Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Yugoslavia
(Jugoslavija na ?угослави?а kwa
Kikyrili
"Nchi ya Waslavoni ya Kusini")
ilikuwa nchi katika
Ulaya
kusini mashariki kati ya 1918 na 2003.
Ufalme wa Waserbia, Wakroatia na Waslovenia
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Ilianzishwa kwa jina la "Ufalme wa Waserbia, Wakroatia na Waslovenia" mwaka
1918
baada ya kuporomoka kwa
Austria-Hungaria
. Ufalme huu uliunganisha nchi za awali za
Serbia
na
Montenegro
pamoja na sehemu za Dola la Austria zilizokaliwa na Waslavoni. Tangu 1929 ufalme ulibadilisha jina kuitwa "Ufalme wa Yugoslavia". Tangu mwanzo tatizo mojawapo la nchi ilikuwa uhusiano kati ya mataifa mawili makubwa ndani yale yaani Waserbia na Wakroatia. Ingawa yote mawili ni karibu sana kuna tofauti za historia, dini na utamaduni ziilizosababisha hofu ya kutawaliwa kwa upande mmoja na mwingine.
Wakati wa
Vita Kuu ya Pili ya Dunia
Yugoslavia ilivamiwa na jeshi la
Ujerumani
. Wapinzani mbalimbali walichukua silaha kupinga wavamizi. Kati ya vikundi hivi wanamgambo
Wakomunisti
chini ya
Josip Broz Tito
wakafaulu kuliko jeshi la msituni wa mfalme. Baada ya mwisho wa vita
1945
kundi la Tito lilichukua utawala.
Shirikisho la Jamhuri ya Watu wa Yugoslavia
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Katiba mpya ya
1946
iliunda Yugoslavia upya kama shirikisho la kisoshalisti. Majimbo 6 zilizoitwa pia "jamhuri" ziliundwa pamoja na mikoa miwili ya kujitawala ndani ya Serbia:
- 1. Jamhuri ya kisoshalisti ya
Bosnia na Herzegovina
(mji mkuu Sarajevo)
- 2. Jamhuri ya kisoshalisti ya
Kroatia
(mji mkuu Zagreb)
- 3. Jamhuri ya kisoshalisti ya
Masedonia
(mji mkuu Skopje)
- 4. Jamhuri ya kisoshalisti ya
Montenegro
(mji mkuu Titograd (sasa Podgorica))
- 5. Jamhuri ya kisoshalisti ya
Serbia
(mji mkuu Beograd) na ndani yake:
- 5a. Mkoa wa kisoshalisti ya
Kosovo
(mji mkuu Pri?tina)
- 5b. Mkoa wa kisoshalisti ya
Vojvodina
(mji mkuu Novi Sad)
- 6. Jamhuri ya kisoshalisti ya
Slovenia
(mji mkuu Ljubljana)
Tito aliamua kutotii tena amri na maagizo kutoka
chama cha kikomunisti
cha
Umoja wa Kisovyeti
.
Yugoslavia ilifuata siasa ya kutoshikamana na pande zote mbili za vita baridi yaani
Marekani
na
Urusi
.
Baada ya kifo cha Tito umoja wa Yugoslavia ulidhoofika. Mashindano kati ya mataifa ndani ya nchi yaliongezeka.
1991 Kroatia, Slovenia na Masedonia zilichukua hatua ya kutoka nje ya shirikisho na kujitangaza kuwa nchi huru za pekee. 1992 jimbo la Bosnia na Herzegovina likafuata na kutoka nje.
Tangu 1992 "Yugoslavia" ilikuwa jina la umoja wa Serbia na Montenegro pekee. 2003 jina la Yugoslavia lilifutwa.
Mwaka 2006 hata umoja uliobaki kati ya Serbia na Montenegro ulifutwa na kila nchi imeendelea pekee yake.
|
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Yugoslavia
kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|