Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Matthew Olusegun Aremu Obasanjo
(alizaliwa
5 Machi
1937
) ni
jenerali
mstaafu wa
Jeshi
la Nigeria aliyepata kuwa
rais
wa
Nigeria
mara mbili. Awamu yake ya kwanza ilikuwa kama rais wa kijeshi kati ya miaka
1976
na
1979
, halafu awamu ya pili kama rais aliyechaguliwa na wananchi kati ya miaka
1999
na
2007
.
Obasanjo alizaliwa katika
kabila
la
Wayoruba
akalelewa kama
Mkristo
wa
Kibaptisti
.
Mwaka
1958
akajiunga na jeshi akapanda ngazi haraka. Miaka 1967-1970 alishiriki katika
vita
dhidi ya
Biafra
. Baada ya
uasi
wa jeshi chini ya
Murtala Mohammed
mwaka 1975 alipewa cheo cha makamu wa rais. Mwaka 1976 Mohammed aliuawa na wapinzani ndani ya jeshi waliokosa kumwua Obasanjo pia. Obansajo aliweza kukandamiza uasi akateuliwa na halmashauri ya kijeshi kuwa rais mpya. Alitumia nafasi yake kuandaa
uchaguzi
wa mwaka 1979 akakabidhi
madaraka
kwa rais aliyechaguliwa,
Shehu Shagari
.
Kati ya
1980
hadi
1995
alikuwa na vyeo mbalimbali vya kimataifa akagombea nafasi ya
Katibu Mkuu
wa
UM
halafu alikuwa
mwenyekiti
wa halmashari ya
Transparency International
(TI).
Dikteta
wa kijeshi
Sani Abacha
alimfunga gerezani mwaka 1995 hadi 1998.
Wakati wa uchaguzi baada ya
kifo
cha Abacha aligombea urais kwa tiketi ya chama cha People's Democratic Party akashinda akawa rais tena tangu 1999. Mwaka
2003
alirudishwa madarakani.
Obasanjo alijaribu kubadilisha
katiba
ili aweze kuwa na nafasi ya tatu lakini hakufaulu kupata
wabunge
wa kutosha kwa kubadilisha katiba.
Katika uchaguzi wa mwaka 2007 alisimama upande wa mgombea
Umaru Yar'Adua
aliyechaguliwa. Kumkabidhi madaraka kulikuwa mara ya kwanza katika
historia ya Nigeria
ya kwamba marais wawili waliochaguliwa na wananchi waliweza kufuatana.
Mnamo Agosti
2021
,
Umoja wa Afrika
ilimteua Olusegun Obasanjo kama
Mwakilishi
Mkuu wa
Amani
katika
Pembe ya Afrika
[1]
.
|
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Olusegun Obasanjo
kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|
- ↑
AU names Obasanjo High Representative for Horn of Africa
, East African 27.08.2021, iliangaliwa Agosti 2021