Watawa wa kike wa dini mbalimbali katika sehemu tofauti za
dunia
.
Mtawa
ni
mtu
anayejitenga na
ulimwengu
ili kuishi
maisha
maadilifu
.
Katika
dini
mbalimbali, mfano mmojawapo wa
utawa
ni ule wa
wamonaki
. Lakini katika
Ukristo
, hasa
wa Magharibi
historia ya Utawa
ilitokeza aina nyingine mbalimbali.
Katika
Kanisa Katoliki
, mtawa ni
mwamini
yeyote aliyejiweka
wakfu
kwa
Mungu
hasa kwa kushika
useja mtakatifu
, lakini kwa kawaida pia
ufukara
na
utiifu
.
Mara nyingi watawa wanaunda ma
shirika
yenye
karama
moja inayofafanuliwa na kuratibiwa katika
kanuni
na
katiba
maalumu.
Mtawa anaweza kuwa
mwanamume
au
mwanamke
, mwenye
daraja takatifu
au la.
Wakristo wote wanavyopaswa kulenga
ukamilifu
kutokana na
amri
kuu ya
upendo
, lakini mtawa ana
wajibu
wa pekee wa kufanya hivyo kwa kuwa
adili
la
ibada
linahitaji kuhuishwa na upendo kwa Mungu ulio safi na wa nguvu zaidi na zaidi.
Msingi wa wajibu huo ni
nadhiri za kitawa
, ambazo
neema
zake si za
muda
, bali za kudumu mtu akizidi kuwa mwaminifu. “Wengine wako katika hali ya ukamilifu, si kwa sababu ya kufanya tendo la upendo kamili, bali kwa kujifunga moja kwa moja, kwa fahari fulani, washike kile kinachoelekeza kwenye ukamilifu… Kwa kuwa watawa wanajifunga kwa nadhiri kujinyima malimwengu ambayo wangeruhusiwa kuyatumia kwa hiari; wanafanya hivyo ili kushughulikia mambo ya Mungu kwa urahisi zaidi… Vilevile maaskofu wanajifunga kushika ukamilifu wanapokubali daraja ya uaskofu, kwa sababu mchungaji anapaswa kutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo zake” (
Thoma wa Akwino
).
Mtawa anatamka atalenga ukamilifu: “Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo, kwa ajili yake, nimeshikwa na Kristo Yesu” (
Fil
3:12). Hatendi kosa la
unafiki
kama hajawa mkamilifu, ila analifanya asipolenga ukamilifu kwa unyofu. Kwake wajibu huo wa pekee na ule wa kushika
nadhiri
zake na
kanuni
aliyoahidi ni mamoja. Lakini wajibu huo uzingatiwe daima kuhusiana na ule wa jumla unaotokana na amri kuu ya upendo; hapo utawa hautatazamwa upande wa
sheria
tu, bali utaonekana katika upana wa maana yake ya Kiroho.
Kwa mtazamo huo tu utaeleweka kweli neno zito la Thoma wa Akwino: “Kufanya tendo kwa nadhiri kunastahili kuliko kulifanya bila nadhiri”. Si kwamba tuzidishe nadhiri ili kustahili zaidi, bali mtawa atekeleze nadhiri zake vizuri zaidi na zaidi, akizidi kuchimba sababu tatu alizozitoa mtakatifu huyo katika
ufafanuzi
wake:
- Nadhiri ni tendo la adili la ibada, ambalo ni bora kuliko yale ya utiifu, ufukara na usafi wa moyo ambayo linamtolea Mungu yawe ibada.
- Kwa nadhiri ya daima mtu anamtolea Mungu si tendo mojamoja, bali uwezo wenyewe wa kutenda, na kwa hakika ni afadhali kutoa
mti
na
matunda
yake kuliko kutoa matunda tu.
- Kwa nadhiri
utashi
unaimarishwa katika kutenda mema, na kwa hakika kutenda kwa msimamo kunastahili zaidi, kama vile ni vibaya zaidi kutenda dhambi kwa utashi ulioshupalia
uovu
.
Mtu akiishi kwa roho hiyo ataelewa kwa namna hai fundisho la kwamba, kwa kujifunga kushika mashauri matatu, yaliyo
kiini
cha utawa, mtu anajitenga na yale yanayoweza yakazuia mapendo yake yasimuelekee Mungu tu, halafu asipofuta uamuzi huo anajitoa kwake kama
sadaka ya kuteketezwa
. Hivyo hali yake ni ya kujitenga na
ulimwengu
na ya kuwekwa wakfu kwa Mungu.
Hasa mambo matatu yanaweza kuzuia mapendo yake yasimuelekee Mungu:
tamaa za macho
(yaani za vitu vinavyoonekana),
tamaa za mwili
na
kiburi
cha maisha (yaani kupenda awe huru tu). Mtawa anayakataa hayo matatu kwa nadhiri zake, akimtolea Mungu
mali
kwa ufukara,
mwili
na
moyo
kwa useja mtakatifu na matakwa yake kwa utiifu. Asipojitwalia tena chochote, bali akitekeleza vizuri, kwa upendo mkubwa zaidi na zaidi, maadili matatu yanayohusiana na nadhiri za kitawa, basi anamtolea kweli Mungu
sadaka
ile kamili inayostahili kuitwa ya kuteketezwa. Hapo maisha yake yanatolewa kila siku pamoja na sadaka ya
misa
kwa adili la ibada. Ni hivyo hasa kama mtawa anarudia mara nyingi
ahadi
zake kwa namna inayostahili kuliko alipozitoa kwa mara ya kwanza.
