Gaius Julius Caesar
(tamka
gayus yulius kaesar
[1]
-
100
-
44 KK
) alikuwa kiongozi wa ki
siasa
na wa ki
jeshi
wa
Roma ya Kale
.
Anakumbukwa hasa kwa mafanikio mbalimbali yanayoonekana kuathiri
dunia
hadi leo.
Baadhi ya mafanikio hayo ni:
- Waroma wa Kale walimheshimu kushinda viongozi wote waliomfuata au kutangulia akatangazwa kuwa
mungu
.
Jina
lake lilipata kuwa neno kwa ajili ya
cheo
cha watawala wa Kiroma waliomfuata. Kutokana na badiliko hilo la jina "Caesar" kuwa cheo, lugha mbalimbali zilipokea cheo hicho kama vile
Kijerumani
("Kaiser"),
Kirusi
("
Tsar
") na
Kiswahili
("
Kaisari
" - kutokana na neno la Kijerumani).
Alizaliwa katika
familia
ya ma
kabaila
wenye nafasi katika
Senatus
ilivyoitwa
bunge
la Roma. Aliingia katika siasa, akachaguliwa kwa vyeo mbalimbali kwa vipindi vya kawaida wa miezi kadhaa hadi
mwaka
moja.
Cheo chake muhimu cha kwanza kilikuwa mkuu wa
koloni
la Kiroma la
Hispania
. Alifaulu kushinda
ghasia
ya Wahispania wenyeji waliojaribu kuwafukuza Waroma kutoka nchini mwao. Caesar aliporudi Roma alitajirika na kujipatia sifa kama kiongozi wa kijeshi pia mwanasiasa aliyeokoa koloni muhimu la Hispania.
Baadaye Caesar alijiunga na wanasiasa wawili wengine: Gnaeus
Pompeius
Magnus aliyekuwa mkuu wa
wanajeshi
na Marcus Licinius
Crassus
aliyekuwa
tajiri
kushinda Waroma wote. Wote watatu waliunda umoja ulioitwa "triumviratus", yaani umoja wa
wanaume
watatu, wakashika
mamlaka
katika
dola
. Caesar alichaguliwa kwa cheo kikuu yaani
Konsul
kwa mwaka
59 KK
. Baada ya mwisho wa kipindi chake alijipatia cheo cha
Prokonsul
au
gavana
wa eneo la Gallia ya Kiroma (
Italia ya Kaskazini
na eneo dogo la
Ufaransa ya Kusini
).
Alitumia nafasi hii kuanzisha
vita
dhidi ya ma
kabila
ya Gallia huru yaani eneo lote la Ufaransa,
Uswisi
na
Ubelgiji
ya leo. Katika miaka minane ya
58
-
51 KK
alitwaa Gallia yote. Aliingia pia ndani ya
Germania
(
Ujerumani
) na kuvuka
bahari
aliposhambulia upande wa kusini wa
Britannia
. Aliandika
kitabu
cha "De bello gallico" (yaani Vita ya Gallia) akieleza mapigano yake. Kitabu hicho kina
habari
muhimu za kihistoria juu ya
utamaduni
wa makabila ya Gallia, Germania na Britannia aliyopigana nayo.
Baada ya kufanikiwa Gallia na kujenga jeshi kubwa tena hodari, wanasiasa wengine huko Roma walianza kumwogopa wakajaribu kumzuia asirudi
Italia
. Mwenzake Crassus alikuwa amekufa tayari vitani mashariki mwa dola; mwenzake Pompeius aliomwogopa Caesar akajaribu kushawishi viongozi wengine kumsimamisha.
Lakini mwaka
49 KK
Caesar aliongoza wanajeshi lake warudi Italia. Pompeius na wapinzani wake walitoka Roma wakaenda
Ugiriki
iliyokuwa jimbo la Kiroma. Mwaka
48 KK
Caesar akachaguliwa tena kuwa Konsul. Akamfuata Pompeius kwa jeshi lake akamshinda katika mapigano. Pompeius alikimbia kwenda
Misri
lakini
mfalme
Ptolemaio XIII
alimwogopa Caesar akamwua Pompeius akampatia Caesar
kichwa
chake alipofika Misri. Caesar alikutana na dada yake Ptolemaio
Kleopatra
akampenda na kuzaliana naye
mwana
wake pekee. Akamsaidia Kleopatra kuwa
malkia
na
mtawala
wa Misri.
Caesar alirudi Roma kutoka Misri akiwa
mshindi
dhidi ya wapinzani wote. Bunge la Senatus lilimpa cheo na
madaraka
ya
dikteta
kwa miaka 10. Baada ya
ushindi
mwingine dhidi ya wapinzani huko Hispania bunge lilibadilisha
azimio
hilo kumpa cheo cha
dikteta
wa
maisha
. Caesar alipokea azimio hili.
Sasa sehemu ya wabunge waliogopa ya kwamba nia yake ilikuwa kuwa mfalme wa Roma - jambo lililokuwa
marufuku
katika
jamhuri ya Roma
. Kikundi cha wabunge -wote makabaila wa familia za kale- kiliunga mikono wakamwua Caesar bungeni tarehe
15 Machi
44 KK
kwa kumdunga
kisu
mara 23. Caesar anasemekana alimtambua
mpwa
wake Brutus akamwuliza kwa maneno yake ya mwisho: "Hata wewe mwanangu?"
Caesar hakuwa na watoto ila huyu mwana wa Kleopatra asiyekuwa Mroma. Kabla ya
kifo
chake alikuwa amempanga mtoto mpwa wake Oktaviano. Huyu Oktaviano -aliyejulikana baadaye kama
Augusto
na mtawala wa kwanza wa Dola la Roma- alilipiza
kisasi
chake katika kipindi cha
vita ya wenyewe kwa wenyewe
na kuua wapinzani wote wa Caesar.
Miaka miwili baada ya kifo chake bunge lilimtangaza Caesar kuwa mungu.
- ↑
Kwa matamshi ya Kilatini sanifu cha Kale herufi "C" ilikuwa na matamshi ya "K"; katika matamshi ya karne za baadaye ilikuwa zaidi "Ch" kwa hiyo "Chesar"; kutoka hapo yametokea matamshi ya Kiingereza "Sizar"