Kalenda ya Juliasi
ni
kalenda
iliyoanzishwa katika
Dola la Roma
kwa
amri
ya
Julius Caesar
mnamo
mwaka
46
KK
Ilichukua nafasi ya
kalenda ya Kirumi
iliyotangulia.
Kalenda ya Juliasi ilibadilishwa na
kalenda ya Gregori
kuanzia
karne ya 16
BK
lakini ilikuwa kalenda rasmi katika nchi mbalimbali kama
Urusi
hadi
karne ya 20
. Mpaka leo ni kalenda ya
liturgia
katika
Kanisa la Kiorthodoksi
.
Juliasi Kaisari alikuwa
mtawala
wa Kirumi aliyeamua kubadilisha kalenda ya kale iliyokuwa ya aina ya
kalenda ya mwezi
.
Majira
yalikosa
tarehe
kamili katika kalenda hiyo, hali iliyosababisha matatizo ya kiutawala, hasa kwa sababu tarehe ya malipo ya
kodi
ilitakiwa kuwa baada ya
mavuno
, wakati
wakulima
walipokuwa na uwezo wa kulipa.
Hivyo Caesar alimwajiri
mtaalamu
M
misri
Sosigenes
atunge kalenda mpya inayofuata mzunguko wa
jua
. Kalenda hiyo iliitwa kwa
heshima
yake Kalenda ya Juliasi. Ilikuwa na
miezi
12 yenye
siku
30 au 31 isipokuwa mmoja mfupi wenye siku 28 ambao ni mwezi wa
Februari
ili kukamilisha siku 365 za mzunguko wa kandokando ya jua. Vipindi hivyo viliendela kuitwa "mwezi/miezi" ingawa havikufuata tena mwendo wa mwezi wenyewe. Kwa sababu muda wa
mwaka wa jua
ulijulikana kuwa na siku 365 1/4, kila mwaka wa nne siku ya nyongeza iliingizwa kama siku ya 29 ya mwezi wa
Februari
.
Mwaka 46 KK wenyewe ulirefushwa kwa ajili ya sahihisho lile ukawa na siku 445 ambao
Warumi
waliukumbuka kama "mwaka uliochanganyikiwa".
Sosigenes alitumia
majina
ya miezi ya kalenda ya kale yanayoendela kutumika hadi leo. Isipokuwa mwaka
44 KK
baada ya
kifo
cha Caesar mwezi wa "Quintilis" ulipewa jina la
marehemu
ukaitwa "Julius" ndiyo
Julai
kwa
Kiswahili
. Mtawala mkubwa aliyefuata baada ya Julius Caesar alikuwa
Augusto
(anayehesabiwa kuwa
Kaisari
wa kwanza wa Kirumi) na mwezi wa Sextilis ulipewa jina kwa heshima yake: ni mwezi wa
Agosti
kwa
Kiswahili
. Hata watawala wengine walijaribu kupachika majina yao kwenye mwezi fulani lakini ni majina ya Kaisari Juliusi na Augusto pekee yaliyodumu.
Miezi ya Septemba hadi Desemba inatunza kumbukumbu ya kwamba ilikuwa miezi ya saba hadi kumi katika kalenda ya kale ya kirumi.
Jina la mwezi - Nambari ya
Kilatini
Septemba
- septem (7)
Oktoba
- octo (8)
Novemba
- novem (9)
Desemba
- decem (10)
Lakini hapakuwa na mapatano kuhusu mwanzo wa mwaka ni mwezi gani. Maeneo mbalimbali yalitumia mwanzo tofauti. Ni tangu
karne ya 13
BK
tu kwamba
1 Januari
ilianza kukubaliwa polepole kuwa mwanzo wa mwaka katika nchi za
Ulaya
.
Kalenda ya Juliasi ilikuwa na kasoro ambayo haikujulikana mwanzoni. Muda kamili wa mwaka wa jua si siku 365 1/4. Hivyo mwaka wa kalenda ya Juliasi ulipita muda kamili ya mwaka wa jua kwa
dakika
11 na
sekunde
14.
Hadi
karne ya 14
BK
tofauti hiyo ilikuwa imefikia tayari jumla ya siku 7. Hayo yalionekana hasa wakati wa
Pasaka
ambayo haikufuata tena utaratibu uliowekwa na
Mtaguso wa kwanza wa Nisea
.
Kwa sababu hiyo
Mtaguso wa Trento
wa
Kanisa Katoliki
uliamua kusahihisha kalenda. Ni
Papa Gregori XIII
aliyeita
wataalamu
waliofanya makadirio mapya.
Tangu mwaka
1582
kalenda ya Gregori
ilipoanzishwa ikawa leo kalenda ya kimataifa.