Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
(
Butiama
,
Mkoa wa Mara
, pembezoni mwa
Ziwa Nyanza
,
13 Aprili
1922
-
London
,
Uingereza
,
14 Oktoba
1999
) alikuwa
rais
wa kwanza wa
Tanzania
, na mara nyingi anatajwa kama "Baba wa Taifa" kwa jinsi alivyoathiri nchi hiyo.
Ndiye mwasisi wa
itikadi
ya
ujamaa
na kujitegemea iliyotangazwa hasa katika
Azimio la Arusha
.
Kabla ya kuingia kwenye
siasa
alikuwa ni
mwalimu
.
Kazi
hiyo ndiyo iliyompatia jina ambalo lilimkaa maisha yake yote la "Mwalimu."
Kwanza aliongoza
Tanganyika
toka mwaka
1961
hadi
1964
kama
waziri mkuu
, halafu kama rais; baada ya
muungano
wa
Tanganyika
na
Zanzibar
, aliongoza Tanzania kuanzia mwaka
1964
hadi mwaka
1985
kama rais.
Mwalimu Nyerere ni kati ya viongozi wachache wa
Afrika
ambao wameacha
madaraka
kwa
hiari
baada ya kutawala kwa muda mrefu, akiwa bado anapendwa na wananchi walio wengi katika
nchi
.
Alipostaafu urais mwaka
1985
alirudi
kijijini
kwake Butiama ambako aliendesha shughuli za
kilimo
. Hata hivyo aliendelea kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.
Kwa ruhusa ya
makao makuu
ya
Kanisa Katoliki
duniani,
Jimbo Katoliki la Musoma
lilianza kushughulikia
kesi
ya kumtangaza
mwenye heri
na hatimaye
mtakatifu
. Kwa sababu hiyo anaitwa pia "
mtumishi wa Mungu
". Baada ya hapo
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
limepokea
jukumu
la kuratibu mchakato huo pamoja na kesi kuhamishiwa
Jimbo Kuu la Dar es Salaam
kutokana na Nyerere kuishi muda mrefu
jijini
humo
[1]
.
Maisha yake
Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka
1922
katika
kijiji
cha
Butiama
,
wilaya
ya
Musoma
,
mkoa wa Mara
, Tanzania (wakati ule:
Tanganyika
).
Alikuwa mmojawapo kati watoto 26 wa Nyerere Burito,
chifu
wa
kabila
la
Wazanaki
.
Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya
baba
yake; katika umri wa miaka 12 aliingia
shule
akitembea
kilomita
30 hadi
Musoma
.
Baada ya kumaliza
shule ya msingi
aliendelea kusomea shule ya
wamisionari
Wakatoliki
huko
Tabora
.
Katika
umri
wa miaka 20
alibatizwa
akawa
Mkristo
Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake.
Ma
padri
wakiona
akili
yake kubwa walimsaidia kusomea ualimu huko
Makerere
,
Kampala
,
Uganda
kuanzia mwaka
1943
hadi
1945
.
Akiwa Makerere alianzisha tawi la Umoja wa Wanafunzi Watanganyika, pia alijihusisha na tawi la
Tanganyika African Association
(TAA).
Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora akifundisha shule ya St.Mary.
Mwaka
1949
alipata
skolashipu
ya kwenda kusoma kwenye
Chuo Kikuu
cha
Edinburgh
,
Uskoti
,
Ufalme wa Muungano
, akapata
M.A.
ya
historia
na
uchumi
(alikuwa Mtanganyika wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na wa pili kupata
shahada
ya
elimu ya juu
nje ya Tanganyika).
Aliporejea kutoka masomoni, alifundisha Historia,
Kiingereza
na
Kiswahili
katika shule ya
St. Francis
iliyo karibu na
Dar es Salaam
.
Mwaka
1953
alichaguliwa kuwa rais wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere.
Mwaka
1954
alibadilisha jina la chama cha TAA kwenda chama cha
Tanganyika African National Union
(TANU), ambacho pia kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kikawa tayari chama cha siasa kinachoongoza nchini Tanganyika.
Uwezo wa Nyerere uliwashtua viongozi wa
kikoloni
akalazimika kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akijisemea kuwa mwalimu kwa kuchagua na
mwanasiasa
kwa
bahati
mbaya.
