Mwanajeshi wa misalaba (
mchoro
wa
karne ya 13
).
Mtawa
Petro mkaapweke
akihubiri vita vya msalaba mbele ya makabaila wa Ufaransa.
Vita za Misalaba
(pia:
Vita vya msalaba
) vilitokea kati ya mataifa ya
Wakristo
wa
Ulaya
na watawala
Waislamu
wa nchi za
Mashariki ya Kati
wakati wa
karne
za
11
hadi
13
, hasa kuanzia
1095
hadi
1291
katika jina la
dini
na kwa
baraka
za
Kanisa Katoliki
.
Kaisari
wa
Bizanti
aliomba msaada wa
Wakristo wa magharibi
dhidi ya mashambulio ya
Waturuki
Waislamu. Hivyo
Papa
aliwaita mataifa ya Kikatoliki ya Ulaya kuikomboa
nchi takatifu
. Tangu mwaka
1096
hadi mwaka
1270
kampeni za kijeshi zilianzishwa Ulaya kuelekea
Yerusalemu
.
Kwa maana nyingine na pana zaidi "vita vya msalaba" vilikuwa
jitihada
za watawala wa Ulaya kutetea
haki
za Wakristo wenzao wa nchi hizo, au kujitetea kwa
silaha
na
vita
na wakati huohuo kueneza
himaya
yao pamoja na
Ukristo
.
Jina limetokana na
desturi
ya
wanajeshi
wa
vita ya kwanza ya misalaba
kushona
alama
ya
msalaba
juu ya
nguo
zao kama
dalili
ya
kiapo
walichotoa cha kuwafukuza Waislamu katika
mji
wa
Yerusalemu
. Walifundishwa kuwa vita hivyo ni vitakatifu: atakayekufa atafika mbinguni kwa hakika. Wataalamu wanahisi kama hapo athari za mafundisho ya Kiislamu juu ya "
jihadi
" zimeingia katika Ukristo.
Hali ya Wakristo wa Yerusalemu na Mashariki ya Kati
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Tangu mwaka
637
BK
mji wa Yerusalemu pamoja na nchi nzima ya
Palestina
ilikuwa mikononi mwa
Waarabu
Waislamu waliofaulu kushinda jeshi la
Bizanti
. Wakazi wengi wa nchi hiyo waliendelea kufuata dini zao, hasa Ukristo na
Uyahudi
, lakini sehemu ya wananchi polepole waligeukia pia Uislamu.
Yerusalemu iliendelea kuwa lengo la
wahiji
Wakristo waliotaka kutembelea mahali ambako
Yesu Kristo
aliishi, hasa
Kanisa la Kaburi na Ufufuo wa Yesu
.
Watawala Waarabu waliwahi kuahidi kuheshimu Wakristo walioishi chini ya utawala wao na kutunza haki zao.
Hali hiyo ilibadilika vibaya mara ya kwanza wakati ya
khalifa
Al Hakim
wa
Misri
aliyewatesa Wakristo kuanzia mwaka
1001
; Kanisa la Kaburi na Ufufuo lilibomolewa pamoja na makanisa mengi nchini
Palestina
.
Dhuluma
ya Al Hakim ililegezwa na waandamizi wake, na
kanisa
hilo la Yerusalemu likajengwa upya kwa msaada wa
Kaisari
wa Bizanti.
Amani
katika mashariki ya kati ilivurugika tena kutokana na uenezi wa
Waseljuki
waliokuwa kabila kubwa la
Waturuki
kutoka
Asia ya kati
waliokuwa wamehamia magharibi, kupokea
Uislamu
na kutawala
Uajemi
pamoja na maeneo ya jirani. Mwaka
1071
jeshi
la Waseljuki lilishinda Wabizanti kwenye
mapigano ya Manzikert
na kutwaa sehemu kubwa ya
Anatolia
(leo
Uturuki
) pamoja na
Siria
na Palestina. Vikosi vya Seljuki walishambulia pia mara kwa mara wahiji Wakristo kutoka Ulaya walioelekea
kaburi
takatifu mjini Yerusalemu na hija ya Kikristo ya Yerusalemu ikaona kipindi kigumu. Wakristo waliohiji huko kutoka Ulaya walishambuliwa njiani mara kwa mara.
