Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Akida Korneli
(kwa
Kigiriki
,
Κορν?λιο?
, Kornelios) alikuwa
akida
wa
kikosi
cha
Italia
katika
jeshi
la
Dola la Roma
aliyefanya kazi huko
Kaisarea Baharini
(
Palestina
). Huko alivutiwa na
dini
ya
Uyahudi
hata akajitolea kujenga
sinagogi
, pamoja na kusali.
Wongofu
wake na wa
jamaa
zake unasimuliwa mara tatu na
Matendo ya Mitume
kwa jinsi ulivyotiwa maanani na
Luka mwinjili
aliyetaka kueleza kwamba
desturi
ya
kubatiza
watu wa mataifa bila kudai kwanza
watahiriwe
ilianzisha na
Mtume Petro
kwa kuangazwa na
Mungu
.
Suala hilo lilisumbua sana
Kanisa
la mwanzo hata baada ya
Mtaguso wa Yerusalemu
(
49
BK
) kupitisha desturi hiyo (
Mdo
15).
Baada ya kuongoka, inasimuliwa kwamba alishuhudia
Injili
hadi
Misia
(leo nchini
Uturuki
) akateswa kwa ajili hiyo.
Habari nyingine zinasema alipata kuwa
askofu
na nyingine
alifia dini
.
Tangu kale anaheshimiwa na
Wakatoliki
na
Waorthodoksi
kama
mtakatifu
.
Sikukuu
yake huadhimishwa
tarehe
20 Oktoba
[1]
[2]
lakini pia
13 Septemba
au
2 Februari
.
|
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Akida Korneli
kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|