Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Namba sanifu ya kimataifa ya vitabu (ISBN) kwa mwandiko wa tarakimu na msimbo pau
Namba sanifu ya kimataifa ya vitabu
(
en:International Standard Book Number
) inayojulikana kwa kifupi chake cha
ISBN
ni namba ya kipekee ya utambulisho wa
vitabu
viuzwavyo kibiashara.
Inasaidia kujua kwa uhakika ni kitabu kipi kinachoagizwa na mteja na kutumwa kutoka wachapishaji kwenda dukani.
ISBN inapangwa kwa kila toleo na tofautisho (isipokuwa marekebisho) la
kitabu
. Kwa mfano, Kitabu cha kielektroniki, paperback na toleo gumu (hardcover) la kitabu kilekile kila moja itakuwa na ISBN tofauti. ISBN ina
urefu
wa tarakimu 13 kama iliwekwa kuanzia tarehe
1 Januari
2007
, na urefu wa tarakimu 10 kama iliwekwa kabla ya mwaka 2007.
Namna ya kuweka ya ISBN inategemea
taifa
lenyewe na hutofautiana kutoka
nchi
hadi nchi, mara nyingi inategemea na ukubwa wa sekta ya
uchapishaji
ndani ya nchi. Kila namba inaweza kuonyeshwa kwa
tarakimu
au
msimbo pau
.