Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(au
Kongo-Kinshasa
) ni nchi iliyoko
Afrika ya Kati
; kwa ukubwa wa eneo ni ya pili
barani
Afrika
. Ni tofauti na nchi jirani ya
Jamhuri ya Kongo
.
Jiografia
Nchi imepakana na
Jamhuri ya Kongo
,
Jamhuri ya Afrika ya Kati
,
Sudan Kusini
,
Uganda
,
Rwanda
,
Burundi
,
Tanzania
,
Zambia
na
Angola
.
Ina sehemu ndogo ya pwani kwenye
Bahari ya Atlantiki
. Sehemu hiyo inatenganisha eneo la
Cabinda
kutoka maeneo mengine ya
Jamhuri
ya
Angola
.
Eneo lote ni la
kilometa mraba
2,345,409 na linafanya Kongo iwe nchi ya 11 duniani kwa ukubwa wa eneo.
Historia
Historia ya kale
Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa
wawindaji
wa jamii ya
Wasani
na ya
Wabilikimo
.
Katika
karne
za
BK
walifika wahamiaji
Wabantu
wenye
ujuzi
wa
kilimo
na
uhunzi
.
Jina la Kongo lahusiana na
mto Kongo
unaopitia nchi yote.
Mnamo
karne ya 15
, wakati
wapelelezi
wa kwanza
Wareno
walipofika kwenye pwani za Afrika,
milki
kubwa katika nchi ya Kongo ya magharibi pamoja na
Angola
ya kaskazini ilikuwa
Ufalme wa Kongo
. Wakati wa uenezaji mkuu ufalme huu ulianza kwenye
mwambao
wa Atlantiki na kuendelea hadi
mto Kwango
kwenye mashariki, halafu maeneo kutoka
Pointe-Noire
(leo:
Jamhuri ya Kongo
, upande wa kaskazini ya
Cabinda
) upande wa kaskazini hadi
mto Loje
(leo: mji wa
Ambriz
) katika kusini.
Mtawala alikuwa na
cheo
cha
Manikongo
na ufalme uligawiwa kwa majimbo sita. Baada ya kufika kwa Wareno wafalme na matabaka ya juu walikuwa
Wakristo
. Ufalme uliporomoka kutokana na vita vilivyosababishwa na
biashara ya watumwa
na kuingilia kwa
wafanyabiashara
ya
watumwa
katika
siasa
ya ndani. Hata hivyo,
nasaba
za watawala waliotumia cheo cha "Awenekongo" waliendelea kukaa katika
mji mkuu
wa kale M'banza-Kongo (iliyobadilishwa jina kuitwa San Salvador) hadi mwaka
1914
ambako Wareno walifuta mabaki ya
uhuru
na kufanya eneo lililobaki sehemu kamili ya koloni lao la Angola.
Upande wa
kusini
, kuanzia
karne ya 17
, kulikuwa na
ufalme
ulioitwa
Dola la Kazembe
.
Koloni binafsi la mfalme kuwa koloni la Ubelgiji
Nchi jinsi ilivyo ilianzishwa kama
Dola huru la Kongo
likiwa
mali
binafsi ya
mfalme
Leopold II wa Ubelgiji
.
Historia
yake ni ya
aibu
na ya
ukatili
kupindukia.
Utawala wa mfalme ulionekana kuwa wa kinyama na upinzani dhidi yake ulikua katika nchi nyingi za dunia.
Hatimaye alipaswa kukabidhi koloni lake binafsi mikononi mwa serikali ya Ubelgiji iliyomlipa
fidia
kwa mali aliyoacha.
Kati ya mwaka
1908
hadi
1960
ilikuwa
koloni
la
Ubelgiji
kwa jina la
Kongo ya Kibelgiji
baada ya kuhamishiwa mikononi mwa
serikali
ya Ubelgiji.
Katika miaka
1925
hadi
1946
maeneo ya
Rwanda
na
Burundi
yalitawaliwa kama sehemu za Kongo ya Kibelgiji.
Siasa ya wakoloni
Wabelgiji walijitahidi kuboresha hali ya maisha ya wenyeji baada ya miaka mibaya ya Leopold II. Nia ilichelewa kuonekana hali halisi kwa sababu utaratibu wa kulazimisha Waafrika kufanyia kazi kampuni na shirika kubwa iliendelea hata bila
idhini
ya serikali mpya ukadai vifo vingi.
Kwenye uwanja wa
elimu
,
matibabu
na
mawasiliano
jitihada
za siasa mpya zilionekana zaidi. Kongo ilikuwa kati ya nchi chache ambako lugha za kienyeji zilifundishwa
shuleni
kwa sababu shule nyingi ziliendshwa na
wamisionari
.
Kwa upande mwingine
ubaguzi wa rangi
uliwaruhusu Waafrika wachache sana kufikia ngazi za juu za elimu.
