Mchoro wake uliofanywa na
Fra Bartolomeo
Mtakatifu Thoma wa Akwino
Mchoro wake uliofanywa na
Carlo Crivelli
.
Mtakatifu Thomas Aquinas
(
Roccasecca
, katika eneo la watawala wa
Aquino
, leo katika
wilaya
ya
Frosinone
,
Italia
, 1224 au 1225 -
Fossanova
, wilaya ya
Latina
, Italia,
7 Machi
1274
) alikuwa
mtawa
wa
Shirika la Wahubiri
na
padri
wa
Kanisa Katoliki
.
Mwenye
akili
kubwa ajabu, alishirikisha
hekima
yake ya pekee kwa mafundisho na kwa
maandishi
.
Mnyofu, mkimya, aliyekuwa tayari kutumikia, kiutu alipendwa na wote, naye alipendelea watu wa chini, akihubiria mafukara kwa
usahili
na
wema
hata zaidi ya mara moja kwa siku.
Kuliko wengine wote, Thoma aliona
elimu
na masomo kama njia ya kufikia
utakatifu
; ni kati ya watu bora upande wa
nadharia
, hasa wa
teolojia ya shule
, iliyofikia kilele chake katikati ya
karne XIII
.
Mwanafunzi wa
Alberto Mkuu
, alitumia hasa mawazo ya
mwanafalsafa
wa
Ugiriki
Aristoteli
na ya
Waarabu
waliomtafsiri, lakini pia ya
Plato
: ili kufafanua
imani
, alikubali
ukweli
ulioweza kutolewa na yeyote, kwa sababu kweli zote zinatoka kwa
Mungu
; kinyume chake alikanusha udanganyifu wowote.
Hivyo aliweza kufanya
usanisi
mpana ambao mpaka leo
Kanisa Katoliki
linautambua kama tokeo bora la mafundisho yake lenyewe na kama kielelezo cha namna ya kufikiri na ya kufanya
teolojia
.
Anajulikana hasa kwa vitabu vyake “Jumla ya Teolojia” (kwa
Kilatini
Summa theologiae
) na “Jumla dhidi ya Wapagani” (kwa Kilatini
Summa contra gentiles
).
Alitangazwa na
Papa Yohane XXII
kuwa
mtakatifu
tarehe
18 Julai
1323
, halafu na
Papa Pius V
kuwa
mwalimu wa Kanisa
mwaka
1568
. Kwa Kilatini anaitwa
Doctor Angelicus
(
Mwalimu wa Kimalaika
) au
Doctor Communis
(
Mwalimu wa wote
).
Ni
msimamizi
wa
wanateolojia
,
wanachuo
, watoaji na wauzaji wa vitabu,
wanafunzi
na
shule
.
Sikukuu
yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe
28 Januari
[1]
.
Alizaliwa na Landolfo,
sharifu
mwenye asili ya
Kilombardi
, na
mke
wake, Teodora, katika
ngome
ya
familia
yao.
Akiwa mtoto wa miaka 5 tu, alitumwa kuishi na
Wabenedikto
katika
abasia
jirani ya
Monte Cassino
ili apate malezi ya msingi kwa
watawa
.
Alipofikia umri wa miaka 14 alihamia
Napoli
,
mji mkuu
wa
Ufalme wa Sicilia
, aliposoma katika
chuo kikuu
maarufu kilichoanzishwa na
Kaisari Federiko II
. Humo mawazo mbalimbali kama yale ya Aristotle yalifundishwa bila vizuio vilivyokuwepo sehemu nyingine.
Basi, Thoma alianza kutambua
thamani
ya falsafa ya
Mgiriki
huyo iliyokuwa imesahaulika kwa muda mrefu lakini wakati huo ilikuja kujulikana upya kupitia wafafanuzi wake wa
Kiarabu
,
Avisena
na
Averoe
.
Ilikuwa na mpango mzima wa mawazo kuhusu
ulimwengu
,
roho
na
maadili
ambao ulikamilika
kabla ya Kristo
kwa kutumia
akili
tu, na ambao ulionekana kujitosheleza na kuridhisha kama mtazamo sahihi.
