Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Meles Zenawi
Meles Zenawi
(*
9 Mei
1955
-
20 Agosti
2012
) alikuwa
Waziri Mkuu
wa
Ethiopia
tangu
22 Agosti
1995
hadi kifo chake. Alitangulia kuwa rais wa nchi kati ya
28 Mei
1991
na
22 Agosti
1995
. Alifuatwa na makamu wake
Haile Mariam Desalegne
.
Zenawi alikuwa mwanafunzi wa
tiba
kwenye
chuo kikuu
cha
Addis Ababa
wakati wa
mapinduzi ya kikomunisti ya Ethiopia
ya mwaka
1974
. 1975 aliacha masomo akarudi kwake Tigray akajiunga na
Harakati ya Ukombozi wa Tigray TPLF
iliyopinga serikali mpya. Tangu 1985 aliongoza TPLF.
1989 alikuwa mwenyekiti wa ushirikiano wa TPLF na vikundi vingine vya upinzani kutoka sehemu mbalimbali za Ethiopia.
Baada ya kupinduliwa kwa serikali ya kikomunisti ya
Mengistu
katika Mei 1991 Zenawi aliteuliwa kuwa Rais.
1995 katiba ilibadilishwa. Cheo cha
Waziri Mkuu
kilikuwa cheo chenye uzito kuliko
rais
na Zenawi alihamia katika ofisi ya waziri mkuu.
Meles Zenawi ameshika shahada ya MA ya utawala wa biashara kutoka Uingereza na MSc ya uchumi kutoka Uholanzi.
Amemwoa Azeb Mesfin; wana watoto watatu. Inasemakana Meles anapenda kusoma, kuogelea na tennis.