Jakaya Mrisho Kikwete
alikuwa
rais
wa nne wa
Jamhuri
ya Muungano wa
Tanzania
tangu tarehe
21 Desemba
2005
hadi tarehe
5 Novemba
2015
.
Asili
Amezaliwa
7 Oktoba
1950
katika
kijiji
cha Msoga,
kata
ya
Lugoba
,
tarafa
ya Msoga,
jimbo la uchaguzi
la
Chalinze
,
Wilaya ya Bagamoyo
,
mkoa wa Pwani
.
Lugha ya mama
ilikuwa
Kikwere
.
Alizaliwa katika
familia
ya
wanasiasa
.
Babu
yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa
chifu
wa
Wakwere
. Baba yake alikuwa
Mkuu wa Wilaya
Pangani
,
Same
na
Tanga
.
Jakaya Kikwete amesimulia
hadithi
ya kifamilia ya kuwa wakati
mama
yake alipokuwa
mja mzito
naye, babu alitamka kuwa ikiwa
mtoto
atakuwa wa kiume atampatia
urithi
wa
cheo
chake.
Masomo
Miaka
1958
?
1961
akasoma
Shule ya Msingi
Msoga, halafu
1962
?
1965
Shule ya Kati
(Middle School) Lusonga, halafu
Shule ya Sekondari
Kibaha
akiongeza A-level huko Shule ya Sekondari
Tanga
.
Kuanzia mwaka
1972
alisoma
uchumi
katika
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
akimaliza kwa kupata
digrii
yake mwaka
1978
.
Akajiunga na
Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ).
Jakaya aliposoma
Shule ya Sekondari ya Kibaha
alikuwa
mwenyekiti
wa
wanafunzi
na pia wa
Vijana
wa
TANU
. Katika
Shule ya Sekondari Tanga
alikuwa
Kiranja Mkuu
na pia
kiongozi
wa
timu
ya
mpira
. Katika
UDS
alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa
halmashauri
ya wanafunzi.
Kupanda ngazi katika siasa
1mwaka huu alikuwa mkulima wa Msoga. Mwaka
1988
akateuliwa kuwa
mbunge
na
waziri msaidizi
. Mwaka
1990
alichaguliwa kuwa mbunge wa Bagamoyo/
Chalinze
akirudishwa kila
uchaguzi
hadi mwaka
2000
. Akawa
waziri
akipita katika
wizara
za
maji
na
fedha
.
Mwaka
1995
alijaribu kuchaguliwa kuwa
mgombea
wa
urais
upande wa
CCM
. Inasemekana ya kwamba
Mwalimu
Julius Nyerere
alimwomba wakati ule kumwachia nafasi
Benjamin Mkapa
aliyeteuliwa na
Halmashauri Kuu ya CCM
. Kikwete akawa
Waziri wa Mambo ya Nje
katika
serikali
zote mbili za Mkapa.
Mwaka
2005
alifaulu kuteuliwa mgombea wa CCM kwa nafasi ya rais akashinda uchaguzi wa Desemba 2005 akizoa 80% za
kura
zote.
Miaka kumi ya urais
Katika
uchaguzi mkuu
wa mwaka
2010
alitangazwa tena mshindi ingawa kwa
asilimia
ndogo zaidi na kwa wasiwasi kuhusu uwezekano wa matokeo kuchakachuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi aliyoiteua mwenyewe. Katiba ya nchi hairuhusu kukata
rufaa
dhidi ya tangazo la tume hiyo.
Kuapishwa kwa mara ya kwanza kwa Jakaya Kikwete kama
Rais
wa 4 wa Tanzania kulifanyika Jumatano, tarehe 21 Desemba
2005
. Ilikuwa ni mwanzo wa muhula wa kwanza wa miaka mitano wa Jakaya Kikwete kama Rais na Ali Mohamed Shein kama Makamu wa Rais.
Katika miaka mitano iliyofuata, rais aliendelea kusafiri sana nje ya nchi, kiasi kwamba alikaa ughaibuni siku nyingi kuliko zile alizokaa nchini Tanzania.
Hali ya mwisho ya nchi ilifananishwa na
mwandamizi
wake
John Magufuli
kuwa kama "shamba la bibi", ambamo kila mtu anaweza kuchuma anavyotaka. Pia rais mpya alilalamika kwa kukuta
hazina
haina
fedha
, mbali na
madeni
ya kimataifa kufikia kiasi cha karibu
Shilingi za Tanzania
milioni
1 kwa kila mwananchi.