Jambo lingine muhimu la miaka hiyo ni kwamba alikuwa karibu na
konventi
ya
Mt. Dominiko
akavutiwa na
karama
ya shirika lililoanzishwa na mtakatifu huyo. Ingawa alipingwa sana na
familia
, mwaka
1244
aliamua kujiunga na
Wadominiko
.
Ngome ya
Monte San Giovanni Campano
, ambapo kijana Thoma alifungwa asiweze kufuata wito wa kitawa.
Wakubwa wa shirika, kisha kuhisi ukuu wa akili yake, walimtuma
Paris
aweze kukamilisha masomo yake, lakini kabla hajafika huko alikamatwa na wanafamilia na kufungwa katika ngome ya baba yake huko
Monte San Giovanni Campano
alipokaa mwaka mzima, akishinikizwa aoe.
Hatimaye, akiwa amefikia
umri
wa kujiamulia maisha, alitoroka au alifunguliwa kwa ombi la
Papa Inosenti IV
.
Baada ya kukaa kidogo Napoli na
Roma
, alifika
Paris
(
Ufaransa
) ili kufundishwa na
Alberto Mkuu
,
mwanasayansi
,
mwanafalsafa
na
mwanateolojia
wa shirika lake.
Mapema walianza kuheshimiana na kupendana, hivyo mwaka
1248
Thoma alimfuata Alberto
Cologne
(
Ujerumani
) alipokuwa ametumwa na viongozi wa shirika aanzishe kituo cha teolojia.
Baadaye, Thoma aliamua kutekeleza mpango wa mwalimu wake wa kulinganisha
Ukristo
na
falsafa
ya Aristotle iliyokuwa inazidi kuathiri
Ulaya Magharibi
na
ustaarabu
wake uliotegemea
imani
, ingawa wengine waliipinga falsafa hiyo, hasa kwa sababu wafafanuzi wake wa Kiarabu walikuwa wameipendekeza tofauti, wakisema, k.mf. kwamba ulimwengu ni wa
milele
kama
Mungu
.
Hapo Thoma alifanya jambo la maana sana kwa
historia
yote ya falsafa, teolojia na
elimu
kwa jumla: kusoma kikamilifu vitabu vya Aristotle na vya wafafanuzi wake, kisha kujipatia
tafsiri
mpya kutoka
Kigiriki
ili asitegemee tu walivyoelewa
Waarabu
hao.
Hapo alifafanua mwenyewe sehemu kubwa ya maandishi ya Aristotle, akitofautisha kweli za kudumu zilizomo, mambo yanayotia
shaka
na yale yasiyo sahihi kabisa, akionyesha yanavyolingana na
Ufunuo
wa Kimungu na jinsi yanavyoweza kutumika katika teolojia ya Kikristo.
Kifupi, Thoma alithibitisha hivyo
ulinganifu
wa imani na
hoja
za
akili
, wakati ambapo hizo mbili zilionekana kupingana moja kwa moja, hata kusababisha watu wajione ni lazima waachane na imani na kufuata akili.
Kwa
usanisi
huo, Thoma aliunda msimamo wa
karne
zijazo, kwamba kweli haziwezi kupingana kamwe; ikionekana hivyo maana yake ama akili imekosea katika hoja zake, ama kinachodaiwa kuwa
ukweli
wa imani hakifundishwi nayo.
Kutokana na
vipawa
vyake kuanzia mwaka
1252
aliitwa kufundisha teolojia kwenye
Chuo kikuu cha Paris
, akianza kama
baccalarius biblis
, na baada ya miaka 4 aliweza kufundisha kama
profesa
.
Wakati huo Thoma alianza kazi ya kutunga vitabu ambayo aliendelea nayo hadi karibu na
kifo
na ambayo ni ya ajabu hata tukizingatia kwamba alisaidiwa na
karani
kadhaa, kati yao akiwemo hasa rafiki yake
Rejinaldo wa Piperno
.
Alipinga falsafa ya wafuasi wa
Mwarabu
Averroe
waliosema
imani
haiwezi kupatana na
akili
: "Imani ni kwa watu wanyofu, falsafa ni kwa wasomi".