Mwaka
1095
Kaisari
Aleksios I wa Bizanti
alipanga kuwaondoa tena Waseljuki katika Anatolia kutoka sehemu walizowahi kutwaa miaka michache ya nyuma. Hapa alituma ma
balozi
kwa
Papa Urban II
wa
Roma
kwa kusudi la kupata msaada wa
askari wa kukodiwa
kutoka Ulaya. Alifanya hivyo miaka 40 baada ya kutokea kwa
farakano la mwaka 1054
kati ya makanisa ya
Waorthodoksi
na Roma, labda kwa tumaini la kuanzisha upya maelewano.
Wito wa Papa Urban II mwaka 1095
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Papa Urban II aliwapokea mabalozi wa Bizanti katika Italia akasikia ombi la Kaisari. Inaonekana aliona nafasi ya kuwaelekeza mashariki ma
kabaila
wadogo wa Ulaya ambao walizoea kuvuruga amani ya Ulaya kwa mapigano ya mfululizo na vita ndogondogo, wakiharibu
mali
ya watu wengi.
Kwenye
sinodi
ya Clermont, mbele ya ma
askofu
na ma
abati
wa
Ufaransa
alitangaza ombi la msaada kutoka Bizanti na kuhimiza makabaila kupokea
wito
huu wa kuwasaidia Wakristo wenzao wa mashariki badala ya kuharibu mali ya watu wa nyumbani.
Hotuba
ya Papa ikapokewa na sinodi na
umati
mkubwa wa wasikilizaji walioitikia kwa
sauti
moja "Mungu anaitaka" (Deus lo vult).
Makabaila kadhaa walipiga ma
goti
mbele ya
Papa
wakiomba baraka kwa mipango yao ya kuitikia wito wake. Wengine walisikia habari hizo baadaye, na makabaila wengi wa
Ufaransa
waliamua kujiunga na
mradi
wa kwenda mashariki kuwasaidia Wakristo wa huko na kuwaondoa Waislamu katika nchi zilizowahi kuwa za Kikristo.
Wahubiri walizunguka Ulaya kutangaza mpango huo. Ni wahubiri hao waliosambaza ujumbe wa kwamba
shabaha
ya vita ni Yerusalemu, ingawa wala Kaisari Aleksios wala Papa Urban waliwahi kutumia jina hilo. Lakini wakati ambapo watu wengi hawakujua kusoma na kuandika wala hawakuwahi kuona
ramani
jina la Yerusalemu lilijulikana kote hata kama wasikilizaji wengine hawakuelewa tofauti kati ya mahali pa dunia hii na
Yerusalemu wa mbinguni
uliohubiriwa pia kanisani.
Vita vya msalaba vilivyoanza na kuendelea
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Mwaka
1096
vilikusanyika vikundi vya watu wa kawaida walioongozwa na wahubiri waliotaka kwenda mashariki kwa hiari yao, ingawa si
wanajeshi
. Umati huo waliomba na kutisha miji walipopita wapewe
chakula
na misaada kwa sababu wengi hawakuwa na kitu wenyewe. Katika miji ya
Ujerumani
ya magharibi na kusini walianza kushambulia
Wayahudi
walioishi huko na kuwaua wengi.
Mwaka
1099
jeshi la Ulaya lilifika mbele ya kuta za Yerusalemu. Baada ya mapigano mafupi
jeshi la msalaba
liliwashinda wateteaji Waislamu. Katika
hasira
ya mapigano waliua ovyo wakazi wengi sana,
wazee
na
watoto
, wakiwemo Waislamu, Wakristo na Wayahudi. Kabaila Mfaransa alipokea cheo cha "Mfalme wa Yerusalemu".
Lakini miaka 100 baadaye
Sultani
Salah-ed-Din
wa Misri aliwafukuza tena wanamsalaba kutoka Yerusalemu. Miaka 40 baadaye alirudisha mji kwa hiari baada ya kupatana na Mfalme Mjerumani. Lakini muda wote huo
Wazungu
walitawala sehemu ya Palestina na Siria tu. Waislamu waliwaona kama maadui. Hata Wakristo wenyeji (
Waorthodoksi
) hawakuwakubali kuwa wakombozi kwani walijaribu kuwaunganisha Wakristo wote chini ya
Kanisa Katoliki
.