Stahili
zinakua ndani mwake pamoja na upendo na maadili mengine, hivyo hali yake ya kuwekwa wakfu kwa Mungu inazidi kuwa ya dhati na kamili.
Lengo la kujinyima pande tatu na kujitoa pande tatu ni kuungana na Mungu kila siku zaidi, kama utangulizi wa
uzima wa milele
. Mtawa anaitwa kuufikia muungano huo kwa kumuiga
Yesu
aliye “njia, na kweli, na uzima” (
Yoh
14:6). Yeye, katika ubinadamu wake, alitenganika na roho ya ulimwengu akaunganika na Mungu vizuri iwezekanavyo. Mtawa anatamka hadharani nia ya kumfuata, lakini Yesu alitoka juu, kumbe mtawa ametoka duniani, palipotawaliwa na dhambi, hivyo anapaswa kujitenga zaidi na zaidi na mambo yote ya dunia, kadiri ya maneno haya: “Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu” (
Kol
3:1-4). Thoma wa Akwino alifafanua hivi, “Msionje malimwengu kwa kuwa mmefia ulimwengu; uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo; mwenyewe amefichika kwetu, kwa kuwa yuko katika utukufu wa Mungu Baba yake, na hivyo uhai… tulionao kutoka kwake umefichika, kadiri ya maneno ya Maandiko matakatifu, ‘Jinsi zilivyo nyingi fadhili zako ulizowawekea wakuchao; ulizowatendea wakukimbiliao mbele ya wanadamu!’ (
Zab
31:19). ‘Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa’ (
Ufu
2:17)”. Hiyo
mana
ya Kiroho, ambayo ile ya
jangwani
ilikuwa mfano wake tu, ndiyo
chakula
cha roho: kujaliwa kuzama katika mafumbo ya imani. Hivyo utekelezaji wa maadili unaandaa kumiminiwa
sala
; kwa namna ya pekee “
ubikira
unalenga ustawi wa roho katika maisha ya kuzamia sala” (Thoma wa Akwino). Hivyo tena maisha ya kitawa yanalenga zaidi na zaidi utekelezaji kamili wa amri ya upendo na undani wa
muungano na Mungu
.
Wajibu wa pekee alionao mtawa wa kulenga ukamilifu uzingatiwe daima kuhusiana na wajibu wa waamini wote unaotegemea amri kuu ya upendo. Amri hiyo inatawala mashauri ya Kiinjili, kwa kuwa hayo ni njia na vyombo tu kwa ajili ya kufikia ukamilifu wa upendo kwa
kasi
na hakika zaidi. Hivyo, maadili matatu ya kitawa yanatekelezwa kikamilifu kwa
maadili matatu ya Kimungu
. Kati ya hayo yote kuna fungamano la dhati, hivi kwamba
tumaini
la
heri
ni kama
uhai
wa
ufukara
mtakatifu ambao unaachana na mali ya dunia na kutufanya tuzidi kumtumainia Mungu ili kupata ya
milele
; upendo ndio uhai wa
useja
unaojinyima
mapendo
ya chini ili kupata upendo wa juu kabisa: unapotekelezwa sawasawa unastawisha ndani mwetu upendo kwa
Bwana
na kwa watu; imani ndiyo uhai wa utiifu unaotekeleza maagizo ya wakubwa kana kwamba yamefunuliwa na Mungu: utekelezaji huo unakuza roho ya imani. Hivyo maisha ya kitawa yanafikisha kwenye
sala ya kumiminiwa
na muungano wa dhati na Mungu unaozidi kustawisha ule na jirani.
Adili la ibada linadhihirika kuwa la
kishujaa
mtu anapotimiza
wajibu
alionao upande huo bila kujali upinzani mkali wa
ndugu
wa
ukoo
na wengineo. Linadhihirika vilevile katika utekelezaji wa nadhiri ya kutenda yaliyo bora, na katika uanzilishi wa familia ya kitawa kati ya matatizo makubwa ambayo kwa kawaida yanaendana nao.
Ufukara wa kishujaa unajinyima vyote, ukiridhika na riziki za lazima tu, ili kufanana na Bwana ambaye hakuwa na mahali pa kupumzikia. Asiyetamani chochote hakosi kitu, ni tajiri Kiroho na mwenye heri. Usafi wa moyo wa kishujaa unadhihirika hasa katika ubikira wa kudumu, mtu anapoishi mwilini maisha ya Kiroho tu hata akasahau vurugu zote za hisi kwa kuzoea kuzishinda. Hatimaye utiifu wa kishujaa unadhihirika katika kujikatalia kikamilifu matakwa ya binafsi, mtu asipofanya chochote bila ruhusa ya wakubwa, akiwatii wote bila kujali walivyo, hata wasipomuonyesha wema. Pengine anadaiwa kutii maagizo magumu, kama vile
Abrahamu
alivyodaiwa sadaka ya mwanae pekee. Hapo anahitaji imani kubwa ambayo imuonyeshe Mungu ndani ya wakili wake. Ni nafasi ya giza ambayo ikivukwa vizuri inaleta mwanga mkubwa, kwa kuwa Bwana anamlipa kwa ukarimu yule anayetii hivyo.
|
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|