Thoma alipambana pia na
Waagustino
ambao walifuata falsafa ya
Plato
hata kusema ile ya Aristoteli haipatani na imani.
Mwaka
1259
alihiriki
mkutano mkuu
wa shirika huko
Valenciennes
, akaingizwa katika jopo la kupanga masomo ya Wadominiko wote.
Baadaye alirudi Italia na kushirikiana na
Papa Urbano IV
, akiishi kwenye konventi ya
Orvieto
(
1261
-
1265
).
Kwa agizo lake, Thoma alitunga au kupanga matini ya
liturujia
yote ya sikukuu mpya ya
Corpus Domini
(
Mwili na Damu ya Kristo
) iliyoanzishwa tarehe
8 Septemba
1264
. Kati ya matini hayo, ambamo zinajitokeza imani na
hekima
yake, maarufu zaidi kimataifa mpaka leo ni utenzi
Pange Lingua
, hasa sehemu ya mwisho inayoanzia na maneno
Tantum Ergo
(
Sakramenti Kubwa Hiyo
).
Waliomfahamu walisisitiza
heshima
yake kwa
fumbo
la
Ekaristi
; pengine alikuwa akiegemeza
kichwa
chake penye
tabenakulo
, kama kwa kusikia mapigo ya
Moyo wa Yesu
na kupata majibu ya maswali magumu aliyojiuliza. Akiadhimisha
Misa
aliweza akalia ma
chozi
ya
huruma
,
furaha
na
shukrani
kwa
Bwana
aliyejitoa
kafara
kwa ajili ya
binadamu
. “Kwa kuwa hii ndiyo
sakramenti
ya
Mateso
ya Bwana wetu, ndani yake ina
Yesu
aliyeteseka kwa ajili yetu. Basi, tokeo lolote la Mateso ya Bwana wetu ni pia tokeo la sakramenti hii.”
Halafu alihamia Roma (
1265
-
1268
) ili kuongoza
chuo
cha
Mt. Sabina
; ila katikati, mwaka
1267
Papa Clemens IV
alimuita kwake
Viterbo
, alipohubiri mara nyingi katika
kanisa
la
Santa Maria Nuova
.
Akiwa Italia ndipo alipoandika vitabu vingi kama vile
Summa contra gentiles
,
De regimine principium
,
De unitate intellectus contra Averroistas
na sehemu kubwa ya kazi yake bora,
Summa Theologiae
, inayotumika hadi leo katika
teolojia
kama ilivyoagizwa na
Mtaguso II wa Vatikano
katika
hati
mbili,
Optatam Totius
na
Gravissimum Educationis
.
Mwaka
1269
alirudishwa Paris; huko wanafunzi wake walikuwa wengi hata kujaza kabisa
ukumbi
; mmojawao alishuhudia kwamba, “kumsikiliza kulimjaza
heri
ya dhati”. Hata waliompinga walikiri mafundisho yake ni bora na yanasahihisha yale ya walimu wengine.
Huko akaanza pia kutetea kiteolojia
mashirika ya ombaomba
na kupinga
Uplato mpya
wa Waagustino.
Mwaka
1272
, akiitwa na mfalme
Karolo I wa Angio
, alirudishwa Napoli na kupanga upya masomo ya teolojia kwenye chuo kikuu karibu na konventi yake asili. Huko alijitosa pia kuhubiria watu wa kawaida, nao walimiminika kumsikiliza. Mahubiri ya
Kwaresima
yake ya mwisho, aliyoyatoa katika
kanisa
la San Domenico Maggiore, yametunzwa kwa jina la “Opusculi” (yaani “Vijitabu”). Humo tunasoma alivyofafanua kwa usahili
Kanuni ya Imani ya Mitume
, [[sala++ ya
Baba Yetu
,
Amri Kumi
na sala ya
Salamu Maria
.
Kwa mfano, kuhusu imani, alieleza thamani yake: kwa njia yake roho inaungana na Mungu na kuzaa
uzima wa milele
; maisha yanapata mwelekeo wa kufaa, nasi tunashinda vishawishi kwa urahisi.