Heshima na Tuzo
Nishani
Nishani
|
Nchi
|
Tarehe
|
Ref
|
|
Nishani Ubora wa Lulu ya Afrika (Bwana tukufu)
|
Uganda
|
Julai 2007
|
[1]
|
|
Nishani ya Hilali Kijani ya Komori
|
Komori
|
Machi 2009
|
[2]
|
|
Nishani ya Abdulaziz Al Saud
|
Saudi Arabia
|
Aprili 2009
|
[3]
|
|
Nishani ya Ubora
|
Jamaika
|
Novemba 2009
|
[4]
|
|
Nishani ya Oman (Daraja la Kwanza)
|
Omani
|
Oktoba 2012
|
[5]
|
Shahada za Heshima
Marejeo
- Nyang'oro, Julius E. (2011).
JK: A Political Biography of Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania
. Trenton, NJ: Africa World Press, Inc.
ISBN
1592217753
.
Tanbihi
- ↑
"
Museveni honours Nyerere
", 10 July 2007. Retrieved on 26 Septemba 2013.
(Kiingereza)
Archived from
the original
on
2014-12-05
.
- ↑
"Rais Kikwete, Jenerali Mwamunyange, Waziri Membe Watunukiwa Anjoun"
.
Ikulu
. 25 Machi 2009. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2013-09-27
. Iliwekwa mnamo
26 Septemba
2013
.
{{
cite web
}}
: CS1 maint: date auto-translated (
link
)
- ↑
"JK akiwa Saudia"
. Michuzi Blog. 16 Aprili 2009
. Iliwekwa mnamo
26 Septemba
2013
.
{{
cite web
}}
: CS1 maint: date auto-translated (
link
)
- ↑
"
President Kikwete Awarded Order of Excellence
", 26 November 2009. Retrieved on 26 Septemba 2013.
(Kiingereza)
Archived from
the original
on
2013-09-27
.
- ↑
"
HM confers Oman Civil Order on Tanzania leader
", October 2012. Retrieved on 26 Septemba 2013.
(Kiingereza)
Archived from
the original
on
2014-12-04
.
- ↑
"President of Tanzania to speak here Sept. 28"
(kwa Kiingereza). Chuo Kikuu cha Mtakatifu Thomas (Minnesota). 25 Septemba 2006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2013-09-28
. Iliwekwa mnamo
25 Septemba
2013
.
{{
cite web
}}
: CS1 maint: date auto-translated (
link
)
- ↑
Swallehe Msuya. "
Tanzania's president touts country's progress at St. Thomas appearance
", 30 September 2006. Retrieved on 25 Septemba 2013.
(Kiingereza)
- ↑
"Kenyatta University Newsletter Vol. 4, Issue 15 (Special Graduation Edition)"
(PDF)
(kwa Kiingereza). Chuo Kikuu cha Kenyatta. 26 Januari 2009. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
(
PDF
)
mnamo 2017-04-21
. Iliwekwa mnamo
25 Septemba
2013
.
{{
cite web
}}
: CS1 maint: date auto-translated (
link
)
- ↑
(in Kiingereza)
Honorary Doctorate to the president of Tanzania from our university
(Press release).
Turkey
: Chuo Kikuu cha Fatih. 19 February 2010. Archived from
the original
on 2012-12-24
.
https://web.archive.org/web/20121224011640/http://fatih.edu.tr/?basin_bultenleri%2C12&language=EN
. Retrieved 25 Septemba 2013
.
- ↑
"MUHAS Annual Report 2010-2011"
(kwa Kiingereza). Chuo Kikuu cha Muhimbili. 2011. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
(
PDF
)
mnamo 2013-09-30
. Iliwekwa mnamo
25 Septemba
2013
.
- ↑
"
JK, late Kawawa honoured at UDOM colourful, maiden graduation
", 27 November 2010. Retrieved on 25 Septemba 2013.
(Kiingereza)
- ↑
"JK atunukiwa udaktari wa sheria UDSM"
(kwa Kiingereza). Michuzi Blog. 21 Ocotober 2011
. Iliwekwa mnamo
25 Septemba
2013
.
;
- ↑
(in Kiingereza)
U of G to Welcome Tanzanian President to Campus
(Press release).
Guelph
, Canada: Chuo Kikuu cha Guelph. 18 September 2013
.
http://www.uoguelph.ca/news/2013/09/u_of_g_to_welcome_tanzanian_president.html
. Retrieved 25 Septemba 2013
.
- ↑
President of Tanzania at War Memorial Hall
katika
YouTube
- ↑
"Rais Mstaafu Jakaya Kikwete atunukiwa shahada ya udaktari ya uhusiano wa kimataifa"
. 21 Januari 2016
. Iliwekwa mnamo
1 Agosti
2020
.
Viungo vya nje
Wikimedia Commons ina media kuhusu: