Kifaransa
(kwa Kifaransa:
francais
) ni lugha ya
Ufaransa
(pamoja na
maeneo yake ya ng'ambo
),
Ubelgiji
ya Kusini,
Uswisi
ya Magharibi,
Luxemburg
na
Kanada
. Inazungumzwa pia katika nchi nyingi za
Afrika
kama vile
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
,
Senegal
,
Mali
,
Shelisheli
,
Chad
, n.k.,
Asia ya Kusini
na
Amerika
zilizokuwa
makoloni ya Ufaransa
.
Takwimu kuhusu matumizi ya Kifaransa hutofautiana. Kadirio ndogo lasema kuna watu milioni 87 wanaotumia Kifaransa kama lugha ya kwanza, na tena milioni 100 wanaoitumia kama lugha ya pili. Kadirio kubwa lataja milioni 112,6 wasemaji wa lugha ya kwanza pamoja na milioni 60,6 wenye uwezo wa kutumia Kifaransa karibu kama lugha ya Mama. Halafu hutajwa takriban milioni 100 -110 wanaotumia Kifaransa kikazi, kibiashara au masomoni jumla takriban milioni 300 wasemaji wa Kifaransa duniani.
Kifaransa ni kati ya
lugha za Kirumi
. Asili yake ni
Kilatini
lugha ya
Waroma wa Kale
. Hadi mwaka 50 KK watu waliokalia
Gallia
(eneo la Ufaransa wa leo) walitumia lugha mbalimbali za
Kikelti
. Baada ya uvamizi na Waroma Gallia ilikuwa sehemu ya
Dola la Roma
. Lugha ya Kilatini ilienea hadi kuwa lugha ya watu wengi. Kikelti kimebaki hadi leo katika maeneo madogo kama
Ubritani
.
Kilatini hiki jinsi kilivyojadiliwa na watu wa kawaida katika Gallia kilipokea kiasi cha maneno na matamshi na lugha ya Kikelti. Baada ya mwisho wa Dola la Roma lugha iliendelea kubadilika haraka zaidi. Makabila ya
Kigermanik
walivamia Gallia na kuleta athira ya lugha zao.
Haya yote yaliunda lugha ya Kifaransa ambayo ni lugha karibu sana na Kilatini hivyo pia na lugha kama
Kiitalia
,
Kihispania
na
Kireno
.
Kifaransa kilichokuwa rasmi kilifuata lahaja ya eneo la
Paris
. Tangu 1634 kuna
Akademia ya Kifaransa
aabayo ni taasisi ya kulinda usafi wa lugha.
Kifaransa kilienea kimataifa kwa sababu Ufaransa ilikuwa taifa lenye maendeleo mengi katika Ualya. Kifaransa kilikuwa katika nchi nyingi lugha ya elimu na pia ya mawasiliano ya kimataifa jinsi ilivyo siku hizi Kiiingereza mahali pengi.
Baada ya Ufaransa kuwa nchi yenye
koloni
lugha ilisambazwa hata nje ya Ulaya. Ubelgiji yenye Kifaransa kama lugha rasmi ilikuwa pia na koloni na kupeleka lugha huko.
Kifaransa ni
lugha ya kitaifa
,
lugha rasmi
,
lugha ya utawala
au
lugha ya mawasiliano
katika nchi zifuatazo:
- Lugha ya kitaifa pamoja na lugha nyingine
- Uswisi
(lugha rasmi hasa katika mikoa ya magharibi)
- Ubelgiji
(lugha rasmi hasa katika jimbo la
Wallonia
)
- Luxemburg
- Italia
katika mkoa wa
Val d'Aoste
Lugha rasmi ya nchi zifuatazo
- Mauritania
- Djibouti
- Lugha ya elimu na mawasiliano, lakini wala lugha ya kitaifa wala lugha rasmi katika
- Algeria
- Moroko
- Tunisia
.
- Lugha rasmi ya
Haiti
- Lugha ya utawala katika
Jamhuri ya Dominika
- Moja ya lugha mbili za kitaifa katika
Kanada
; ni lugha rasmi ya pekee katika jimbo la
Quebec
(13% ya Wakanada wote hujua Kifaransa pekee, 18% wanajua lugha zote mbili)