Dhidi ya hoja ya kwamba imani ni
upumbavu
kwa sababu inamfanya mtu asadiki kitu kisichofikiwa na
hisi
zake, Thoma alijibu kwamba akili yetu ina mipaka, haiwezi kujua yote. Ingeweza kufahamu kikamilifu mambo yote yanayoonekana na yasiyoonekana, hapo tu ingekuwa upumbavu kukubali ukweli fulani kwa imani. Kumbe hatuwezi kuishi bila kutegemea
ushahidi
wa wengine kila tunaposhindwa kujua kitu wenyewe. Kama ni hivyo, basi, inafaa tumsadiki Mungu anayejifunua na pia ushahidi wa
Mitume wa Yesu
. Ni kati ya maajabu ya historia kwamba mapema watu wengi wenye
mali
na hekima waliwasadiki hao watu wachache,
fukara
na wanyofu waliovunjwa
moyo
na
kifodini
cha mwalimu wao. Lisingetokea kama wasingekutana naye mfufuka.
Thoma alieleza pia kwamba
tafakuri
juu ya
umwilisho
wa
Mwana wa Mungu
inaimarisha imani na
tumaini
kwa wazo la
ujio
wake kati yetu kama mmojawetu kwa lengo la kuwashirikisha watu
umungu
wake; pia inachochea
upendo
kwa sababu hakuna
ishara
wazi zaidi ya upendo wa Mungu kuliko kumuona
Muumba
wa ulimwengu kujifanya
kiumbe
kama sisi; hatimaye inawasha
hamu
ya kumfikia
Kristo
katika
utukufu
: “Kama
ndugu
wa
mfalme
angeishi mbali sana naye, bila shaka angetamani kuishi karibu naye. Basi, Kristo ni ndugu yetu; kwa hiyo tunapaswa kutamani tuwe naye na kuwa moyo mmoja naye”.
Akifafanua Baba Yetu, alionyesha ni sala kamili kutokana na kuwa na
sifa
tano zinazohitajika: tumaini tulivu, maombi ya kufaa,
mpangilio
mzuri wa maombi,
ari
ya upendo na
unyofu
wa
unyenyekevu
.
Kuhusu
Bikira Maria
, alimuita “Triclinium totius Trinitatis”, yaani “mahali ambapo
Utatu Mtakatifu
unastarehe”, kwa maana
Nafsi
tatu za Mungu hazifurahii kukaa ndani ya mtu yeyote kuliko ndani ya roho yake iliyojaa neema.
Miezi ya mwisho ya maisha yake iliathiriwa na
tukio
la pekee lililofanya azidi kuzama katika tafakuri. Ni kwamba tarehe
6 Desemba
1273
, katika kanisa la Mt. Dominiko, alitoka nje ya nafsi yake na tangu siku hiyo aliacha kuandika, akimueleza kwa unyenyekevu ndugu
Reginaldo wa Piperno
, msaidizi na muungamishi wake: ≪Yale yote niliyoyandika naona ni fungu dogo la majani makavu kulingana na yale ambayo nimeyaona na kufunuliwa. Ndio mwisho wa kuandika kwangu na natumaini umekaribia pia mwisho wa maisha yangu≫.
Ndiyo sababu
Summa Theologiae
haikukamilika (inaishia kwenye mada ya
Kitubio
) baada ya kukabili ma
suala
512 katika hoja 2,669 kwa kuchimba mafundisho ya
Biblia
na ya ma
babu wa Kanisa
, hasa
Augustino wa Hippo
).
Ukurasa wa
Summa theologiae
Humo Thoma anazingatia kwanza kwamba Mungu yupo kwa namna tatu: 1) ndani mwake, akiwa
asili
na
lengo
la vyote, hivi kwamba viumbe vyote vinatokana naye na kumtegemea; 2) kwa njia ya
neema
katika
uhai
na
utendaji
wa watu anaowatakasa; 3) kwa namna ya pekee kabisa katika nafsi ya Kimungu ya
Mwana
iliyounganika kweli na ubinadamu wa Yesu na inayotenda katika sakramenti zinazotokana na kazi yake ya
ukombozi
.