Makampuni makubwa ya
migodi
kama vile "Societe Generale" na "Union Miniere du Haut Katanga" yalichimba
madini
hasa katika jimbo la
Katanga
. Makampuni haya yalikuwa na athira kubwa.
Katanga ilikuwa maarufu kwa
shaba
iliyochimbwa huko. halafu pia kwa
uranium
iliyotumiwa kwa
mabomu ya kwanza ya kinyuklia
ya
Marekani
mwaka
1945
.
Upinzani
Baada ya
unyama
wa miaka ya Leopold II upinzani dhidi ya utawala wa kikoloni ulikuwa hafifu. Kuanzia
miaka ya 1920
Wakongo wengi walionyesha upinzani huo katika mahudhurio katika madhehebu mapya ya wafuasi wa
Simon Kimbangu
yaliyopigwa marufuku na Wabelgiji kuanzia mwaka
1926
.
Tangu mwaka
1950
upinzani uliongezeka na kuonyesha pia uso wa kisiasa.
Wabelgiji ambao hawakujiandaa kwa madai hayo yalipaswa kukubali
uchaguzi
wa halmashauri za vijiji na miji mwaka
1957
.
Mwaka
1958
vyama vya kisiasa vilikubaliwa.
Harakati
mbili muhimu kati ya hivi zilikuwa Abako (Alliance de Bakongo) chini ya
Joseph Kasavubu
na MNC (Mouvement National Congolais) chini ya
Patrice Lumumba
.
Mwaka
1959
mkutano wa wanasiasa Wakongo ulidai
uhuru
wa nchi.
Mwisho wa koloni na uhuru
Wabelgiji walijaribu kuchelewesha harakati hizo lakini baada ya kutambua matatizo serikali ya Ubelgiji ilitangaza mnamo Januari
1960
kuwa uchaguzi utaendeshwa haraka na baada ya miezi sita Wabelgiji watakabidhi nchi kwa wenyeji.
Chama
cha Patrice Lumumba kilishinda kwa
kura
nyingi naye akawa kiongozi wa kwanza wa nchi huru kama
waziri mkuu
.
Koloni la
Kongo ya Kibelgiji
lilipata
uhuru
tarehe
30 Juni
1960
.
Kati ya
27 Oktoba
1971
na
17 Mei
1997
, chini ya utawala wa
dikteta
Mobutu
, nchi ilijulikana kwa jina la "
Zaire
".
Leo hii ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mikoa
Nchi imegawiwa katika mikoa 26 kadiri ya
Katiba
mpya (
2006
) na utekelezaji wake wa mwaka
2015
.
Watu
Mwaka
2017
wakazi walikuwa 81,339,988:
idadi
hiyo ni ya 4 kati ya nchi zote za Afrika, baada ya
Nigeria
,
Ethiopia
na
Misri
.
Wakazi asilia ni
Wabilikimo
, ambao kwa sasa ni 600,000. Kumbe walio wengi ni
Wabantu
.
Lugha
Kifaransa
ni
lugha rasmi
ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ilikuwa lugha ya utawala ya koloni ikaendelea kutumiwa kama lugha isiyoelekea upande wowote kati ya ma
kabila
,
lugha
na
tamaduni
za nchi hii.
Lugha ya
Kiholanzi
iliyotumiwa na Wabelgiji pamoja na Kifaransa katika utawala haitumiki tena.
Kwa jumla kuna takriban lugha 242, hasa
lugha za Kibantu
, zinazozungumzwa nchini (angalia
orodha ya lugha
). Kati yake, lugha 4 zinatambuliwa kama
lugha za kitaifa
, nazo ni:
Kikongo
(
Kituba
),
Kingala (Kongo)
,
Kiluba
(
Tshiluba
) na
Kiswahili
. Wakati wa ukoloni lugha hizo nne za kitaifa ziliwahi kutumiwa kieneo katika
shule za msingi
.
Kingala
kilikuwa lugha rasmi ya
jeshi
la kikoloni lililoitwa "
Force Publique
" chini ya utawala wa Ubelgiji likaendelea kuwa lugha ya jeshi la jamhuri baada ya
uhuru
.
Tangu
mapinduzi
ya
1997
sehemu za jeshi, hasa
mashariki
, hutumia pia Kiswahili.
Takriban 47% wanatumia Kifaransa kama
lugha ya kwanza
au
lugha ya pili
.
Dini
Wananchi wengi (zaidi ya 90%) wanajihesabu
Wakristo
wa
madhehebu
mbalimbali; kati yao asilimia 29.7 ni
Wakatoliki
.
Waislamu
ni asilimia 10-12. Wafuasi wa
dini asilia za Kiafrika
ni 3%.
Tazama pia
Marejeo
- Clark, John F.,
The African Stakes of the Congo War
, 2004.