Alijiuzulu ualimu
[2]
na kuzunguka nchi nzima ya Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta
umoja
katika kupigania
uhuru
. Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Trusteeship Council na Fourth Committee ya
Umoja wa Mataifa
(UN) huko
New York
.
Uwezo wake wa kuongea na wa kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila
umwagaji wa damu
.
Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa
gavana
wa wakati huo,
Richard Turnbull
, ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru.
Nyerere aliingia katika
bunge
la kikoloni mwaka
1958
na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka
1960
.
Mwaka
1961
Tanganyika ilipata uhuru wake na tarehe
9 Desemba
1961 Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa
Tanganyika
huru; mwaka mmoja baadaye akawa rais wa kwanza wa
Jamhuri
ya Tanganyika.
Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania mara baada ya
mapinduzi ya Zanzibar
mwaka
1964
yaliyomtoa madarakani
sultani
wa Zanzibar
Jamshid bin Abdullah
.
Julius Nyerere akiwa mzee mnamo mwaka
1977
.
Tarehe
5 Februari
1977 aliongoza chama cha TANU kuungana na
chama tawala
cha Zanzibar
Afro Shirazi Party
na kuanzisha chama kipya cha CCM (
Chama cha Mapinduzi
) akiwa mwenyekiti wake wa kwanza.
Nyerere aliendelea kuongoza
taifa
hadi 1985 alipomwachia nafasi rais wa pili,
Ali Hassan Mwinyi
.
Aliacha kuongoza Tanzania ikiwa ni mojawapo kati ya nchi maskini zaidi duniani, ingawa yenye huduma za elimu na afya zilizoenea kwa wananchi wengi.
Hata hivyo aliendelea kuongoza CCM hadi mwaka
1990
na kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.
Kwa mfano, inasadikika kuwa Nyerere alishawishi uteuzi wa
Benjamin W. Mkapa
kama
mgombea wa urais
mwaka
1995
, ambaye alichaguliwa kuwa rais kwenye
uchaguzi
.
Nyerere alikaa muda mwingi kwake Butiama akilima
shamba
lake. Pamoja na haya alianzisha
taasisi
yenye jina lake; mwaka
1996
alionekana akiwa
mpatanishi
wa pande mbalimbali za
vita vya wenyewe kwa wenyewe
huko
Burundi
.
Tarehe 14 Oktoba 1999 aliaga dunia katika
hospitali
ya
St Thomas
mjini
London
baada ya kupambana na
kansa
ya
damu
.
Mafanikio
Nyerere akichanganya
udongo
wa Zanzibar na Tanganyika wakati wa muungano mwaka 1964.
Kati ya mafanikio makubwa ya Nyerere kuna: kujenga umoja wa taifa kati ya watu wa makabila na dini tofauti, na hivyo kudumisha
amani
ya muda mrefu tofauti na hali ya
nchi
jirani, iliyofanya Tanzania iitwe "kisiwa cha amani".
Pia kustawisha
utamaduni
wa
Kiafrika
pamoja na
lugha
ya
Kiswahili
, kushinda
ubaguzi wa rangi
, kutetea
usalama wa taifa
katika
vita
dhidi ya mvamizi
Idi Amin
wa Uganda.
Kutoa mchango kwa vyama vya
ukombozi
vya nchi za
Kusini mwa Afrika
kama vile:
Zimbabwe
(
ZANU
),
Afrika Kusini
(
ANC
na
PAC
),
Namibia
(
SWAPO
),
Angola
(
MPLA
) na
Msumbiji
(
Frelimo
).
Ukosoaji dhidi yake
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Nyerere analaumiwa kwa siasa yake ya kiujamaa kuwa ilichelewesha
maendeleo
ya kiuchumi wa Tanzania. Siasa yake ya
ujamaa
ilishindikana kwa kiasi kikubwa baada ya mwaka
1976
kwa sababu mbalimbali za nje na za ndani ya nchi.
Baada ya kuona kuwa uchumi wa Tanzania hautaweza kusimama kwa siasa ya kijamaa na kuwa hataweza kuvumilia kuendesha nchi kwa siasa nyingine ambazo yeye hakuwa na imani nazo, Nyerere kwa hiari yake mwenyewe aliamua kustaafu nafasi ya urais kuanzia uchaguzi wa mwaka 1985 na kumwachia
usukani
Ali Hassan Mwinyi, aliyetawala kwa siasa ya uchumi wa
soko huria
.
