Republic of Zambia
Jamhuri ya Zambia
|
Jamhuri ya Zambia
ni nchi ya
Kusini mwa Afrika
isiyo na
mwambao
baharini
.
Imepakana na
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
na
Tanzania
upande wa
kaskazini
,
Malawi
upande wa
mashariki
,
Msumbiji
,
Zimbabwe
na
Botswana
upande wa
kusini
,
Namibia
na Angola upande wa
magharibi
.
Mji mkuu
ni
Lusaka
(wenye wakazi 1,747,152 mwaka 2010).
Jina
limetokana na
mto
Zambezi
. Jina la zamani za
ukoloni
(hadi
1964
) lilikuwa "
Northern Rhodesia
".
Nchi kwa sehemu kubwa ni
nyanda za juu
kuanzia
mita
1.000 hadi 1.400 juu ya
UB
.
Milima
ya Muchinga imepanda hadi mita 2.164,
kilele
cha juu kabisa kiko kwenye mita 2.301 huko milima ya
Mafinga Hills
.
Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa
wawindaji
wa jamii ya
Wasani
na
Watwa
.
Katika
karne
za kwanza za
milenia ya 1
BK
walifika wahamiaji
Wabantu
wenye
ujuzi
wa
kilimo
na
uhunzi
.
Baada ya
wapelelezi
Wazungu
kufika katika
karne ya 18
, Zambia ikawa
nchi lindwa
ya
Uingereza
kwa jina la
Northern Rhodesia
mwishoni mwa
karne ya 19
.
Tarehe
24 Oktoba
1964
, Zambia ikawa huru na
waziri mkuu
Kenneth Kaunda
akawa
rais
wa kwanza.
Chama
chake cha
kijamaa
United National Independence Party (UNIP) kilitawala kuanzia mwaka 1964 hadi
1991
, kikiwa chama pekee halali kuanzia mwaka 1972.
Baada ya Kaunda kuanguka,
Frederick Chiluba
wa Movement for Multi-Party Democracy alitawala tangu mwaka 1991, akafuatwa na
Levy Mwanawasa
(
2002
-
2008
).
Aliyefuata tena ni rais
Rupiah Banda
(2008-2011), halafu
Michael Sata
wa Patriotic Front party (2008-2014).
Baada ya
kifo
chake,
Guy Scott
alikaimu hadi
uchaguzi
wa tarehe
20 Januari
2015
, ambapo
Edgar Lungu
alipata kuwa rais wa sita.
Wakazi wa Zambia ni wasemaji wa
lugha
za
Kibantu
katika
makabila
73. Makubwa ndio
Wabemba
(19%),
Watonga
(13.6%),
Watumbuka
,
Wachewa
,
Walozi
,
Walunda
,
Waluvale
,
Wakaonde
,
Wankoya
na
Wanyanja
-. Hata hivyo
lugha rasmi
ni
Kiingereza
.
Idadi kubwa ni
wakulima
wa kujitegemea, ingawa 44% wanaishi mijini.
Upande wa
dini
, karibu wote ni wafuasi wa
Ukristo
ambao ndio
dini rasmi
kwa mujibu wa
katiba
ya nchi. 75.3% ni
Waprotestanti
, 22% ni
Wakatoliki
na wengine wana dini ya aina nyingine au ni
wakanamungu
.
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Afrika
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Zambia
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|