wa nchi kwa pande zote mbili za mfereji kwa Marekani; Marekani iliahidi kutunza uhuru wa Panama.
Hali halisi ukanda wa mfereji ilikuwa eneo la Kimarekani hadi
31 Desemba
1999
iliporudishwa kwa serikali ya Panama.
Wakazi walio wengi (70%) ni ma
chotara
Waindio
-
Wazungu
, 14% wana asili ya
Afrika
au ni machotara wa Kiafrika, 10% ni Wazungu na 6% Waindio.
Lugha rasmi
na ya kawaida ni
Kihispania
.
Upande wa
dini
, 65-75% ni
Wakatoliki
na 15-25%
Waprotestanti
. Nje ya
Ukristo
, dini kubwa zaidi ni ile ya
Bahai
(2%).
- Buckley, Kevin,
Panama
, Touchstone, 1992.
ISBN 0-671-77876-5
- Diaz Espino, Ovidio,
How Wall Street Created a Nation
, Four Walls Eight Windows, 2001.
ISBN 1-56858-196-3
- Harding, Robert C.,
The History of Panama
, Greenwood Publishing, 2006.
- Harding, Robert C.,
Military Foundations of Panamanian Politics
, Transaction Publishers, 2001.
ISBN 0-393-02696-5
- Joster, R.M. and Sanchez, Guillermo,
In the Time of the Tyrants, Panama: 1968?1990
, W.W. Norton & Company, 1990.
- Mellander, Gustavo A.; Nelly Maldonado Mellander (1999). Charles Edward Magoon: The Panama Years. Rio Piedras, Puerto Rico: Editorial Plaza Mayor.
ISBN 1-56328-155-4
. OCLC 42970390.
- Mellander, Gustavo A. (1971). The United States in Panamanian Politics: The Intriguing Formative Years. Danville, Ill.: Interstate Publishers. OCLC 138568.
- Porras, Ana Elena,
Cultura de la Interoceanidad: Narrativas de Identidad Nacional de Panama (1990?2002)
, Editorial Carlos Manuel Gasteazoro, 2005.
ISBN 9962-53-131-4
- Serrano, Damaris,
La Nacion Panamena en sus Espacios: Cultura Popular, Resistencia y Globalizacion
, Editorial Mariano Arosemena, 2005.
ISBN 9962-659-01-9
- Villarreal, Melquiades,
Esperanza o Realidad: Fronteras de la Identidad Panamena
, Editorial Mariano Arosemena, 2004.
ISBN 9962-601-80-0
- Weeks, John and Gunson, Phil,
Panama. Made in the USA
, 1992.
ISBN 978-0-906156-55-1
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Amerika ya Kati
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Panama
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|