Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Chombo cha angani
ni
chombo kwa ajili ya kusafiri
katika
anga-nje
ya
dunia
yetu.
Vyombo vya anga vinaundwa kwa
kazi
nyingi pamoja na
mawasiliano
, kubeba vifaa vya kutazama dunia au
hali ya hewa
, kufanyia
utafiti
sayari
nyingine au kusafirisha
watu
na mizigo.
Vyombo vingine vinaingia kwa
muda
mfupi tu juu ya
angahewa
bila kumaliza
mzingo
wa dunia. Vingine vinazunguka kwenye mzingo kwa muda mrefu hata miaka.
Chombo cha angani cha kwanza kilikuwa
Sputnik 1
kilichorushwa na
Umoja wa Kisovyeti
mwaka
1957
na kuzunguka dunia kwa miezi 3. Kilifuatwa na chombo cha
Marekani
"Explorer 1" mwaka
1958
.
Mtu wa kwanza kwenye anga-nje alikuwa
Mrusi
Yuri Gagarin
aliyerushwa na Umoja wa Kisovyeti kwa chombo cha
Vostok 1
tarehe
12 Aprili
1961
na kumaliza mzingo mmoja wa dunia.
Marekani ilifuata tarehe
5 Mei
1961 kwa kumpeleka
mwanaanga
Alan Shepard
nje ya angahewa lakini bila kumaliza mzingo kamili. Mnamo
Februari
1963
Mmarekani
John Glenn
alifaulu kutimiza mizingo 3 ya dunia.
Marekani iliendelea kuandaa
safari
ya kufika
mwezini
na kuwafikisha wanaanga
Neil Armstrong
na
Buzz Aldrin
mwezini tarehe
20 Julai
1969
kwa kutumia chombo
Apollo 11
.
Ilhali maandalizi ya safari za kupeleka watu
anga-nje
ni ghali sana bila kuleta
faida
kubwa
kiuchumi
au
kisayansi
, kuna mamia ya vyombo vya anga vinavyozunguka dunia na kutekeleza kazi muhimu. Hivi huitwa pia
satelaiti
zikifuata mwendo wa kudumu wa kuzunguka dunia au kukaa mahali pamoja angani juu ya
uso
wa dunia.
Utabiri
wa
hali ya hewa
hutegemea
data
na
picha
kutoka vyomboanga. Sehemu ya
majadiliano
kwa
simu
na sehemu kubwa ya picha za
televisheni
hupitia satelaiti, na vilevile data za
teknolojia
kama
GPS
.
Vyomboanga vingine kama
vipimaanga
vinapewa kazi ya
upelelezi
angani hasa kukaribia
sayari
, kukusanya data zao na kuzituma duniani. Habari nyingi juu ya sayari za
mfumo wa jua letu
zimepatikana kutokana na
upimaji
uliotekelezwa na vipimaanga hivi.