Ndiyo sababu kitabu hicho kikubwa kimegawanyika katika sehemu tatu: “Kwa kuwa lengo kuu la teolojia ni kufundisha
ujuzi
wa Mungu, si tu jinsi alivyo mwenyewe, bali pia kama asili na lengo kuu la vitu, na hasa la viumbe wenye akili, ilivyo wazi katika yale tuliyoyasema tayari, basi tutafafanua: 1) Mungu; 2)
maendeleo
ya kiumbe mwenye akili kumuelekea Mungu; 3) Kristo ambaye kama mtu ndiye
njia
yetu kwa Mungu”.
Ni kama
duara
inayorudi ilipoanzia: Mungu alivyo anajitokeza kwa nje na kutushika
mkono
hivi kwamba pamoja na Kristo tumrudie yeye na kuungana naye awe yote katika wote.
Sehemu ya kwanza ya Summa Theologiae inamchunguza Mungu mwenyewe, fumbo la Utatu na kazi yake ya kuumba. Humo tunakuta tafakuri ya dhati juu ya mtu pia, kama kiumbe aliye
tunda
la upendo wake. Uhai wetu unamtegemea Mungu, lakini ni wa kweli kwa sababu yeye ametaka kututia thamani.
Sehemu ya pili inazidi kumzingatia mtu ambaye, akisukumwa na neema, anatamani kumjua na kumpenda Mungu ili awe na heri sasa na milele. Thoma anafafanua kiteolojia matendo maadilifu, ambayo yanachangiwa na akili,
utashi
na
maono
ya mtu, pamoja na
uwezo
wa neema ya Mungu kupitia maadili na
vipaji vya Roho Mtakatifu
, mbali ya msaada wa
sheria
yake. Kwa msingi huo, Thoma anamchora mtu ambaye anaongozwa na
Roho Mtakatifu
na hivyo kuwa mfano wa Mungu. Hapo anasimama kufafanua maadili matatu ya Kimungu na zaidi ya maadili hamsini ya kiutu, yanayotegemea ma
adili bawaba
manne. Hatimaye anatakari juu ya miito mbalimbali yaliyopo ndani ya Kanisa.
Sehemu ya tatu inachunguza fumbo la Kristo, aliye njia na ukweli, ambalo linatuwezesha kumfikia
Mungu Baba
. Humo Thoma anaeleza vizuri ajabu umwilisho na Mateso ya Yesu, akiongeza maelezo marefu kuhusu sakramenti ambazo Kristo anatushirikisha faida ya ukombozi. Akitumia vitu alivyochagua, anatugusa mpaka ndani.
Asubuhi
moja, Thoma alipokuwa anasali mbele ya
msalaba
wa
kikanisa
cha
Mt. Nikola
mjini Napoli, mtunza
sakristia
Dominiko wa
Caserta
alisikiliza maongezi yake na Yesu. Thoma alikuwa anauliza kwa
fadhaiko
kama aliyoyaandika kuhusu mafumbo ya imani ni sahihi au sivyo. Msulubiwa alimjibu: “Umeandika vema juu yangu, Thoma. Unataka
tuzo
gani?” Hapo Thoma alisema, “Si kitu kingine, ila wewe mwenyewe”.
Mnamo Januari
1274
Papa Gregori X
alimuagiza ashiriki
Mtaguso wa pili wa Lyon
, na Thoma akafunga safari ingawa hali yake haikuwa nzuri.
Alilazimika kusimama kwenye ngome ya
Maenza
, lakini alipoona hali inazidi kuwa mbaya asiweze kufikia konventi ya shirika, akitaka kufia
monasterini
, aliagiza aletwe kwenye
abasia
ya
Wasitoo
ya Fossa Nuova (leo
Fossanova
, karibu na
Priverno
), ambapo alifariki baada ya wiki chache.
Masalia yake yanatunzwa katika konventi ya Wadominiko des Jacobins huko
Tolosa
(
Ufaransa
).
Super Physicam Aristotelis
, 1595
Sababu
si mafundisho yake tu, bali
mbinu
alizozitumia katika kusanisi falsafa na teolojia bila kuzichanganya kama ilivyotokea kabla yake. Falsafa kama ile ya Aristotle iliweza kujitegemea katika hoja zake, badala ya kumezwa na teolojia ambayo ilitegemea imani katika Ufunuo wa Mungu na kuja kukamilisha falsafa pale ambapo hiyo haiwezi kufika.
