Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Siku ya Mtoto wa Afrika
(kwa
Kiingereza
:
Day of the African Child
) ni siku inayosherehekewa kila
mwaka
tarehe
16 Juni
tangu mwaka
1991
ilipoteuliwa na
Umoja wa Afrika
katika kuenzi michango ya
watoto
walioshiriki katika
maandamano
katika
mji
wa
Soweto
,
Afrika Kusini
mwaka
1976
pamoja na kujengea
jamii
uelewa juu ya umuhimu wa
elimu
bora kwa watoto.
Tarehe 16 Juni 1976, maelfu ya watoto katika nchi ya Afrika Kusini walikusanyika katika mji wa Soweto kwa ajili ya maandamano yenye malengo ya kudai
elimu
bora, mamia ya watoto walipigwa
risasi
na kuuliwa, watoto zaidi ya
elfu
moja walijeruhiwa.
Tarehe 16 ya kila mwaka, mataifa, jumuia mbalimbali na jumuia za kimataifa pamoja na wadau mbalimbali hukusanyika pamoja kwa ajili ya kujadili fursa na changamoto zinazowakumba watoto katika
bara
la
Afrika
.