Katika hali ya kukubali
ukweli
, Nyerere katika
tafrija
ya kumwaga alitamka juu ya siasa yake upande wa uchumi: “Nimefeli. Tukubali hivyo.”
Kosa lingine ambalo wengine wanaona Nyerere alilifanya ni kumhadaa aliyekuwa
Rais wa Zanzibar
Mzee
Abeid Amaan Karume
kwa kuziunganisha Tanganyika na Zanzibar, na kuanza kupora
mamlaka
ya Zanzibar kidogokidogo. Kwa hivi sasa Wanzanzibari wengi wamechoka na Muungano huo, na wanataka uhuru wa nchi yao ili wapumue. Hata upande wa
bara
wananchi wengi wanalalamikia kutoweka kwa Tanganyika na serikali yake.
Pia kuna makundi ya
Waislamu
wanaomtuhumu kwa kuendesha kwa siri vita dhidi ya dini yao na kupendelea Wakristo katika utoaji wa elimu na madaraka,japo wasomi wengi kwa kipindi cha utawala wake walikuwa Wakristo.
Sifa zake
Nyerere akicheza
bao
kwake
Butiama
, akitazamwa na mwandamizi wake katika urais Ali Hassan Mwini,
mke
wake
Mama Maria
, na kaka yake, chifu Burito.
Pamoja na hayo, Nyerere bado anakumbukwa na Watanzania hasa wa hali ya chini kutokana na
sera
zake za kujali
utu
. Pia ataendelea kukumbukwa na Waafrika barani kote hasa kwa mchango wake mkubwa wakati wa harakati za kupigania uhuru katika nchi mbali mbali barani Afrika.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni mmoja wa viongozi wachache waadilifu waliokwepa kujilimbikizia
mali
pamoja na kutawala kwa miaka zaidi ya 24.
Kaburi
la Nyerere kijijini Butiama.
Mwishoni mwa maisha yake Nyerere aliishi kama mkulima wa kawaida kijijini kwake Butiama. Alipatwa na
kansa ya damu
(leukemia) akafariki Uingereza wakati wa kutibiwa katika mji wa
London
tarehe 14 Oktoba 1999.
Alizikwa mahali pa kuzaliwa kwake, kijiji cha Butiama.
Heshima na Tuzo
Nishani
Tuzo
Kisha kufa
Machapisho ya mwl.Julius K. Nyerere
- Freedom and Unity
(Uhuru na Umoja): Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1952?1965
(
Oxford University Press
, 1967)
- Freedom and Socialism
(Uhuru na Ujamaa). Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1965-1967 (1968)
- Ndamo zimo: "The Arusha Declaration"; "Education for self-reliance"; "The varied paths to socialism"; "The purpose is man"; and "Socialism and development."
- Freedom & Development
(Uhuru na Maendeleo). Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1968-73
(Oxford University Press, 1974)
- Ndani zimo mada za elimu kwa watu wazima; uhuru na maendeleo; kujitegemea; na miaka kumi ya uhuru.
- Ujamaa - Essays on Socialism'
(1977)
- Crusade for Liberation
(1979)
- Julius Kaisari
, Tafsiri ya mchezo wa
William Shakespeare
unaoitwa
Julius Caesar
- Mabepari wa Venisi
, Tafsiri ya mchezo mwingine wa William Shakespeare,
The Merchant of Venice
- Utenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo wa Mathayo
, Tafsiri ya kishairi ya
Injili ya Mathayo
- Utenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo wa Marko
, Tafsiri ya kishairi ya
Injili ya Marko
- Utenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo wa Luka
, Tafsiri ya kishairi ya
Injili ya Luka
- Utenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo wa Yohana
, Tafsiri ya kishairi ya
Injili ya Yohane
- Utenzi wa Matendo ya Mitume
, Tafsiri ya kishairi ya
Matendo ya Mitume
Marejeo
Viungo vya nje
|
---|
Nadharia
| |
---|
Watetezi
| |
---|
Mashirika
| |
---|
|
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Julius Nyerere
kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|