Msingi
wa hakika hiyo ya Thoma ni kwamba falsafa na teolojia vilevile zinatokana na chanzo cha kweli zote, ambacho ni
Neno wa Mungu
, aliyehusika na kazi ya uumbaji na ya ukombozi pia. Ingawa
fani
hizo zinafuata
taratibu
tofauti katika kulenga ujuzi sahihi, hazitakiwi kutengana, bali kushirikiana.
Kadiri yake, kwa mfano, akili ya binadamu kwa njia ya hoja inaweza kufikia hakika kuhusu uwepo wa Mungu mmoja, ila imani tu, kwa kupokea Ufunuo kutoka juu, inaweza kuchota katika fumbo la Upendo wa Mungu Utatu.
Wakati imani inakamilisha ujuzi wa akili, hoja pia inasaidia imani kwa namna tatu: “kwa kuthibitisha kweli zinazoandaa kusadiki; kwa kufafanua wazi zaidi kweli za imani kwa njia ya mifano kadhaa; kwa kupinga wale wanaosema dhidi ya imani, ama kwa kuonyesha
kauli
zao ni za
uongo
, ama kwa kuonyesha si hakika kuwa za kweli”.
Ulinganifu huo wa msingi kati ya hoja za akili na imani ya Kikristo unajitokeza tena katika wazo lingine muhimu la Thoma: kwamba neema ya Mungu haibatilishi
umbile
la binadamu, bali inalitumia na kulikamilisha. Hiyo ni kwa sababu, hata baada ya kutenda
dhambi
, umbile hilo halijaharibika kabisa, ila limejeruhika na kudhoofika. Neema ambayo tunakirimiwa na Mungu na kushirikishwa kwa njia ya Neno aliyefanyika mwili, ni
zawadi
tu ya
hiari
yake ambayo umbile letu linaponywa, linatiwa nguvu na kusaidiwa lifikie heri ile linayotamani tu kwa dhati, hata bila kutambua na kuamua. Vipawa vyote vya mtu vinatakaswa, vinageuzwa na kuinuliwa na neema ya Mungu.
Fundisho hilo juu ya
uhusiano
wa umbile na neema ndani mwetu linatumiwa hasa katika
maadilidini
ya Thoma. Kiini chake ni
sheria mpya
ya
Injili
, ambayo ni Roho Mtakatifu, yaani neema yake wanayopewa wale wanaomuamini Kristo. Mafundisho yote ya Kanisa kuhusu imani na maadili yameunganika na neema hiyo ambayo ni ya msingi katika kuishi kwa
uadilifu
: kutoka kwake yanapatikana maadili ya Kimungu na ya kiutu. Hivyo Wakristo wote wanaweza kufikia
ukamilifu
uliopendekezwa na Yesu katika
hotuba ya mlimani
, ikiwa wanaishi naye katika uhusiano wa imani na wako wazi kupokea kazi ya Roho Mtakatifu.
Pamoja na hayo, “ingawa neema ina nguvu kuliko umbile, hata hivyo umbile linamhusu mtu zaidi, na kwa hiyo ni la kudumu zaidi”. Ndiyo maana kuna nafasi kwa hoja za akili katika kutambua maadili yanayodaiwa na
utu
kwa jinsi ulivyo. Akili inaweza kuyatambua kwa kutofautisha yanayofaa na yasiyofaa kufikia ile heri inayotamaniwa na mioyo yetu.
Hayo yanahusika pia na ma
jukumu
kwa ajili ya wengine, mmojammoja na kwa jumla (
ustawi wa jamii
). Watungasheria wanapaswa kuzingatia hayo katika kazi yao ya kuratibu
maisha ya jamii
. Ndio msingi wa kuorodhesha na kutetea
haki za binadamu
. Si ajabu kwamba fundisho la
hadhi
ya nafsi ya mtu, inayomfanya kila mmoja awe na
haki
za msingi kwa sababu tu ni mtu, lilistawi kwanza kati ya waliozingatia
urithi
wa Thoma katika kuthamini umbile letu: “ndilo lililo kamili kuliko yote yanayopatikana ulimwenguni, yaani mmoja anayeishi akiwa na akili”.
