Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jonas Malheiro Savimbi
(
3 Agosti
1934
-
22 Februari
2002
) alikuwa
kiongozi
wa
vita vya msituni
nchini
Angola
.
Mwaka
1966
alianzisha tapo la
UNITA
(kwa
Kireno
:
Uniao Nacional para a Independencia Total de Angola
) kama harakati ya kukomboa Angola kutoka
ukoloni
wa
Ureno
. UNITA ilikuwa moja kati ya harakati tatu zilizoshindana.
UNITA ilianza kama kikundi cha
kikomunisti
kufuatana na
itikadi
ya
Mao Zedong
. Uadui kati ya Wakomunisti wa
Uchina
na
Urusi
ulionekana katika mashindano ya UNITA dhidi ya
MPLA
(kwa Kireno: Movimento Popular de Libertacao de Angola - Partido do Trabalho) iliyosaidiwa na Urusi.
Baada ya
uhuru
mwaka
1975
MPLA ilitawala
mji mkuu
na kuunda
serikali
rasmi lakini Savimbi aliendelea kuipinga.
Savimbi alipata kupokea baadaye usaidizi kutoka maadui wote wa MPLA bila kujali itikadi. UNITA ilipata misaada toka serikali mbalimbali
duniani
ili kuiondoa
madarakani
serikali ya MPLA. Savimbi alikuwa akipata misaada ya
fedha
na
silaha
toka serikali za
Marekani
,
China
,
Afrika Kusini
,
Ivory Coast
,
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(wakati huo ikijulikana kama
Zaire
),
Moroko
, n.k. Serikali ya Angola ilikuwa ikipata misaada toka
Urusi
,
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani
,
Kuba
, na
Nicaragua
.
Savimbi aliuawa vitani tarehe 22 Februari 2002. Muda mfupi baadaye UNITA na MPLA zilikubaliana kusimamisha mapigano. UNITA ilichukua nafasi ya chama cha upinzani. Hata hivyo taratibu za kidemokrasia zilichelewa hadi
chaguzi
za miaka
2008
na
2012
na toleo la katiba mpya la mwaka
2010
.
|
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Jonas Savimbi
kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|