Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nchi lindwa
ni
dola
au eneo lililokubali kukabidhi sehemu za
mamlaka
yake mikononi mwa nchi kubwa na yenye nguvu. Sehemu za mamlaka zinazotekelezwa na nchi nyingine mara nyingi ni
siasa ya nje
au mambo ya
usalama
na
jeshi
.
Hali ya nchi lindwa wakati mwingine ilikuwa na tofauti ya jina tu na
koloni
, lakini mara nyingi ilikuwa na tofauti kadhaa kweli.
Kwa kawaida nchi lindwa ni nchi ndogo au nchi hafifu inayopokea
ahadi
ya nchi mlinzi ya kuitunza na kuitetea au kusaidia katika shughuli mbalimbali. Uhusiano huu umejulikana katika
mawasiliano
ya kimataifa tangu
karne
nyingi. Kimsingi uhusiano wa
ulinzi
wa aina hiyo umetambuliwa katika
haki ya kimataifa
.
Zote mbili ni eneo chini ya mamlaka ya nchi ya nje. Tofauti ni kwamba koloni liko kabisa chini ya
utawala
wa nje. Nchi lindwa iko katika hali yake kwa sababu imekubali kulindwa ama kwa
hiari
yake au kwa sababu ililazimishwa kukubali. Koloni ni mali ya nchi ya nje, lakini nchi lindwa imetambuliwa kama nchi ya pekee. Kwa kawaida nchi lindwa huratibu
siasa yake ya ndani
na nchi mlinzi inaangalia mambo yake ya nje.
Mifano ya kinyume ni makoloni ya
Ujerumani
yaliyochukuliwa baada ya
Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia
na mataifa washindi kama
Ufalme wa Maungano
(Uingereza) au
Ufaransa
. Nchi hizo kama
Tanganyika
ziliendelea kutawaliwa kama makoloni mengine lakini kwa niaba ya
Shirikisho la Mataifa
.
Kuna mifano kadhaa ambako nchi kubwa imekubali kutunza nchi ndogo.
- Mfano wake ni
Andorra
ambayo ni nchi ndogo sana katika
bonde
la
milima ya Pirenei
kati ya
Hispania
na
Ufaransa
. Inawezekana kusema nchi hii ndogo iko kwa sababu majirani makubwa wamesahau kuimeza nyakati mbalimbali katika
historia
na kwa jumla hawakupenda kuiachia nchi jirani. Eneo lake ni dogo mno, haliwezi kugawiwa. Tena si hatari kwa majirani. Hivyo majirani wote wakubwa wamepatana kulinda usalama wake.
- Nchi ya
Visiwa vya Cook
ilikuwa nchi lindwa chini ya
New Zealand
na uhusiano huo umebadilika kuwa "ushirikiano wa hiari" ambao hali halisi bado ni aina ya ulinzi isipokuwa Visiwa vya Cook vina haki ya kujiondoa wakati wowote. Visiwa havina
jeshi
ila
polisi
tu. Usalama wake umetegemea New Zealand. Kinadharia Visiwa vinaweza kuwasiliana na nchi za nje lakini hali halisi vinaweza kuwa na
balozi
mbili
pekee, moja huko New Zealand na moja kwa
Umoja wa Ulaya
, halafu
idadi
ya
makonsuli
. Kwa jumla kama mawasiliano na nchi za mbali ni ya lazima yanafanyika kupitia balozi za New Zealand.
Wakati wa
karne ya 19
ilijitokeza aina nyingine ya nchi lindwa. Wakati ule
uwezo wa kijeshi
na wa kiuchumi wa nchi za
Ulaya
uliwezesha nchi hizo kulazimisha maeneo mapana ya
Asia
na hasa
Afrika
kukubali ubwana wao.
Ukoloni
ulianza wakati mwingine polepole.
Nchi zenye makoloni kama Uingereza ziliona
faida
kama zifuatazo kuingia katika uhusiano wa ulinzi badala ya kuunda koloni moja kwa moja:
- kupata
mabandari
na vituo vya kijeshi katika nchi fulani bila kugharimia utawala wa nchi yote
- kuzuia nchi nyingine za Ulaya zisiingie katika eneo lilelile
- kuhakikisha ya kwamba
wafanyabiashara
wa nyumbani watakuwa na nafasi bora kuuza
bidhaa
zao au kununua
mazao
ya nchi
- kutumia jeshi la nchi dhidi ya majirani yasiyoshirikiana
- kuzuia watawala wa nchi lindwa kuanza
vita
katika sehemu yao, hivyo kupunguza
gharama
za usimamizi wa eneo kubwa zaidi
- kuwa na nafasi ya
ushirikiano
na nchi koloni nyingine kwa sababu nchi lindwa bado ilikuwa nchi ya pekee hivyo kulikuwa na uwezekano wa kuipa hata nchi nyingine nafasi fulani kiuchumi hali iliyoweza kupungua uchungu kati ya nchi koloni.
Ngazi ya kujitawala au kutawaliwa
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Hali ya nchi hizo ilikuwa na ngazi mbalimbali ya kujitawala au kutawaliwa.
- Usultani
wa
Sarawak
ulikuwa na
mkataba
na Uingereza uliosema ya kwamba usultani ulikuwa nchi huru ya pekee na Uingereza haukuwa na haki ya kujiingiza katika shughuli za ndani. Hata mawasiliano ya nje yalikuwa mikononi mwa
Sultani
. Wawakilishi wa
mfalme
wa Uingereza walitakiwa kujiandikisha katika
ofisi
ya sultani. Mtawala wa Sarawak hakuwa huru tena kuiachia nchi nyingine sehemu yoyote ya eneo lake. Vinginevyo alipaswa kushauriana na
mwakilishi mkazi
wa Uingereza lakini aliendesha siasa yake nchini.
- Opobo katika
Nigeria
ilikuwa na mkataba uliokataza kila mawasiliano au mikataba na nchi za nje.
- Sultani wa
Zanzibar
alikubaliwa kama mtawala mwanzoni wa ulinzi mnamo mwaka
1890
. Mwaka
1896
Uingereza ulingia ndani ya utawala wa Zanzibar kwa njia ya kijeshi ikamfukuza
Ali bin Said
kama sultani mpya baada ya
Khalifah bin Said
na kumpandisha
Hamad bin Thuwaini
kwenye utawala. Tangu
1906
Sultani
Ali bin Hamud
alipaswa kumpa mwakilishi mkazi Mwingereza nafasi ya
Waziri Mkuu
wake na uhusiano ulikuwa zaidi wa kikoloni kwa sababu sultani hakuweza tena kufanya azimio lolote bila mwakilishi mkazi Mwingereza kuwepo na kukubali.
- Usultani wa
Witu
ulikuwa nchi lindwa ya Ujerumani ikakabidhiwa na Wajerumani mikononi mwa Uingereza mwaka 1890; baadaye ilifanywa kuwa sehemu ya kawaida ya koloni la
Kenya
bila kujali mikataba ya awali.
Hivyo kuna mifano ambapo hali ya kuwa nchi lindwa ilikuwa kipindi kifupi tu kabla ya kumezwa kabisa na kuwa sehemu ya koloni kamili.
Lakini kuna pia mifano ambapo mapatano ya awali yaliheshimiwa, kwa mfano kwenye
Falme za Kiarabu
zilizorudishiwa mamlaka yote mnamo mwaka
1970
.