- Devlin, Larry
(2007).
Chief of Station, Congo: A Memoir of 1960?67
. New York: PublicAffairs.
ISBN
978-1-58648-405-7
.
.
- Drummond, Bill and Manning, Mark,
The Wild Highway
, 2005.
- Edgerton, Robert,
The Troubled Heart of Africa: A History of the Congo.
St. Martin's Press, December 2002.
- Exenberger, Andreas/Hartmann, Simon.
The Dark Side of Globalization. The Vicious Cycle of Exploitation from World Market Integration: Lesson from the Congo
, Working Papers in Economics and Statistics 31, University Innsbruck 2007.
- Exenberger, Andreas/Hartmann, Simon.
Doomed to Disaster? Long-term Trajectories of Exploitation in the Congo
Archived
1 Septemba 2011 at the
Wayback Machine
., Paper to be presented at the Workshop "Colonial Extraction in the Netherlands Indies and Belgian Congo: Institutions, Institutional Change and Long Term Consequences", Utrecht 3?4 December 2010.
- Gondola, Ch. Didier, "The History of Congo", Westport: Greenwood Press, 2002.
- Joris, Lieve, translated by Waters, Liz,
The Rebels' Hour
, Atlantic, 2008.
- Justenhoven, Heinz-Gerhard; Ehrhart, Hans Georg. Intervention im Kongo: eine kritische Analyse der Befriedungspolitik von UN und EU. Stuttgart: Kohlhammer, 2008. (In German)
ISBN 978-3-17-020781-3
.
- Kingsolver, Barbara
.
The Poisonwood Bible
HarperCollins, 1998.
- Laremont, Ricardo Rene, ed. 2005.
Borders, nationalism and the African state
. Boulder, Colorado and London: Lynne Rienner Publishers.
- Lemarchand, Reni and Hamilton, Lee;
Burundi: Ethnic Conflict and Genocide.
Woodrow Wilson Center Press, 1994.
- Mealer, Bryan: "All Things Must Fight To Live", 2008.
ISBN 1-59691-345-2
.
- Melvern, Linda
,
Conspiracy to Murder: The Rwandan Genocide and the International Community
. Verso, 2004.
- Miller, Eric: "The Inability of Peacekeeping to Address the Security Dilemma", 2010.
ISBN 978-3-8383-4027-2
.
- Mwakikagile, Godfrey,
Nyerere and Africa: End of an Era
, Third Edition, New Africa Press, 2006, "Chapter Six: Congo in The Sixties: The Bleeding Heart of Africa", pp. 147 ? 205,
ISBN 978-0-9802534-1-2
; Mwakikagile, Godfrey,
Africa and America in The Sixties: A Decade That Changed The Nation and The Destiny of A Continent
, First Edition, New Africa Press, 2006,
ISBN 978-0-9802534-2-9
.
- Nzongola-Ntalaja, Georges,
The Congo from Leopold to Kabila: A People's History
, 2002.
- O'Hanlon, Redmond,
Congo Journey
, 1996.
- O'Hanlon, Redmond,
No Mercy: A Journey into the Heart of the Congo
, 1998.
- Prunier, Gerard,
Africa's World War: Congo, the Rwandan Genocide, and the Making of a Continental Catastrophe
, 2011 (also published as
From Genocide to Continental War: The Congolese Conflict and the Crisis of Contemporary Africa: The Congo Conflict and the Crisis of Contemporary Africa
).
- Renton, David; Seddon, David; Zeilig, Leo.
The Congo: Plunder and Resistance
, 2007.
ISBN 978-1-84277-485-4
.
- Reyntjens, Filip,
The Great African War: Congo and Regional Geopolitics, 1996?2006
, 2009.
- Rorison, Sean,
Bradt Travel Guide: Congo ? Democratic Republic/Republic
, 2008.
- Schulz, Manfred.
Entwicklungstrager in der DR Kongo: Entwicklungen in Politik, Wirtschaft, Religion, Zivilgesellschaft und Kultur
, Berlin: Lit, 2008, (in German)
ISBN 978-3-8258-0425-1
.
- Stearns, Jason:
Dancing in the Glory of Monsters: the Collapse of the Congo and the Great War of Africa
, Public Affairs, 2011.
- Tayler, Jeffrey,
Facing the Congo
, 2001.
- Turner, Thomas,
The Congo Wars: Conflict, Myth and Reality
, 2007.
- Van Reybrouck
, David,
Congo: The Epic History of a People
, 2014
- Wrong, Michela,
In the Footsteps of Mr. Kurtz: Living on the Brink of Disaster in Mobutu's Congo
.
- Osman, Mohamed Omer Guudle(November,2011) Africa: A rich Continent where poorest people live, The Case of DR Congo and the exploitation of the World Market
Viungo vya nje
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|