Basi, Thoma alipendekeza mtazamo mpana na lenye tumaini kuhusu akili ya binadamu. Mpana kwa sababu hauishii katika ujuzi wa
sayansi
zinazotegemea
upimaji
wa vitu vinavyoonekana, bali unakabili yote yaliyopo, kuanzia Mungu, na hivyo unahimizwa kutafuta maana ya maisha yetu. Lenye tumaini kwa sababu akili, hasa ikiangazwa na imani ya Kikristo, inapigania ustaarabu ambao unathamini hadhi ya kila mtu, unatetea haki zake pamoja na kumhimiza kuwajibika kwa wengine.
Dhati ya mawazo ya Thoma ilitokana daima na maisha yake ya imani na sala yaliyojitokeza katika maneno kama haya: “Ee Bwana, Mungu wangu, unijalie akili ya kukufahamu, moyo wa kukutafuta, hekima ya kukupata,
mwenendo
wa kukupendeza,
udumifu
mwaminifu katika kukutarajia, na tumaini la kukukumbatia mwisho”.
Mungu wa wema wote, utujalie tutamani motomoto, tutafute kwa busara, tujue kwa hakika na kutekeleza kikamilifu matakwa yako matakatifu kwa utukufu wa jina lako.
- Ad Bernardum
- Aurora Consurgens
- Compendium theologiae
- Contra errores Graecorum
- Contra impugnantes Dei cultum
- Contra retrahentes
- Contra Saracenos
- De aeternitate mundi
- De alchemia
- De anima
- De articulis Fidei
- De ente et essentia
- De forme absolutionis
- De lapide philosophico
- De malo
- De motu cordis
- De operationibus occultis
- De perfectione
- De potentia
- De principiis naturae
- De rationibus Fidei
- De regimine principum
- De spiritualibus creaturis
- De substantiis separatis
- De unione Verbi Incarnati
- De unitate intellectus contra Averroistas
- De veritate
- De virtutibus
- Summa contra Gentiles
- Summa theologiae
- GEROLD SCHMID, Toma na Marieta ? ed. Benedictine Publications Ndanda-Peramiho ? Peramiho 1978
- Shughuli au kuhusu Thomas Aquinas Mtakatifu
katika maktaba ya WorldCat catalog
- Complete works of St. Thomas Aquinas
in
(Kilatini)
and
(Kiingereza)
side by side
- Corpus Thomisticum
? his complete works in
(Kilatini)
- Documenta Catholica Omnia
? his complete works in PDF files, in
(Kilatini)
,
(Kiitalia)
,
(Kiingereza)
,
(Kijerumani)
,
(Kihispania)
,
(Kifaransa)
,
(Kireno)
- Summa contra Gentiles
- Summa Theologica
- The Principles of Nature
Archived
5 Desemba 2004 at the
Wayback Machine
.
- On Being and Essence
Archived
27 Novemba 2014 at the
Wayback Machine
.
(
De Ente et Essentia
)
- Catena Aurea
(partial)
- Works by Thomas Aquinas
katika Project Gutenberg
- Bibliotheca Thomistica IntraText
: texts, concordances and frequency lists
- An Aquinas Bibliography
- St Thomas' Multilanguage Opera Omnia
- Thomas Aquinas in English
- De Magistro
Archived
12 Mei 2012 at the
Wayback Machine
. (
On the teacher
q. 11, a.1 of
de Veritate
)
- Writings of Thomas Aquinas in Article Form at PhilosophersAnswer.com
Archived
24 Agosti 2011 at the
Wayback Machine
.
- Online Galleries, History of Science Collections, University of Oklahoma Libraries
Archived
16 Mei 2012 at the
Wayback Machine
. High resolution images of works by Thomas Aquinas in .jpg and .tiff format.
- "St. Thomas Aquinas"
katika
Catholic Encyclopedia
- Opera omnia
- Summa theologiae
- Thoma katika Kamusi elezo ya Falsafa kwa
Kiingereza
- Thoma katika Stanford Encyclopedia of Philosophy
- Opera omnia
katika
Kilatini
na tafsiri 6