Safari
moja iliyoondoka Ulaya mwaka 1204 ili kuikomboa Yerusalemu, kumbe ilifika mpaka Bizanti tu ambako wanajeshi wa msalaba waliteka mji, kupora
utajiri
na kumfukuza Kaisari wa Bizanti. Miaka 100 baadaye Kaisari alirudi na kuunda upya Ufalme wa Roma ya Mashariki.
Mwaka
1291
jeshi la Kiislamu liliwafukuza kabisa wanajeshi wa msalaba katika
nchi takatifu
wasirudi tena. Lakini walikuwa wamevunja nguvu ya Bizanti kiasi cha kutosha. Kumbe Ulaya Magharibi iliharibu
ulinzi
wa dola la mashariki dhidi ya
Waturuki
waliofaulu baadaye kuingia Ulaya. Badala ya kufukuzwa, jeshi la Waturuki lilianza kuishambulia Ulaya Kusini-Mashariki. Mwaka
1453
ulianguka mji wa Bizanti, na mwaka
1529
Waturuki walifika mpaka
Vienna
,
mji mkuu
wa Mfalme wa Ujerumani. Hapo walirudishwa nyuma. Lakini nchi nyingi za Ulaya Kusini-Mashariki pamoja na Wakristo wao walikaa chini ya Waturuki kwa
karne
tatu zijazo.
Kwa ujumla majaribio ya vita vya msalaba ya kuikomboa nchi takatifu yalishindikana. Vita hivyo vilidhoofisha Wakristo wa Mashariki waliozoea kuishi chini ya Waarabu Waislamu. Kipindi cha vita vya kidini kilisababisha mateso mengi kwa Wakristo Waorthodoksi chini ya Waislamu. Walidaiwa kulipa ma
deni
yaliyoachwa nyuma na
ndugu
zao kutoka Ulaya Magharibi.
Katika uhusiano mgumu kati ya dini hizo mbili kule Ulaya na Mashariki ya Kati, Waislamu walivunja ahadi nyingi walizozitoa, lakini mahali pengi Wakristo walipewa nafasi za kuendelea kuishi kati ya Waislamu. Maisha haya yalikuwa mara nyingi magumu, lakini mahali pengi waliruhusiwa kuendelea na ibada zao (ila waliweza kukataliwa kujenga makanisa au hata kutengeneza makanisa ya kale isipokuwa kwa kulipa tena kodi za nyongeza). Katika mambo ya
ndoa
au
urithi
wa mali walikuwa chini ya makanisa yao. Viongozi wa makanisa yao waliwajibika mbele ya serikali ya Kiislamu juu ya ushirikiano mwema.
Kwa namna hiyo jumuiya za makanisa kama vile la Kigiriki, la Kikopti, la Kisiria, la Kiarmenia n.k. zilihifadhiwa mpaka leo katika nchi za Kiarabu, isipokuwa idadi ya waumini wao iliendelea kupungua. Sababu kuu ni kwamba kama Mkristo alikuwa amegeuka Mwislamu hakuweza kurudi tena. Sheria ya Kiislamu inamruhusu Mkristo kugeukia Uislamu, lakini mtu aliyekuwa Mwislamu anastahili
adhabu ya kifo
akigeukia Ukristo au
dini
nyingine. Pamoja na hayo, Wakristo wengi walianza kuhamia nchi ambako watakuwa
raia
huru bila kasoro.
Wakati ule Wakristo wengi walikosa vilevile ustahimilivu kwa watu wenye
imani
tofauti. Hakuna Mwislamu aliyeweza kubaki katika nchi za
Hispania
na
Ureno
baada ya kuvunjwa wa utawala wa Kiarabu. Lakini ipo mifano mingine: Wakristo wote walifyekwa Uarabuni kwenyewe kumbe Waislamu waliweza kubaki chini ya Waaustria Wakristo waliotawala nchi za Ulaya Kusini-Mashariki. Kweli kati ya dini hizo mbili hakuna anayeweza kujisifu tu juu ya historia yake bila kukiri makosa na kasoro zake.